Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KUTOKA IKULU: KWELI HUYU MZEE HATARI HII NDIO KAULI YENYE UJUMBE MZITO KWA AJALI YA WANAFUNZI HAPO JANA..

Rais John Magufuli ametoa salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki kwa vifo vya wanafunzi, walimu na dereva vilivyotokea leo saa 3.00 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Rais Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo hivyo  vya wanafunzi 32 wa darasa la saba, walimu 2 na dereva wa gari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha.

Wanafunzi na walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya msingi iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni ambako limesababisha vifo hivyo na majeruhi watatu.

Kufuatia ajali hiyo, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Gambo na kueleza kuwa ajali hiyo imezima ndoto za watoto waliokuwa wakijiandaa kulitumikia Taifa na imesababisha uchungu, huzuni na masikitiko makubwa kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla.

“Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo naomba unifikishie pole nyingi kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wote wa wanafunzi, walimu na dereva waliopoteza maisha, hiki ni kipindi kigumu kwetu sote, na uwaambie naungana nao katika majonzi na maombi.

“Muhimu kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira, ustahimilivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,” amesema Rais Magufuli.

SAD NEWS: INASIKITISHA MNO UNDANI WA AJALI MBAYA YA WANAFUNZI ILIYOTOKEA HIVI PUNDE '''BONDENI KARATU'''


Basi aina ya Toyota Coaster lililobeba wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ya Arusha limetumbukia bondeni Karatu. 
Zaidi ya watoto 20 na waalimu wanahofiwa kufa. 
Walikuwa wakienda tour kwenye hifadhi ya Ngorongoro. 
Ni ajali kubwa na mbaya kuwahi kutokea tangu ya miaka 7 iliyopita. 
Pole sana kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza watu wao katika ajali hii mbaya, Mungu azilaze roho za marehemu peponi

HABARI NZITO YA KUSIKITISHA: BASI KAMPUNI YA SARATOGA LATUMBUKIA MTONI LIKIWA NA ABIRIA ZADI YA 50 TAZAMA TUKIO HILI LA AJALI HAPA.

saratoga
Takribani watu 50 wanusurika kifo baada ya basi la Kampuni ya Saratoga kupoteza mwelekeo na kutumbukia katika mto Malagarasi Mkoani Kigoma.
– Mashuhuda wamesema basi hilo limetumbukia mtoni baada ya kivuko kutia nanga na abiria kushuka. Hivyo wameiomba Serikali kujenga daraja katika eneo hilo
Zaidi ya abiria 50 waliokuwa wakisafiri kutoka vijiji vya mwambao wa kusini katika ziwa Tanganyika tarafa ya Buhingu wilayani Uvinza mkoani Kigoma wamenusurika kufa baada ya basi aina ya Saratoga walilokuwa wakisafiria kuelekea mjini Kigoma kutumbukia katika mto Malagarasi wakati basi hilo na abiria wengine wakivushwa katika kivuko cha mto huo.
Mashuhuda wa tukio hilo pamoja na nahodha wa kivuko cha MV Malagarasi wamesema basi hilo lenye namba za usajili T 938 AGQ limetumbukia mtoni baada ya kivuko kutia nanga upande wa pili baada ya kurudi nyuma taratibu huku abiria wote wakiwa wameshuka na kwamba hilo ni tukio la tano kutokea katika eneo hilo hivyo wameiomba serikali kujenga daraja ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea.
Akizungumza katika eneo la tukio, kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema katika ajali hiyo hakuna mtu aliyepoteza maisha na kwamba jitihada zinazofanywa sasa ni wazamiaji kujaribu kulitoa majini basi hilo
Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top