Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

FAHAMA NJIA HIZI ZAKULINOGESHA PENZI LAKO KWAKE DAIMA...


KUPITIA safu hii uipendayo, leo ninakupa njia nne zitakazolifanya penzi lako liendelee kunoga, hata kama litakuwa limeanza kufubaa utaliamsha upya.

Wengi wamekuwa hawaelewi mambo mengi kuhusu uhusiano ndiyo maana huishia kulalamika kwamba wanapenda sana lakini mwisho wa siku huishia kutendwa.

Hakuna mtu ambaye hahitaji faraja, kila aliyekuwa na mpenzi wake anahitaji kuwa na furaha. Hakuna mtu ambaye anaingia kwenye mapenzi ili apate msongo wa mawazo, kila mtu anayediriki kuutoa moyo wake, kitu cha kwanza anachokitarajia ni faraja kisha furaha.

Ipo hivyo! Watu wengi wanakuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wakiwa na matumaini kwamba hao waliokuwanao inawezekana watakuwa wapenzi wa maisha yao yote. Pasipo kujua, wakati mwingine kuna makosa hufanyika, mtu hajui afanye nini ili penzi alilonalo kwa mpenzi wake linoge, hajui ni njia zipi zitamfanya kupendwa kila siku.

Leo nitakutajia njia chache ambazo kama utazifanya, nakuhakikishia penzi lenu litashamiri zaidi ya lilivyo hivi sasa.

MPE UHURU KWANZA

Kila mtu anapenda kuwa huru, kuachwa afanye mambo yake anayoyapenda. Hakuna mtu anayependa kuingiliwa, hasa kwenye masuala ya kutumia simu yake. Kama kweli unahitaji penzi linoge, usitake kuingilia mambo yake hasa katika matumizi ya simu, unachotakiwa ni kumwambia muda ambao hupendi kuona akizungumza na simu na si kwamba kila unapoona simu yake inaita, unaichukua kwa nguvu.

Mapenzi hayapo hivyo, mpe uhuru mwenza wako. Haimaanishi mtu kama hajatulia basi kuchukua simu muda wote inapoita ndiyo kutamfanya kutulia, hapana, bali kwa kufanya hivyo utampa mbinu nyingine ya kuweza kupambana nawe. Unachotakiwa ni kumfanya kuwa huru, usimuingilie.

CHUKUA MUDA WAKO KUMTOA ‘OUT’

Wengi hukosea hapa, huwa hawapendi kwenda matembezi na wapenzi wao. Wengine hujifanya wapo bize, hata ukimwambia Jumamosi nataka tutoke out atakwambia anataka kufanya hili na lile.

Rafiki yangu, kila mtu anahitaji kuwa karibu na mpenzi wake, hakuna anayependa kuwa na mpenzi ambaye muda wote yupo bize tu. Mchukue, nenda naye sehemu. Kutoka mitoko ya mara kwa mara itawafanya muwe karibu zaidi, itawafanya muda wote mzidi kupendana, ila kama utajifanya upo bize, jua kuna mtu ataitumia nafasi hiyo kutoka na umpendaye.

PENDELEA KUFANYA UTANI

Hakuna mtu anayempenda mpenzi ambaye yupo siriazi saa ishirini na nne. Pata muda wa kukaa na kutaniana naye. Mchombeze kwa vineno vya utani, mpetipeti, mlaze kitandani na uanze kupiganapigana naye vibao vya kimahaba hata kwa kutumia mito ya kulalia.

Unapokuwa siriazi kila wakati inakuwa ni vigumu mwenzako kulifaidi penzi, pendelea kutabasamu inapobidi kila unapokuwa na mpenzi wako, siyo kila atakachokwambia wewe uso wako umekunja ndita kiasi kwamba ataonekana kukuogopa na kumtafuta mtu mwingine ambaye atahitaji kuliona tabasamu lake, atahitaji kuona akifanyiwa utani wa mahaba nk.

HEBU MSIFIESIFIE BASI

Wengi wanaogopa kuwasifia wapenzi wao, hawajui kama kila mtu duniani anapenda kusifiwa. Mpenzi wako anapovaa nguo nzuri zilizomtoa, usikae kimya, mwambie amependeza kwani hilo litamfanya kufurahi sana. Kama utakuwa na mpenzi halafu kila siku humsifii hata akifanya kitu gani, jua kwamba atajisikia vibaya, wakati mwingine atahisi hayupo sawa kwa kuwa tu hujawahi kumsifia.
Unapomsifia mpenzi wako kunamfanya kuongeza umakini katika kuvaa kwake, kununua manukato na hata jinsi atakavyosuka au kunyoa atafanya kwa ubora wa hali ya juu kwa kuwa anajua utamsifia

NOMA SANA NI KUFURU YA KARNE MSANII NISHA AKIRI YU MAPENZI NA MNYAMA HUYU...

Salma Jabu aka Nisha
WAKATI waumini wa Dini ya Kiislam wakiendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, msanii wa filamu, Salma Jabu ‘Nisha’ ametoa kali ya mwaka kufuatia kukiri kuwa na uhusiano na mbwa.

Nisha alifanya hivyo juzikati baada ya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa amevaa gauni jeupe la harusi huku mkononi akiwa ameshika mkanda wa mbwa na kuandika kuwa, mnyama huyo ndiye mpenzi wake, jambo ambalo liliwachefua baadhi ya marafiki zake.



Dada acha kukufuru halafu huu ni Mwezi Mtukufu, Kiislam mbwa ni najisi halafu wewe ni Muislam unashika mbwa na kusema ndiyo mpenzi wako, tangu lini mbwa akawa na uhusiano na binadamu?” aliandika mmoja wa mashabiki aliyeonekana kukerwa na kitendo hicho. Jitihada za kumtafuta Nisha kuzungumzia kitendo alichokifanya hazikuzaa matunda baada ya simu yake kutopokelewa na hata alipotumiwa SMS hakujibu.

MAMBO ya Kumfanyia Msichana Uweze Kumteka Asikuache Hata Kama Hujamtongoza


1. KILA siku usisahau kumsifia kwa kumwambia ni kiasi gani alivyo mzuri. Kumbuka kila msichana anapenda kusifiwa hivyo unapomuambia yeye ni mzuri anaona una mthamini kuliko msichana yeyote awaye.


2. Wakati wowote ukipata nafasi muandikie barua au msg kwenye simu mueleze hisia zako kiasi gani unampenda. Kumbuka wasichana hupenda kusikia zaidi kutoka kwa wapenzi wao ni kiasi gani wanapendwa. Haitakiwi iwe tu katika kipindi cha siku ya wapendanao ndio umuoneshe kuwa unampenda. Muoneshe msichana ni kiasi gani yeye ni muhimu sana kwako.


3. Busu la ghafla na kumshika mkono wakati mkitembea pamoja itamfanya yeye kujisikia raha zaidi. Na wakati mwingine msuprise kwa kumtembelea mara kwa mara hi humfanya akuone wewe ni mtu muhimu pale usipokuwa naye karibu na kumfanya kukuhitaji zaidi ukiwa naye mbali.


4. Tambua mahitaji yake. Uwe msaada kwake kipindi ambacho mpenzi wako amekasirika kuwa pale kwa ajili yake na ukimpooza kwa sauti ya upole na mahaba. Utashangazwa sana na kiasi gani msaada huo umeleta mabadiliko kwake. Hakikisha unamsaidia katika shida zake hapa ndipo kuna tatizo kwa wavulana wengi. Mapenzi si pesa lakini kuna kipindi ambacho pesa huitajika kulinda penzi lako. Si msichana anapokuomba pesa ina maana ana nia ya kukuchuna au amekupendea pesa kuna shida nyingine inabidi akuombe wewe tena kwa kukupima kama utakuwa tayari kumsaidia.


5. Mchukue mpenzi wako out mara nyingine itamfanya ajisikie furaha sana kwa sababu wasichana hupenda enjoyment na boyfriend zao. Hii haitamfanya mpenzi wako tu kuwa na furaha bali itawafanya nyie kwa pamoja kujuana na kufahamiana zaidi.


6. Kuwa muwazi kwake usimfiche jambo linalokuhusu. Msichana hupenda kutoa ushauri kwa mtu ampendaye hivyo unapokuwa muwazi atajisikia kuthaminiwa nawe na kukuona umemuamini.


7. Ukijiona upo busy sana usithubutu kuacha japo kumpigia simu mara mbili kwa siku hata kama ukishindwa kumpigia wakati upo ofisini darasani au kwingineko hakikisha unapopata nafasi japo ujumbe mfupi wa kumwambia unampenda.


8. Mkumbatie mara kwa mara katika tukio la kumbatizi kuna jambo kubwa sana hutokea. Si kwake tu hata kwako mvulana. Hali ya joto lenu huwaweka pamoja kifikra hata pale msipokuwa pamoja.


9. Epuka maugomvi na hasira za mara kwa mara ukiwa nae. Mwanamke hupenda ustaarabu kwa mtu ambaye yupo serious naye hivyo ukionesha hasira kabla hata hujamtongoza unaweza ukamkosa msichana hivihivi wasichana huwaogopa wavulana wenye hasira na wagomvi kwa sababu hupenda kubembelezwa.


10. Mdekeze. Msichana anapenda kudeka anaenda kudeka sana na kubembelezwa sana hivyo mvulana ukidekewa usikasirike eti huyu msichana kazidi wewe ndio wakati wako wa kumuonesha msuchana wako unampenda mdekeze mpaka aone aibu kudeka siku nyingine. Wasichana wameumbwa kwa jili ya wavulana ndio maana hudeka hii ndiyo silaha pekee na ya mwisho kumpata msichana hata kamasi wako ni wa rafiki yako unaweza ukatumia silaha hii kumpora msichana huyo kwa mwenzio usipojua kudekeza utaachwa pia

KAULI ZA HATARI KWENYE MIGOGORO YA MAPENZI...


WAKATI fulani kwenye uhusiano suala la migogoro ni la kawaida. Inaelezwa kwamba, wapenzi wanapoingia kwenye kuhitilafiana ndiyo uimara wa penzi unapotokea. 


Yeah! Matatizo hukomaza akili. Mkikaa bila kugombana ni vigumu kujua namna mwenzako alivyo hasa kama ikitokea kutoelewana baadaye.

Rafiki zangu, kugombana hakuna maana ya kumalizika kwa uhusiano hasa kwa wale walio kwenye ndoa. Mambo yanatokea, yanatatuliwa na mwisho wake maisha yanaendelea kama kawaida.


Kwa bahati mbaya sana ni kwamba, wengine wanapokuwa kwenye migogoro na wenzi wao, badala ya kutafuta njia za utatuzi, wanazalisha tatizo lingine!

Jambo la kusikitisha ni kuwa, tatizo jipya linalozaliwa linaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi katika uhusiano huo na mwisho wake kusababisha kuachana kabisa.

Ngoja tupanue mawazo yetu leo hapa kwenye All About Love. Zipo kauli ambazo ukizitoa kwa mpenzi/mke/mume wako wakati mkiwa kwenye ugomvi, zinaweza kuzalisha tatizo kubwa zaidi mbeleni.

Tutaona tu. Tuendelee kuwa pamoja.

KWA NINI KAULI?

Inawezekana ukajiuliza; ni kwa nini nimesema kauli? Rafiki zangu, kwa kawaida, watu wakiwa kwenye ugomvi, jambo kubwa linalotokea ni kutupiana maneno.

Katika hali hiyo basi, kwa wenzi au wanandoa ni vyema kuchunga ndimi zao maana zinaweza kusababisha matatizo makubwa siku zijazo. Sasa twende tukaone... 

‘HUNA AKILI’

Wako baadhi ya watu wakigombana (hasa wanaume) wamekuwa na tabia ya kuwaambia wanawake wao: “Wewe huna akili kabisa...yaani hutumii akili kabisa katika kufanya mambo yako.

“Unakurupuka tu. Sasa ishu kama hii, hata mtoto mdogo anajua ni makosa, inakuwaje wewe unakosea?”

 

Hili ni jeraha la moyo. Mwanamke ukimwambia hana akili anajisikia vibaya, unampa kovu kubwa moyoni mwake. Anajiona wa hali ya chini na anahisi ameshuka thamani yake.

Kwake, kumwambia hana akili, ataanza kuwaza kuwa yupo mwanamke mwingine ambaye kwako ana akili kuliko yeye. Ni maumivu makali sana kwake.

‘NITAKUACHA’

Baadhi ya wanaume wana ulemavu huu. Ugomvi kidogo tu, atamwambia mwenzake: “Endelea na tabia zako za hovyo, ipo siku utajuta. Nimevumilia mengi sana lakini kuna siku nitachoka.

“Hutaamini macho yako. Siyo lazima niishi na wewe. Siwezi kuendelea kuteseka nikiwa na wewe. Nitakuacha nakuambia ukweli.”

Hii ni kauli mbaya ambayo inapandikiza chuki ndani ya moyo wa mwanamke. Kwanza kwa kumwambia hivi, hata kama alikuwa hakusaliti, unamfanya aanze kufikiria kutafuta mtu mwingine wa kumliwaza.

 

Kauli hii hasa kama ukiirudia zaidi ya mara mbili, humkaa akilini mwake na huanza kuwaza kuhusu kuwa na mwanaume mwingine nje ili apate mahali ambapo hata kama ukimuacha, atapata pumziko la uhakika.

‘NAKUVUMILIA TU’

Ni kweli mapenzi ni uvumilivu. Kuvumiliana ni siri ya uhai wa ndoa nyingi lakini hilo linapaswa kubaki moyoni.

Kugombana na mwenzako halafu umwambie kuwa unamvumilia tu, inamaana kwamba kuna siku uvumilivu wako utaondoka na utafanya maamuzi magumu – kuachana!

Si kauli njema kwa mwenzi wako. Mbaya zaidi humfanya aanze kufanya maandalizi ya mtu wa kuziba nafasi yako hata kama ni kwa usaliti. 

‘KUNA SIKU UTAJUTA’

Kauli hii haina tofauti kubwa sana na iliyotangulia maana kinachofanyika hapa ni kumuandaa mwenzi wako kwa ajili ya matatizo siku zijazo.

Kumwambia: “Kuna siku utajuta, endelea na mambo yako tu, utaona.” Hii inamaanisha kwamba, uamuzi ulio ndani yako si mzuri kwake lakini ni suala la muda tu.

Ataamini (na ndivyo ilivyo mara nyingi) kuna muda ambao atajuta sana kwa sababu yako. 

Hiyo ni sawa na kutengeneza bomu unaloliandaa kulilipua muda ujao.

Bado zipo kauli zaidi ambazo zina maudhi lakini pia zinaweza kusababisha matatizo zaidi kwa mwenzi wako

UNAJUA KWA NINI MAAPENZI YA MBALI HAYA DUMU HIZI NDIZO SABABU 5.

Wengi wetu hujiuliza kwanini  maisha ya mapenzi ya mbali huwa  hayafiki mbali na kubaki wa kijiuliza tatizo ni nini? Wakati mwingine watu huanza kuulizanaa mchawi ni nani katika mapenzi yao. Laa hasha!! Huenda mchawi wa mapenzi yako ni wewe mwenyewe lakini hujui kwa sababu hakuna mtu ambaye ameshawahi kukueleza jambo hili na lile ndio tatizo

Hata hivyo hakuna kumbukumbu ambazo zinaonesha ni kwa asilimia ngapi ambazo wapenzi wanapenda kuwa mbali mbali japo mazingira mara nyingi ndo huwa chanzo

Katika tafiti mbali mbali zinaonesha kwamba umbali humaliza kabisa mapenzi ambayo  wapenzi wengi wenye malengo ya kufika mbali huwakuta.

Lakini zipo sababu mbalimbali ambazo ukizichanganua utajua kwa nini mapenzi mengi ya mbali huw hayadumu

Wivu.

Wivu huwa ni chachu ya kupima upendo lakini ukizidi pia huwa tatizo. Wivu wa mapenzi  ukizidi husababisha kutokuaminiana  kwani kila mmoja kwa wakati wake tofauti huhisi mwenzake anamsaliti, mara nyingi hali kama hii humfanya mmoja wapo kati ya wapenzi hao wawili kuona kama mwenzake ameshamchoka na anamtafutia sababu. Ni vyema kuwa na wivu kiasi kwa mpenzi wako

Mawasiliano

Mawasiliano huimarisha mapenzi na hufanya wahusika kujihisi wapo pamoja. Inapotokea kuwa na ufinyu wa mawasiliano ndipo hali ya mapenzi ya upande mmoja hupungua na kuhisi kwamba tayari mwanamke/mwanaume tayari ameshapata mwingine wakumfanya asifanye mawasiliano ya mara kwa mara.

Ugomvi

Magomvi ya mara kwa mara hufanya mmoja wenu ahisi kuchoka na mahusiano. Inapotokea sababu za  ugomvi ambao unahisi unaweza kuwa chanzo cha kuvunja mahusiano yenu ni afadhali ukazizuia na kutafuta siku nyingine ya kutatua tatizo hilo.

Kutojali

Hii mara nyingi imetajwa sana kuwa ni chanzo cha mapenzi ya mbali kuvunjika kwa sababu  tofauti mfano mpenzi wako alipokuwa karibu ulikuwa ukimpatia huduma mbalimbali kama zawadi nk, lakini anapokuwa mbali unajisahau hali hii humfanya mpenzi wako ajiulize kulikoni?

Usikivu

Nayo ni sababu ambayo ukiwauliza wengi wao ambao walikuwa na uhisiano wa mbali ukavunjika lazima atakulalamikia kwamba alikuwa hanisikilizi nachomwambia. Mfano alitaka kutoka kwenda ‘OUT’ na wenzake nikamyima lakini hajanisikiza hivyo hanifai.

Hizi huenda zikawa ni baadhi ya sababu ambazo wapenzi wengi ambao mapenzi yao hayajafanikiwa kama jinsi walivyo hitaji wamekumbana nazo.

Ili kuepuka changamoto za kutengana  na mtu ambaye unamuhitaji katika maisha yako ni vyema ukaanza kujifunza pole pole kutoka kwake ili siku ukiwa mbali naye ujue kipi mwenzako anapenda na kipi hakipendi mnapokuwa mbali.

MAPENZI: FAHAMU FAIDA HIZI MURUA KABISA ZA KUFANYA MAPENZI KIPINDI CHA UJAUZITO.

kuna watu wamekua wakiuliza mara kwa mara kama inaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka umri gani wa mimba au ni sahihi kufanya tendo la ndoa kipindi cha ujauzito? maswali yalikua mengi sana hivyo leo nimeamua nijibu maswali hayo na makala hii.

mwanamke akiwa na mimba anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa hata kama anatarajia kuzaa kesho yake, hakuna tatizo lolote linalomzuia kufanya hivyo, baadhi ya wanawake wamekua wazito sana kufanya hivyo kwa kua na sababu mbalimbali za kujitetea bila kujua kwamba wanazikosa faida hizi ambazo ni muhumu kiafya.faida zenyewe ni kama zifuatazo

husaidia uchungu mzuri na kupona mapema; kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa huambatana na kubana kwa misuli ya nyonga hii husaidia kuweka imara misuli ya nyonga ambayo ni muhimu sana wakati wa kusukuma mtoto na baada ya kuzaa kwani misuli hii ikiwa legevu mwanamke huweza kushindwa kuzaa kwa njia ya kawaida na hata baada ya kuzaa huweza kushindwa kuzuia mkojo usitoke wenyewe au kuvuja damu kwa muda mrefu.

hupunguza kwenda ovyo kukojoa au kujikojolea; wakati wa ujauzito mtoto anapozidi kua mkubwa anazidi kukandamiza kibovu cha mkojo, hii humfanya mama aende chooni kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine hata akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe. tendo la ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuia hali hii.

huzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba; tafiti zinaonyesha kwamba aina ya protini inayopatikana kwenye mbegu za mwanaume huongeza kinga ya mwili na kuzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba ambacho kinaua wanawake wengi sana.

hutibu tatizo la kufika kileleni kwa shida; kipindi cha ujauzito chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia mara dufu huku kiwango cha homoni za oestrogen kikiwa juu sana, hii humfanya kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni.

huwapa uwezo wa kujiamini; kipindi cha ujauzito mwanamke hua anapata hofu sana na kutojiamini na mwili wake, hua na wasiwasi kwamba mwili wake unaharibika hivyo kitendo cha mwanaume wake kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko kwenye hali nzuri na anapendwa.

hupunguza msongo wa mawazo; kipindi cha ujauzito wanawake wengi huwaza sana kuhusu kesho yao...je swala la uchumi litakuaje? mwili wangu utakuaje? je ntapata jinsia nayotegemea? na kadhalika.. tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo kwa jina la oxytocin, homoni hii hupunguza mawazo na kumpa amani mjamzito.

huongeza upendo na mshikamano  kati ya wapenzi; katika hali ya kawaida wanandoa wakikwazana wanaweza wakapatana kwa kushiriki tendo la ndoa tu, amani na upendo kipindi hiki ni muhimu sana kwani kuna mtoto anakuja ambaye anatakiwa kuzaliwa huku baba na mama wakiwa wanapatana.

hukuandaa na uchungu; ukishiriki ndoa wakati wa tarehe zilizokadiriwa zimefika unapata homoni moja kutoka kwenye mbegu za  mwanaume kwa jina la prostglandin, homoni hii huivisha mlango wa uzazi na kuanza kufunguka taratibu kujiandaa na uchungu.

hutibu tatizo la kukosa usingizi; wanawake wengi wajawazito hua na dalili mbalimbali za maumivu na kuumwa sehemu tofauti za mwili na msongo wa mawazo, hii huweza kuwakosesha usingizi kabisa..tendo la ndoa huweza kuwapa usingizi mzuri.

hupunguza presha ya damu; kipindi cha tendo la ndoa presha ya damu hushuka kwenye kiwango kizuri sana, hii ni muhimu sana kwa wanawake wenye hatari ya kupata kifafa cha mimba kama wanene sana, wenye kisukari au wenye historia za ugonjwa wa presha kwenye koo zao.

mwisho; hakikisha unatumia staili za tendo la ndoa ambazo hazimuumizi mtoto na mama yaani hakikisha haulilalii tumbo hasa mimba ikiwa kubwa, kuna staili muhimu kipindi hiki kama kuangalia upande mmoja, mwanamke kuja juu, au mwanamke kuinama

MAMBO YANAYOSHUSHA THAMANI YA MWANAUME MBELE YA MWANAMKE.

Katika uhusiano baina ya mume na mke hutokea mambo mbalimbali yanayoimarisha uhusiano baina yao au kuuharibu. Baadhi ya nyakati mwanaume hufanya baadhi ya mambo yanayomshusha thamani mbele ya mwanamke. Hivyo, wanaume wote wenye khofu ya heshima na thamani yao kuanguka, ninawaletea mambo muhimu ambayo yanashusha thamani ya mwanaume mbele ye mwanamke:

1. HADAA NA UNYONYAJI:
Baadhi ya wanaume ni wazuri sana katika kumnyonya mwanamke kwa kutumia kisingizio cha mapenzi. Wanazitumia mali zake na kuzinyonya kwa kutumia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na maneno matamu ya mapenzi au kutengeneza simulizi za uongo kuhusu matatizo ya kipesa na kiuchumi. Mwanamke akigundua kuwa analaghaiwa, basi atamshusha thamani haraka mwanaume huyo na kuamua kujitenga naye. Na iwapo ataendelea kuwa naye, basi hasara na majuto yatakuwa juu ya mwanamke huyo.

2. WANAWAKE WENGI:
Mwanamke anapenda ahisi kuwa yeye ndiye mtu pekee katika maisha ya mwanaume. Kuwa na uhusiano na wanawake wengi wasiokuwa na ukomo, husababisha katika kushusha heshima yake mbele ya mkewe. Tambua kuwa hiyo sio sifa nzuri ya kujivunia.

3. UONGO:
Urongo ni miongoni mwa mambo ambayo mwanamke huchukia sana kuyaona kwa mwanaume. Kuna wanaume hodari katika kutunga na kusema uongo. Lakini mwanamke akigundua kuwa unamuongopea, basi heshima na thamani yako itakuwa imeshuka kabisa machoni mwake hata kama ataamua kuendelea kuishi nawe.

4. UKOSEFU WA HESHIMA:
Utovu wa heshima ni miongoni mwa mambo yanayoharibu uhusiano maridhawa baina ya wanandoa hata kama kutakuwa na mambo yanayowaunganisha. Hivyo, ewe mwanaume mwenzangu, usiishushe haiba ya mkeo kwa lugha chafu au kumdhalilisha. Usishushe thamani ya vitu anavyovifanya kwa ajili yake hata kama vitakuwa vidogo. Daima jitahidi kuwaheshimu ndugu zake kwa sababu ukifanya kinyume na hivyo, thamani yako mbele yake itashuka, hata kama hatakwambia.

5. KUTOMUAMINI:
Kuaminiana ni miongoni mwa mambo mazuri ambayo yakipatikana katika mapenzi ya wawili, huwasaidia kukabiliana na vikwazo na changamoto mbalimbali. Ikiwa mume ni mtu anayetilia shaka maneno na matendo ya mke kila siku, thamani yake machoni mwa mkewe itashuka. Kuaminiana kuna mafungamano makubwa sana na upendo na kujiamini. Iwapo kutakuwa na ulegevu katika jambo hilo, mahabba yao hayatakuwa maridhawa.

AINA 12 ZA WANAWAKE AMBAO WATAFANYA MAISHA YAKO KUWA MAGUMU.


Kila mtu hapa ulimwenguni ameumbwa na sifa tofauti tofauti. Kuna wengine wameumbwa na tabia za kuridhisha na wengine wameumbwa na tabia ambazo hazifurahishi. Hii pia inajitokeza katika wanawake. Katika mahusiano, utapata kuwa wanawake wanakuwa na tabia ambazo aidha zinawapendeza wanaume wao ama zinawachukiza.
Ok. Katika kuangalia tabia za wanawake, tumekuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mwanamke anayekuganda nguoni
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kisai cha kuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kukuhusisha wewe. Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye amekuwa amezama na penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua. Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu nayeye. Well, hii ni poa kwa mahusiano lakini itafikia mahali fulani ambapo utachoshwa na tabia zake haraka. Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila wakati anapokumbwa na jambo fulani hawezi kulitatua bila kukuhusisha.

2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele. Lakini kulingana na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.
Mwanamke kama huyu ungempenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni kuwa kadri siku zinavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani, mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako. Hii inamaana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na marafiki zako, vilabuni, wanjani...nk, yaani kiufupi kila uendapo anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli huyu?

3. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

4. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

5. Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

6. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

7. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

8.Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

9. Nusa Nusa
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

10. Asi na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.

11. Mcheza ndondi
Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

12. Mtoto wa mama
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

Hii ni baadhi ya tabia za wanawake ambazo mwanamume yeyote anafaa kuwa chonjo kwani mwishoni wanaweza kuleta taabu ambazo zitakuwa vigumu kutatua.

HILI NDIO TATIZO SUGU KWA WANA WENGI WA SASA..

Tabia ya wasichana kuwaombaomba wanaume hela bila sababu imeondoa imani na heshima kwa wasichana.

Utakuta wasichana hao wana kazi, wana biashara ila kutwaa kuombaomba.

Hii tabia imefanya wanaume waone kuwa wasichana wote wanatabia hiyo hiyo.

Pia imesababisha hata kushindwa kuwapa hela wale wasioomba eti kwakuwa wanakuwa wanawapima tabia hiyo.

Enyi wasichana 'ombaomba' acheni tabia hiyo, mnashusha heshima za wasichana wote

HUU NDIO UMUHIMU WA KUFAHAMU JUU YA KUWA NA MWENZA WA MAISHA YAKO,

Hivi umewahi kujiuliza kwanini tunakuwa na wenzi wa maisha? Kwanini mapenzi yakawepo? Kwanini wewe una mpenzi na ikitokea mkawa mmehitilafiana unakosa raha? Sina shaka kuwa katika hili, kila mmoja anaweza kuwa na fikra zake mwenyewe, lakini leo nitafafanua sababu za msingi zaidi zinazowafanya wapenzi kuwa pamoja na hatimaye kuishi katika ndoa.

Lakini kabla ya kufika mbali zaidi hebu jiulize swali moja, mapenzi humaanisha nini hasa? Kimsingi mapenzi ni hisia za watu wawili ambazo hukutana pamoja zikimaanisha upendo wa dhati. Pendo hukamilika ikiwa wawili hao kwa wakati mmoja wakahisi hisia hizo, ingawa wakati mwingine mmoja ndiyo huwa wa kwanza kuanza kuhisi hisia hizo.

Wakati mwingine inawezekana mkajikuta mmependana tangu siku ya kwanza tu mlipokutana, lakini wengine huchukua muda mrefu kidogo kabla hisia hizo hazijachukua nafasi.

Wengine hutumia nafasi hii vibaya, baadhi yao huamini kuwa ngono ndiyo mapenzi yenyewe, jambo ambalo halina ukweli. Hebu fuatilia vipengele vifuatavyo kwa makini bila shaka kuna kitu utajifunza!

KUSAIDIANA MAWAZO
Hili ni jambo la msingi zaidi katika uhusiano, mwanaume kama mwanaume, kwa uwezo wake peke yake, hata kama ana uwezo mkubwa kifedha, siyo rahisi kutimiza mipango yake ya kimaendeleo kwa uwezo wa akili yake peke yake.

Huu ni ukweli ambao wanaume wengi huukwepa kwa kuhofia kale kamsemo ka ‘tulichuma pamoja’, kimsingi unapokuwa katika muunganiko hasa kama mwenzi wako ana hekima chanya, ni wazi kuwa kutakuwa na kitu kinachoongezeka katika maisha yako. Fikra za kuwa mwanamke ni mtu wa kuzaa na kuangalia familia pekee, ni fikra za kizamani zisizo na mantiki.

VIPI KUHUSU KUKUTANA KIMWILI?
Mapenzi ni kitu kingine na ngono ni kitu kingine, ingawa baadhi ya watu hufikiria kuwa ngono ni sehemu ya uhusiano, jambo ambalo sio la kweli hata kidogo. Kimsingi ngono huja baada ya tamaa kuingia kati ya hao wawili wanaopendana!

MAPENZI: FUATA NJIA HIZI MWANAMKE HAKUKATAI NG'OO HATA AWE VIPI..

Kifupi unakuta mwanaume ana status nzuri tu lakini anakosa mwanamke anayejielewa.yaani wengine hadi wananiuliza sometimes mimi "hivi wewe unawapataje wanawake wazuri na wanaojimbua hivo".

Sasa leo nimeona ni vyema nikishare na nyinyi namna ya kumnasa demu hata awe ni anajitambua vipi!

1: Unapoomba namba ya simu hakikisha huombi kwa papara, yaani usioneshe kama una shida sana na usioneshe kama unataka kumtongoza, bali onesha kama unataka tu ulafiki wa kawaida,yaani lafiki wa kuchati nae tu kawaida.

2: Akikupa namba leo kausha usimtafute leo leo, mtafute baada hata ya wiki,msalimie tu na umpigie, hapa uangalie na muda ambao unadhani mtu anakuwa free, sio kupiga simu asubuhi sana au mchana au usiku sana, piga mida ya saa mbili usiku,na usiongee nae zaidi ya dakika 5.

3: Hakikisha kila siku unamtumia msg mara 3 na kumpigia simu mara moja, yaani asbh mtakie asbh njema, mchana, jioni na usiku piga kumpa pole na heka heka za mchana, ongea nae si zaidi ya dakika 5 ili usimchoshe.

4: Hakikisha hutumii maneno ya mtaani sana mfabo oya,inakuwaje,michongo vipi, barida, mzuka, poa n.k. Tumia maneno mazuri ya busara mfano sawa, haya, umeshindaje, habari yako, n.k. yaani asikuone wewe hujitambui.

5: Weka nae urafiki wa kudumu kiasi kwamba awe anakumiss, na ukimtext asipojibu mtumie vocha hata ya buku. Ila angalia usitumie pesa sana.

6: Omba outing nae, na akikubali basi mpeleke sehemu tulivu yenye adabu na sio mnaenda bar, mkiwa huko ongelea zaidi maisha ya kawaida ya mwanadamu, usiongelee ishu za X wako kamwe, ishu za mapenzi usiongelee kabisa, weka vistory vya kuchekesha ili awe anafurahi na kukumiss mkitoka hapo.

7: Ukiwa unapiga nae stori kwenye simu usiwe unaongea sana, na hata mkiwa pamoja basi usiongee sana kama chiriku, pangilia maneno sana ya kuongea(waza kabla ya kusema).

Baada ya urafiki wa kama miezi miwili hivi, hapo sasa mtamkie wazi wazi kwamba unampenda tangu muda mrefu, na umtongoze kwa heshima sana. Nakuhakikishia hapo hachomoki hata kwa dawa.

NB: Mbinu hizi ni za kuwapata tu wanawake wanaojielewa, wanaotaka mwanaume/mpenzi na sio wanaotaka pesa. Kwa wale wanawake vicheche, we tumia pesa tu, ukimtongoza leo jioni basi kesho unamfunua

HABARI YA KUSIKTISHA USIKU HUU: MWALIMU AFUMANIWA AKIMBAKA MWANAFUNZI WAKE SHUHUDIA TUKIO HILI HAPA...


Taarifa zaidi zilidai kuwa wanafunzi walioshiriki fumanizi hilo dhidi ya mwalimu na mwanfunzi mwenzao walimuadhibu mtuhumiwa (mwalimu) wao na kufanikisha kukamatwa kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, aliiambia Nipashe jana kuwa atalitolea ufafanuzi suala hilo baada ya kupokea taarifa rasmi.
Hata hivyo, inaelezwa na mashuhuda kuwa mwalimu huyo alitiwa mbaroni usiku wa kuamkia jana na wananchi pamoja na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Songa wilayani humo, Juma Bendera, ambaye alipata taarifa kwamba mwalimu amemfungia mwanafunzi chumbani mwake.
Akizungumza na Nipashe jana, Afisa Mtendaji huyo alisema juzi saa tano usiku, alipata taarifa kuwa katika shule hiyo ya Songa kuna mwalimu aliyemfungia mwanafunzi wake wa kike chumbani.
Alisema baada ya kupata taarifa hiyo, alifika shuleni ambapo alimkuta mkuu wa shule hiyo, Habibu Shedafa na mwenyekiti wa Wazazi wa shule hiyo, Rashidi Madiwa, na kundi la wanafunzi wavulana wakiwa eneo la nyumba ya mwalimu huyo huku mtuhumiwa akiwa ndani na mwanafunzi huyo wa kike.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wazazi wa shule hiyo, Rashidi Madiwa, alisema baada ya kupata taarifa hizo, alikwenda katika nyumba anayoishi mwalimu huyo na kupitia dirishani aliwaona yeye (mwalimu) na mwanafunzi wakiwa watupu kama walivyozaliwa huku wakinyonyana ndimi zao.
“Milango ya nyumba ilifungwa, tulipochungulia dirishani tulimuona mwalimu na mwanafunzi wamevua nguo zote na wananyonyana ulimi… ni jambo linaloshitua na kuumiza hasa kwa kuzingatia mwalimu ni mtu muhimu katika jamii,” alisema Madiwa.
Alisema walipojaribu kumuita ili atoke nje, alikataa na ndipo kundi la wanafunzi wavulana wakaamua kuvunja mlango wa nyumba na kufanikiwa kuingia ndani.
Alisema wanafunzi walishindwa kumkamata mwalimu huyo baada ya kuwatishia kwa panga na hatimaye kupata nafasi ya kukimbia hadi katika nyumba ya mwalimu mwenzake.
Alisema hatua yake hiyo haikumsaidia kufuatia wanafunzi kumfuata huko na kuangushia kipigo kabla ya kumuweka chini ya ulinzi na kisha polisi kuja na kumchukua.
CHANZO KUNASWA
Ilielezwa kuwa kabla ya mwanafunzi huyo kwenda kwenye nyumba ya mwalimu, alikuwa akitumiana ujumbe mfupi wa simu ya mkononi na mwalimu wake huyo.
“Katika ujumbe huo, mwalimu alimwambia mwanafunzi atoroke nje ya bweni lao na aende nyumbani kwake wakafanye mapenzi, “ alieleza mtendaji Bendera.
Alisema baada ya mwanafunzi huyo kufanikiwa kutoroka alielekea moja kwa moja nyumbani kwa mwalimu huyo na kuingia ndani.
Alisema baadhi ya wanafunzi anaoishi bweni moja baada ya kuhakikisha mlango umefungwa, walianza kutoa taarifa sehemu mbalimbali ikiwamo kwa mwenyekiti wa kitongoji cha ambaye alikuja kuungana nao kumtoa.
Mwanafunzi aliyehusishwa na tukio hilo, amefanyiwa vipimo katika Zahanati ya Songa, na baadae alipelekwa polisi kwa ajili ya mahojiano.
Diwani wa kata ya Songa, Leslie Nchimbi, alilaani kitendo hicho na kusema ni imani yake kuwa hatua kali zitachukuliwa ili kukomesha uvunjifu huo wa maadili ya kazi ya ualimu na pia ya kijamii.
Naye Mkuu wa wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo, ametoa onyo kwa vijana na walimu wa shule hiyo, kuacha mara moja tabia ya kujihusisha mapenzi na atakayegundulika atakamatwa na kufunguliwa mashtaka. Mkuu wa shule hiyo, Habibu Shedafa, amethibitisha kutokea tukio na kueleza kuwa juhudi zinafanyika kuhakikisha matukio ya aina hiyo yanakomeshwa.

VIDEO: Kitanda cha Wolper Chapambwa Madola Kumkaribisha Birthday Boy, Harmonize

Jumanne hii ni birthday ya mkali wa wimbo ‘Matatizo’, Harmonize ambapo mastaa mbalimbali pamoja na mashabiki wake katika mitandao ya kijamii wamem-wish kwa kumtakia heri na mafanikio katika maisha yake.

Kwa upande wa malkia wa filamu, Jacqueline Wolper ambaye ni mpenzi wa staa huyo, ameonyesha maandalizi ya kitanda chache kilichopambwa na madola pamoja na keki kwa ajili ya mpenzi wake huyo ambaye leo hii ametimiza miaka kadhaa. 

Siri ya Mama Diamond Kutoka na Muarabu Yafichuka....

Imefichuka kuwa mama Diamond alitoka na Muarabu na kuzaa mtoto wa kike ambaye sasa ni mkubwa.
Mtoto huyo amesema kuwa huwa hapendi kufahamika ndio maana anajitahidi kuweka 'low profile'.

Mtazame Hapa mtoto huyo ambae ni Nusu Mwarabu nusu Mwafrika:


chanzo: Udakuspecially

Kama Wewe Mwanaume Una Tatizo la Kufika Kileleni Haraka Kabla Mpenzi Wako Hajaridhika Hii Inakuhusu

Pre mature ejaculation ni nini?
Hii ni hali ambayo mwanaume anatoa mbegu mapema sana kipindi cha tendo la ndoa na mara nyingi huambatana na kushindwa kumridhisha mpenzi wake.

Tatizo hili limekua likiwapata wanaume wengi na kujisikia aibu mbele za wenzi wao pale wanaposhindwa kuendelea kabisa baada  ya hali hii kutokea.

Kimsingi  mwanaume anatakiwa achukue dakika nne mpaka nane kabla ya kutoa mbegu za kwanza lakini watafiti wanasema tatizo hili hugundukiwa mtu anapotoa mbegu ndani ya dakika moja au kabla ya dakika moja.

Tatizo hili huweza kutokea mara tu baada ya kubalehe,{primary pre mature ejaculation} mda mrefu baada ya kubalehe{secondary PE} au kutokana na aina ya mwanamke uliompata.{situational PE}

Chanzo ni nini?
Tatizo hili halina sababu za kitaalamu zilizofanyiwa utafiti zikakakubalika ila wanasayansi wanaamini sababu zifuatazo zinaweza kua chanzo kikuu cha tatizo hilo.

Kupiga punyeto au kujichua; 
mara nyingi watu wanaopiga punyeto hua wanafanya haraka kwa kujificha ili wasikutwe na mtu. tabiaile ya kulazimisha mbegu zitoke haraka huweza kuleta tatizo hili.

Kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa;
kukaa mda mrefu sana bila kushiriki tendo la ndoa husababisha mkusanyiko mkubwa wa mbegu za kiume ambazo zinaleta msisimko mkubwa na ukichelewa sana kushiriki tendo la ndoa zitatoka kwenye ndoto nyevu. kawaida mwanaume anatakiwa ashiriki tendo angalau mara nne kwa wiki.

Kuwa na wasiwasi wakati wa tendo la ndoa; 
mtu akiwa na historia ya kupata  hali hii kabla, hua hajiamini na kua na wasiwasi kwamba litatokea tena na matokeo yake hulipata kweli.

Madhara ya dawa zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu; 
baadhi ya dawa za usingizi, mawazo na zingine zinazofanya kazi kwenye mishipa ya fahamu huleta tatizo hili mfano amitriptyline.

Kurithi;
baadhi ya koo au familia fulani hurithi vimelea vya kua na ugonjwa huu kwa vizazi mbalimbali vya familia husika.

Magonjwa ya mfumo wa uzazi wa mwanaume mfano prostatitis.

Diagnosis{ kuutambua ugonjwa]
Mwanaume yeyote ambaye anatoa mbegu chini ya dakika moja au mbili ni muhanga wa hili tatizo na anatakiwa apewe matibabu.


Matibabu
Matibabu ya ugonjwa huu yamegawanyika sehemu kuu mbili kulingana na ukali wa tatizo husika.


Non pharmacological treatment{matibabu yasiyo hitaji dawa}:  matibabu haya hupewa watu ambao wanahimili mpaka dakika tatu bila kutoa mbegu.
Pharmacological treatment{matibabu yanayohusu dawa}: matibabu haya hupewa watu ambao hutoa mbegu ndani ya dakika moja baada ya kuanza kushiriki tendo la ndoa, watu hawa hushauriwa kutumia na mbinu zote mbili za matibabu.


Yafuatayo ni matibabu yasiyohitaji dawa.

Tumia condom:
Condom ni moja ya tiba nzuri ya tatizo hili kwani hufanya kazi kwa kupunguza hisia kali za mapenzi mtu anazozipata pale ambapo hatumii condom.

Kandamiza perineum kwa kidole:
Perineum ni eneo kati ya mkundu na korodani, ile sehemu ikikandamizwa na kidole huweza kuzuia kukojoa haraka wakati wa tendo la ndoa.

Punguza wasiwasi: 
hebu lifikirie tendo hili kama njia ya kujifurahisha sio njia pekee ya kutafuta kutoa mbegu,  hii itakusaidia kuondoa mawazo ya kutafuta mbegu na kuchelewa kumaliza.

Fanya taratibu: 
picha za ngono zinadanganya sana watu kwamba kulala na mwanamke lazima ufanye kwa haraka haraka kama mbwa. HAPANA; ukifanya taratibu ndio njia nzuri ya kumfikisha mwenzako na wewe kuchelewa kufika kileleni.

Badilisha style: 
ile style ya zamani ya kumlalia mwanamke kwa juu{missionary position} inaleta msuguano mkubwa kwenye kichwa cha uuume hivyo itakufanya ufike haraka sana.

Tumia style ya wewe mwanaume kutangulia chini afu mwanamke juu au kulala kwa upande wote mnaangalia upande mmoja hii itakusaidia sana kuchelewa

Toa mawazo kwamba unafanya ngono:
hebu jaribu kufikiria mambo mengine ya kikazi au masomo wakati unafanya tendo hilo, hii itakupunguzia hisia kali za mapenzi na kuchelewa kufika.

Fanya na kuacha:
hii ni ile hali ya kuzuia msuguano pale unapoona unakaribia kutoa mbegu kwa kama sekundi 30 kisha unaanza upya. Hakikisha haufiki “point of no return”. pointi ambayo huwezi kujizuia tena kumaliza.

Kandamiza sehemu ya shingo la uume:
hii sehemu ya shingo ya uume kwa chini ambayo ukiibana itakusaidia kuanza upya tena kihisia. Nimetumia shingo la uume kwasababu najua uume hauna mabega.

Tumia kilevi:
unywaji wa pombe mfano bia mbili kwa siku kwa wanaume pombe hupunguza kidogo nguvu ya mishipa ya fahamu na kufanya mtu aliyekunywa kuchelewa sana kufika kileleni, [watu wanaokunywa pombe lazima mtakubaliana na hili] hivyo unaweza kunywa bia, wine au whisky nusu saa kabla ya tendo na kuondoa shida hii.

·     
Matibabu ya kutumia dawa.
hizi hupewa iwapo tatizo lako ni kubwa sana na hizo njia hapo juu zimeshindikana...

1. Serotonin reuptake inhibitors mfano paroxetine na  clomipramine zimefanya kazi nzuri ya kuzuia kufika kileleni haraka..... humezwa saa moja kabla ya tendo la ndoa.

2. anesthetic creams:  hii hupakwa kwenye kichwa cha uume saa moja kabla ya tendo la ndoa kuzuia msisimuko na kufanya mwanaume achelewe kufika kileleni wakati wa tendo.

Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top