Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI NZITO: WABUNGE UKAWA MATATANI ZAIDI KUMSHIKA ''MATITI'' KATIBU TAWALA..

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru wabunge wa Ukawa na makada wao waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando.

Hakimu Mkazi Mkuu,Huruma Shaidi amewaachia huru leo wabunge hao  baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibu.

Hakimu Shaidi amesema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka  umeshindwa kuthibisha, hata  mlalamikaji Mmbando hakumbuki ni nani alimjeruhi.

Ushahidi wake ulielezea jinsi washtakiwa walivyojishughulisha na nyaraka siku ya tukio na siyo kumjeruhi.

Kuhusu kushikwa matiti, Hakimu Shaidi alisema;

 “Sijui alishikwa matiti na nani?”

 Kutokana na  ushahidi huo Hakimu  aliwaachia huru washtakiwa wote kwa kuwa hawana kesi ya kujibu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top