Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Witness: Nimejichora tattoo kiunoni ili nisisaliti ndoa yangu

Msanii hip hop hapa nchini, Witness aka Kibonge Mwepesi, ameitaja sababu ya kujichora tattoo ya jina la mpenzi wake Ochu Sheggy kwenye kiuno chake.

Akiongea katika kipindi cha E-News cha East Africa TV, Witness amesema ameamua kufanya hivyo ili kuepuka kumsaliti mpenzi wake.

“Ukiweka tattoo sehemu kama niliyoweka mimi(kiunoni) inazuia, hata unapotaka kumsaliti mwenza wako yule unayekuwa naye inamnyima hamu kabisa na anashindwa hata kukutamani tena,” alisema Witness.

Pia Witness alisema kuwa watu wanadhani kuwa kuolewa ndiyo kumaliza kila kitu lakini kwa sehemu ambayo mapenzi yao yamefikia hakuna kitu ambacho anakihitaji tena kwakuwa mapenzi ni kuungana mkono na Ochu anamsaidia katika kila kitu anachofanya.

PICHAZ 22 : Majengo ya Kushangaza Duniani.

June 12 2016 nakusogezea picha 22 za majengo yenye muonekano tofauti na majengo mengine uliyowahi kuyaona, Majengo haya  yanapatikana nchi mbalimbali ikiwemoFrance, Marekani, Korea n.k imejengwa kwa staili ya kipekee kabisa pia usisahau kunidondoshea comment yako chini mtu wangu.
1.Jengo hili limejengwa nchini Poland mwaka 2014 na lenye kuonekana kama jengo linalodondoka.
crooked house
crdhs
2. Jengo hili la nyumba lenye muonekano wa chini juu juu chini limejengwa  kwa siku 114 nchini Poland kwenye kijiji kidogo cha Szymbark mwaka 2013.
upside-down-house-poland
UpsideDownHouse
3. Jengo hili la mfano wa kinanda limejengwa mjini Huainan, nchini China mwaka  2007.
ThePianoHouseHuainanAnhuiChina
piano
4. Jengo hili limejengwa chini ya ardhi ndani ya korongo  nchini  Switzerland.
hill house
5. Nyumba hii iliojengwa juu ya jiwe katikati ya mto na kund la marafiki na baada ya kupata hida ya mafuriko kila mara ikachukuliwa na Rock Restaurant na kuijenga tena nchini Serbia.
river house
Muonekano wa nyumba hiyo mara ya kwanza kabla ya kupatwa na dhoruba.
rvr hs
Mtazamo wa nyumba hii mara ya pili baada ya kujengwa tena.
6. Nyumba ya jiwe iliyojengwa nchini Portugal mwaka 1973.
stone house
7. Nyumba hii iliyojengwa kwa mfano wa sheli ya samaki nchini 1960 nchini Mexico.
seashell house
Nautilus-House6-600x400
8. Jengo hili limejengwa nchini Singapore.
singapore
9. Jengo hili limejengwa na linatumika kama makazi ya watu nchini Netherlands.
cubes
10. Jengo la Kingdom Tower jengo lililopo katika mji wa Jeddah, Saudi Arabia, ni miongoni mwa majengo marefu duniani, lilijengwa kwa gharama ya dola bilioni.
saud
11. Jengo la Cathedral of our Lady of Aparecida ni jengo la kanisa ambalo lipo Brazil, lilijengwa mwaka 1946 hadi 1980, hupokea watalii milioni 10 kila mwaka, huchukua watu zaidi ya 70,000 lina ukubwa wa mita 12,000.
brazil
12.Jengo la nyumba hii yenye shepu ya ndege aina ya Airbus A380, imejengwa uko nchini Miziara, Lebanon.
airplane_house1-600x399

13. Jengo hili iliojengwa kwa mfano wa gari nchini Austria.
gar
garii
14. Jengo hili limejengwa kwa tani 110 za chuma nchini Texas kwanzia mwaka 1973 mpaka 1996.
The-Steel-House2-600x400
The-Steel-House1-600x450
15. Jengo la Crystal Cathedral limejegwa Kjiji cha Garden Grove, California.
cry
ULIKOSA KUIONA VIDEO YA TUZO ZA NDOA ZILIZODUMU MUDA MREFU KUTOLEWA TANZANIA? ICHEKI VIDEO HII HAPA CHINI.



Electronic Train Launch: Ethiopia wameanza rasmi kutumia Treni za abiria zinazotumia umeme Picha Zote Ziko Hpa

Nimepita kwenye page ya Facebook ya BBC Swahili nikakutana na hii stori ambayo nimeguswa kuishare hata hapa Tanzaniastar.com kuhusu nchi ya Ethiopia kuzindua Treni za umeme.

 Ripoti inasema Treni hizi ambazo zimezinduliwa September 20 2015 zinaanza kubeba abiria na zinatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa watu kwenye mji mkuu wa Addis AbabaEthiopia nchi ambayo mpaka mwaka huu wanasema idadi ya watu wake ni zaidi ya MILIONI 90


 BBC wanasema hizi Treni zimetajwa kuwa mfano na za kwanza kusini mwa jangwa la sahara ambapo ujenzi na uendeshaji wa huduma hii ya reli unatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya China.

 

 Treni hizi za umeme zitakua na uwezo wa kuhudumia Abiria elfu kumi na tano ndani ya dakika 60 ambapo Treni moja inaweza kubeba abiria 286 kwa wakati mmoja.






 Credit: Millardayo

USIDANGANYIKE! Hizi Hapa Dalili 7 za Mwanamke Anayekupenda Kwa Dhati!

MSHAURI WAKO NAMBA MOJA
Mwanamke sahihi kwako ni yule ambaye anakushauri hasa unapokuwa katika matatizo makubwa zaidi ya kimaisha.
Sifa hii itaonekana tangu mapema kabisa, unapokutana naye ukiwa huna furaha, ni rahisi kukuliza kulikoni, anakuuliza si kwa sababu anataka kuona furaha yako pekee bali pia anataka kujua kama kuna tatizo ili aweze kutoa mchango wake wa mawazo katika tatizo lako.


Siku zote, mwanamke mwenye busara na anayekupenda, ni wazi kwamba atapenda kujua tatizo lako na kulichukulia kama lake, ili aweze kukushauri namna ya kutatua kwa namna moja ama nyingine.

KUJITOA KWA KILA HALI
Mwanamke anayekupenda kwa dhati, atajitoa kwako kwa kila hali. Unajua, kuna mambo ambayo si rahisi kufanyiwa na kila mtu, yapo ambayo yanafanywa kwa watu wanaopendana tu.


Huyu atajitoa kwako, atafanya mambo muhimu ambayo si rahisi kuyafanya kwa mtu mwingine. Atakupa vipaumbele kwenye mambo yake yote kwa kukueleza mipango yake (hata ile ya siri) na kukufanya wa kwanza kujua kinachoendelea katika maisha yake.


Lazima ujiulize na uangalie, je, wewe ni moja ya vipaumbele vyake? Je, wewe unakuwa wa kwanza kujua mambo yake kabla ya rafiki zake? Je, uzito anaochukulia kwako ukiwa na tatizo, ndiyo anaouchukua pia kwa rafiki zake ama ndugu zake? Lazima kuwe na tofauti. Siku zote, umuhimu wako hauwezi kuwa sawa na mfanyakazi mwenzake ofisini.


WIVU
Ingawa si lazima awe na wivu lakini inaelezwa kwamba wivu ni moja ya alama ambazo unatakiwa kuziangalia wakati ukimchunguza kama anakupenda kwa dhati. Wivu ni ladha ya mapenzi. Ni kama ndimu kwenye mchuzi au kitunguu swaumu kwenye pilau.

Wivu ni afya ya uhusiano, kwamba lazima aoneshe wasiwasi na wewe, atilie mashaka simu yako, achunguze email yako, blog na hata ukurasa wako wa Facebook. Hana nia mbaya, lakini anachotaka kujua, ni kama kweli yupo peke yake au la.

PESA SI KILA KITU
Kama anakupenda, hawezi kuithamini sana pesa. Hiyo itakuwa kama sehemu ya uhusiano wenu lakini si kitu anachokipa kipaumbele kwa asilimia kubwa.

Kama anaomba sana pesa, anazungumzia sana pesa, matatizo yake makubwa ni ya fedha, basi ujue kwamba penzi lake lina hati hati.

Mwenye mapenzi ya kweli, pesa ni matokeo tu, lakini si kukufanya wewe kitegauchumi au sehemu ya kutatua matatizo yake.

WASIWASI NA USALAMA WAKO
Baadhi ya wanawake wanaweza kusema mengi lakini wasiwasi kwa ajili ya usalama wa mtu unayempenda ni muhimu sana. Hii ni moja ya njia ya kujua kama mwanamke anakupenda. Anapenda kujua uko wapi, unafanya nini na utarudi nyumbani muda gani.


Si rahisi kufanya hivyo kwa mwanaume ambaye hana mapenzi naye. Anafanya kwako, kwasababu anakupenda na anajali usalama wa maisha yako, na si maisha yako pekee, bali kuna jambo kubwa na zito zaidi. Anajali usalama wa penzi lake maana hataki kukupoteza na kulipoteza penzi hilo.


ANAKUSIKILIZA
Kusikilizwa na mwanamke si tabia mpya au ya kujifunza, ni agizo la moja kwa moja kutoka kwa Mungu mwenyewe. Kwa meneno mengine, kama mwanamke wako atakuwa hakusikilizi, mpinzani, mkaidi, mkali, mkorofi, maana yake anapingana na maagizo ya Mungu moja kwa moja.


Kupingana na agizo hilo, ambalo ni stahili yake, ni wazi kwamba hata mambo mengine ya kibinadamu ambayo atatakiwa kujifunza yeye mwenyewe kwa nia ya kuonesha heshima kwako wewe mumewe mtarajiwa, atashindwa.


Sipo hapa kuhubiri dini, lakini kuna mahali maandiko yameagiza, mwanaume ampende sana mke wake na mwanamke amheshimu/amtii mumewe.


Hapo kila kitu kipo wazi, kwahiyo katika hali ya kawaida, kama mwanamke wako atashindwa kukutii, kukuheshimu na kukusikiliza kama kiongozi wake, basi ni dhahiri kwamba, atakuwa tatizo katika maisha yenu ya baadaye, hasa mkiwa tayari mmeshaingia kwenye kifungo cha ndoa.


ANAWAPENDA NDUGU ZAKO
Ndugu zako ni cheni katika maisha yako. Ndiyo watu wako wa karibu. Ndiyo wanaokusaidia/watakaokusaidia pindi utakapokuwa na matatizo.

Unapotaka kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamke, hasa kuingia katika hatua kubwa zaidi ya ndoa, unapaswa kufikiria mara mbili juu ya hawa wanaoitwa ndugu. 

Ni tatizo kubwa sana, kama mwanamke unayetarajia awe mkeo, akawa hawapendi, anawadharau au anawachukia ndugu zako kwa sababu zake mwenyewe.

Mfano; kama mwanamke wako hamheshimu mama yako mzazi, baba yako, kaka na dada zako ni tatizo. Inakuwa tatizo kwa sababu hawa ni watu ambao unatakiwa kushirikiana nao katika mambo mengi ya kijamii, hasa unapokuwa katika matatizo. Kwakuwa unawapenda ndugu zako, pia utakuwa na mapenzi na mwanamke wako, lazima kutakuwa na mgawanyiko maana pande hizi mbili ni muhimu kwako.
Hapa namaanisha kwamba, inawezekana kabisa ukajikuta unaegemea aidha kwa ndugu zako zaidi au kwa mwanamke wako na hapo ndipo mkanganyiko mkubwa wa kiuhusiano unapoweza kutokea.
Mwanamke wako akiwa na upendo na ndugu zako ni wazi kwamba yote hayo niliyoeleza hapo juu hayatajitokeza na hivyo kuishi kwa amani.

Hivi Ndivyo MARAFIKI Wanavyoharibu MAHUSIANO ya WAPENDANAO!

Watu wengi wamekuwa wepesi sana kukimbilia kwa rafiki zao ili kuomba msaada wa mawazo ya nini wafanye kwenye mapenzi. Imani iliyojengeka kwa watu wengi katika jamii yetu ni kuwa ushauri ni kitu muhimu sana kwa kila hatua.
Kwa mtazamo wa haraka haraka unaweza kuishia kwenye ukomo huo wa fikra na kuamini juu ya ushauri wa mtu kukufikisha mahali sahihi kwenye mapenzi. Unapokerwa na mpenzi unakimbilia kushauriwa na wakati mwingine hata unapotaka kuoa au kuachana na umpendaye, unamuomba rafiki yako ushauri.
Je, umeshawhi kufikiria hasara za kuomba ushauri wa kimapenzi kwa rafiki yako? Hebu ungana nami wiki hii ili nikumegee kidogo hasara za ushauri.

UTAKUPOTOSHA
Ni wazi kwamba kipimo cha uelewa kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Ifahamike kuwa, uhodari wa mambo nao hutofautiana, mtu anaweza kuwa mahiri katika siasa na akaaminika kwenye jamii, lakini ukimpelekea suala la mapenzi anakuwa hajui kitu, hivyo ni rahisi kukupotosha.

Uchunguzi unaonyesha kuwa, wapenzi wengi sana hupotoshwa na rafiki zao wasiokuwa na uelewa wa kutosha juu ya tatizo au suala husika la kimapenzi. Ni vema kuwa makini unaposhauriwa.

UTARAHISISHA MAMBO
Mara nyingi washauri huwa si wao wanaokabiliana na mambo, hivyo ni rahisi kwao kupima vitu kwa juu juu tu na kushauri kirahisi rahisi. “Vipi kakupiga namna hii, aaa huyu si mwanaume kwa kweli ni bora ukaachana naye.” Anasema ni bora kuachana naye kwa sababu haumizwi na kuachana, unayeachana ni wewe anayekushauri.

“Mkubali tu bwana unalaza damu, hiyo tabia yake ya uhuni atabadilika, shosti unataka kuacha bahati ipite?” Kwa mshauri ni rahisi kusema hivyo lakini kumbuka ukubwa wa tatizo hatimaye utakabiliana nao wewe. Hii ina maana kwamba, unapofikiria kuhusu ushauri ufikirie pia kuhusu kushauriwa jambo kirahisi, ukiuvaa mkenge mwenye kuumia utakuwa ni wewe.

UTAKUGEUZA
Ulimwenguni kuna aina zaidi ya 1000 za mapenzi na kila mmoja anatajwa kupenda kwa staili zake. Mapenzi ni kama chembe hai nyekundu zilizopo kwenye damu ya mwanadamu ambazo zinaelezwa na wataalamu kuwa hazifanani hata kidogo. Uzoefu unaonyesha kuwa, washauri wengi hushauri kwa uzoefu wao, lakini je ni sahihi uzoefu huo uwe msaada kwa mtu mwingine?

Jibu ni hapana, kinachotokea mara nyingi kwenye ushauri ni mtu kumfanya mwenzake awe kama yeye alivyo, yaani apuuze aamue na apende kama staili yake, jambo ambalo haliwezekani kabisa kwenye mapenzi. Vipi Juma ageuke ghafla awe kama Hassan kwenye suala la mapenzi? Ushauri ni muhimu lakini upime kama unalingana na matakwa yako.

UTAKUONDOLEA UJASIRI
“Kwa maelezo hayo mumeo ni malaya sana, naona itakuwa vigumu kumbadilisha, ni bora ukaanza maisha yako kwa sababu kuna siku hali itakuwa mbaya.”
Huu ni ushauri ambao unaweza kumuondolea mtu ujasiri wa kukabiliana na tabia ya mumewe hadi kufikia hatua ya kumsaidia akaachana na tabia zake mbaya.

Ushauri huondoa ujasiri wa kukabili tatizo hasa pale anayekushauri atakapolipeleka suala lako kwenye njia ngumu isiyokuwa na ufumbuzi. Ikumbukwe kuwa anayeamini kushindwa ni mshauri lakini wewe kama mwanamke unaweza kusimama kutetea penzi lako na kuliweka sawa mpaka jamii ikasema: “Jamani huyu dada kamrekebisha kweli mumewe, hakuwa hivi alikuwa mlevi lakini sasa kaacha pombe.

UTAKUNYIMA FURSA
Kwenye mapenzi kuna fursa nyingi za mafanikio ambazo unaweza usizipate ukiwa mtu wa kusikiliza sana ushauri wa watu. Kuna wakati ambao unatakiwa usimame wewe kuamua kumpenda mtu ambaye jamii inaona kama utapotea.

Je, Kuna Mapenzi ya Kweli Kati Yako na Mpenzi Wako?! Soma Ujue Hapa...

Katika mahusiano wengi kama si wote hupenda kuelewa mpenzi wake anampenda kiasi kipi, pengine saa ingine hata kutamani angekuwa na uwezo wa kuona nafsi ya mpenzi wake huyo ni kwa kiasi kipi penzi hilo limetawala; bahati mbaya ama nzuri haiwezekani. Hata hivyo kuna dalili katika mahusiano kati ya wawili ambazo uashiria endapo mpenzi wako huyo anakupenda ama lah. Hii huambatana na kutokana na tabia na nyenendo za mpenzi wako huyo dhidi yako.

Baadhi ya viashiria ambavyo vinaweza kukusaidia katika kutafakari ama kutambua endapo Mpenzi wako huyo ni kweli anakupenda.

Mawasiliano egemezi kati yenu (Communication)
Hii ni mawasiliano kwa njia za viwezesha mawasiliano hasa simu. Sasa hivi mawasiliano yamerahisishwa mno ikiwa na njia nyingi kama vile kupiga simu, njia za messages hasa kama vile Whatsapp, Viber, Skype na text messages. Kwa yeyote aliye na simu ya mkononi ni rahisi kuwasiliana na mpenziwe wakati wowote ule.


Mawasiliano ni njia moja wapo ya muhimu sana katika kujenga na kuboresha mawasiliano kati ya wapenzi. Inapotokea mawasiliano hayo yame elemea Zaidi upande mmoja siku zote; hapo kidogo ni tatizo. Kimsingi mawasiliano hupaswa kuwiana (mtu na mpenzi wake wote watafutane kwa usawa) ingawa inaweza pishana kidogo tokana na sababu mbali mbali. Ila inapotokea siku zote mpenzi wako huyo katka mawasiliano hufanya haya;

– Hakutafuti siku zote hadi uanze wewe.
– Kukukatia simu na kukuzimia bila maelezo yoyote ya msingi.
– Kuwa mkali kila ukimtafuta, kukuonyesha kana kwamba simu zako kwake ni kero.
– Kuchukua mda mrefu kujibu jumbe zako ama kutojibu kabisa na hata ukimuuliza hakuna sababu za msingi.
*Kwa baadhi ya tabia hizo katika mawasiliano ni dalili ambazo zinachangia kuonyesha kuwa mpenzi wako huyo hakupendi. Na hasa ikiwa tabia hizo zote anazo zote.

Ushirikiano egemezi kati yenu

Ushirikiano ni muhimu baina ya wapenzi katika masuala yale ambayo ni msingi katika maisha yenu; kila mmoja anapaswa kushiriki na kujitoa kwa mpenzi wake kwa yale yote ambayo huitaji ushiriki kwa mpenziwe. Ushirikiano hu upo wa aina mbili 

Kuna ushirikiano wa hali:-
Ushirikiano huu ni namna ambavyo wewe na mpenzi wako hushirikiana hasa katika mambo ya kijamii, kijamaa, kifamilia nakadhalika; ya wale na vile vilivyokuzunguka. Ikiwa pale unapokua na tatizo kama vile kuugua/kuuguliwa, misiba ama matatizo mengine yoyote yeye siku zote ana sababu za kushindwa kuwa karibu yako. Na ikitokea akapata nafasi yupo juu juu akionyesha dalili za kutokua comfortable kua hapo.

Kuna ushirikiano wa Mali:-
Ushirikiano huu ni namna ambavyo wewe na mpenzi wako hushirikiana linapokuja suala la kujitoa kwa vitu vihusuvo pesa bila kujalisha kipato cha mwenzako. Ikiwa una mpenzi wako akawa na shida ama kuhitaji msaada wa kifedha ama unaohususha matumizi ya fedha (bila kujalisha ni mwanamke ama mwanaume) huwa ni muhimu kutoa msaada huo; hasa pale ambapo ni wazi kabisa mwenzio anakuwa amekwama. Kuna baadhi ya wapenzi hawezi toa msaada wa mali hata kidogo; ingawa naamini kuwa mtu yeyote yule anapokua na mtu anampenda sana ni lazima atataka kumsaidia mwenzie wakati wa shida. 
 

Taratibu za kuonana (Meetings)
Katika hiki kipengele cha Kuonana kipo katika maeneo mawili pia.
Nafasi yake ya kukuona:- 

Mtu yeyote hata kama yupo na majukumu kiasi kipi, akimpenda mwenzie (iwe kwa mwanamke ama mwanaume) atatafuta tu muda kwa ajili ya kuwa na mpenzi wake. Haijalishi huo muda utakua mfupi ama mrefu, dakika chache ama masaa, ila tu lile wazo la kutomuona mpenzi wake kwa muda mrefu na hali yupo karibu na ana uweo huo linamkosesha raha. Ikiwa mpenzi wako yupo karibu, na unajua fika anauwezo wa kukuona na kuwa na wewe mara kwa mara lakini haipo hivyo – hiyo inaweza kuwa moja ya dalili ya kutopendwa na huyo mtu (labda kuwe na sababu za msingi na iwe ni kitu cha kupita na si tabia yake).

Maeneo ya kuonana:-
Hii inahusu mpenzi wako kutotaka ufike kwake (na hali pengine anakaa peke yake ama yeye ndiye mmiliki wa anapoishi). Siku zote atataka aje kwako ama mkutane sehemu za maficho. Pia linahusu yeye kutotaka kuonekana na wewe kwa watu ama katika jamii. Yupo radhi siku zote mkutane mahala na kila mmoja aondoke vyake, ama kama ana usafiri akuchukue toka utokapo hadi pale mnapoelekea. 

Kutokuwa na chembe ya Wivu dhidi yako
Wivu ni kiungo muhimu sana katika mahusiano, mwanadamu hachagui ni wakati upi awe ama asiwe na wivu, hilo lipo ndani yetu na ni kitu ambacho hakizuiliki ikiwa kweli mtu wako wampenda. Kinachotutofautisha wote ni viwango vya wivu na namna/wapi wa kuonyesha huo wivu. Wivu haimaanishi kuwa mtu hajiamini ama kuwa ndio hampendi mwenza wake; wivu huja ‘naturally’ mana unapo mpenda mwenzako kiukweli kwa ni wazi kua mapenzi ya kweli ya viwango vya wivu ndani yake na kutaka chako kiwe chako peke yako na hivyo kutaka kukilinda chako kubaki chako siku zote.

Inaptokea mpenzi wako hana habari kabisa, na wala hashtuki ni wazi kuwa anaweza kuwa asiwe anakupenda vile ambavyo mhusika ungetaka. Ikiwa yeye haisumbui kabisa ukiwa na wengine, akikukuta na wengine, akihisi upo na wengine hapo ni wazi kuwa hakuna mapenzi yale ya dhati.

Hata hivyo ni muhimu sana kutoendekeza wivu katika mapenzi na kuwa makini kiasi cha wivu dhidi ya mpenzio. Wivu kwa kiwango ni chachu katika mapenzi, Wivu uliokithiri huwa kero tokana na tabia ambazo huambatana na wivu huo ambao mwisho wa siku huwa karaha na kero katika mahusiano. 

Kutokutambulisha kwa Ndugu, Jamaa & Rafiki
Kawaida wengi wa wenye wapenzi ambao haswa wanawapenda, hutaka ndugu, jamaa na marafiki zao wawajue na mara nyingi hata kutambulisha kabisa kuwa ni mtu wake. Ikiwa upo katika mahusiano na mtu wako hapendi kukutambulisha kwa watu wake wowote katika maisha yake hilo nalo linaweza kuwa ni tatizo. Ingawa wengi huwa rahisi kukutambulisha kwa marafiki maana yeye pamoja na marafiki zake hujuana kwa viremba. 

Sababu za Kukutafuta zinamhusu yeye tu (Selfish reasons of Meetings)
Kila akikutafuta anakutafuta sababu tu anashida toka kwako.
Kwa wanawake mara nyingi inaweza kuwa anashida toka kwako ya kitu Fulani, ama kufanyiwa kitu Fulani ama shida ya pesa. Nje ya hapo hahawahi kukutafuta kwa sababu tu kakukumbuka, ama sababu tu anataka kupumzika na wewe ama sababu yoyoye ile ambayo haimnufaishi yeye tu. Wapo na wanaume ambao pia wana wapenzi wao wanawatumia na kila wakiwatafuta inakuwa ni sababu tu wanataka kitu ama fedha toka kwa wapenzi wao.

Kwa wanaume hii mara nyingi huwa shida yake kubwa kwako ya kuonana ni kutaka kukutana kimwili. Na akishamaliza hapo basi kuonana ni tatizo hadi pale tena atakapotaka kukutana na wewe kimwili.

Anavyokuita hasa majina mbadala (The way they address you)
Hii inahusu namna atakavyo kuita mkiwa wenyewe ama mbele za watu. Kuna watu wasio na haya na ukimchekea anaweza hata muita mpenzi wake mbele yake na hata kwa wenzie majina kama demu (kwa mwanamke) ama buzi langu (kwa wanaume). Hii ni mifano tu, kuna aina ya majina mengi ambayo si busara kuyatumia, na ambayo naamini mtu ambaye anampenda na kumthamini mpenzi wake hawezi yatumia iwe yupo na mpenzi wake ama hayupo na huyo mpenzi wake.

Namna anavyo Kuthamini/Kujali/Kuheshimu
Ikiwa mpenzi wako hakujali, hakuheshimu, hakusikilizi, hakuweki kipau mblele pale panapostahili ina maana kuwa hakuthamini. Kuthamini huja tu pale ambapo kuna mapenzi ya kweli dhidi ya mtu wako. Ni kitu ambacho huwezi kulazimisha, na hata ukilazimisha kwa siku chache mwisho wa siku mhusika atachoka kujifanya anakuthamini na hali hakutamini. Thamini inatokana na neon thamani… Kile kilicho na thamani siku zote mtu kukitunza kwa uangalifu, upendo na kujali kwa hali ya juu sana. Mtu anaye kuthamini ni lazima atakuheshimu na kukukali, ila si lazima kuwa mtu anaye kujali na kukuheshimu atakuthamini. Mpenzi wako akikuthamini, siku zote atakua karibu na wewe, atajali hisia zako, atajali afya yako na atajali yote yale ambayo ni msingi kwako na wale wote waliomzunguka.


Tendo la ndoa (Sex)
Hili la tendo la ndoa linaweza kutazamwa kwa namna mbili
*Ikiwa hashirikiani na wewe kwa lolote lile (hali na mali), hakuthamini na tabia zote ambazo huonyesha kutofurahia kuwa na wewe wakati wowote ziku zote LAKINI linapokuja suala la kukutana kimwili ndio hulipa kipaumbele. Hapo ni tatizo. Inakuwa ni wazi hukuhitaji tu kwa sababu ya kukidhi haja zake za kimwili.

*Ikiwa hashirikiani na wewe kwa lolote lile (hali na mali), haonyeshi kuthamini na tabia zote ambazo huonyesha kutofurahia hayo mahusiano hasa kama pia ana tabia ya kukutafuta tu pale ambapo yeye ana shida; inapotokea ukitaka kukutana nae kimwili anasita/hapendi/hafurahii ama kutokua na ushirikiano mzuri katika tendo – hapo ni wazi pia kuwa hakupendi ila anakutumia tu.


MSOMAJI NAOMBA ZINGATIA
Mawazo yangu ya nakala hii ni muhimu sana na ina nguvu Zaidi kwa wale ambao wapo katka mahusiano kati ya wawili. Kwa maneno mengine, ikiwa upo katika mahusiano ambayo unajua kabisa kuwa nyie kama wapenzi wa huyo mpenzi wako mpo Zaidi ya mmoja kuna masuala ambayo yametajwa hapa na hayawezi tumika kama kigezo cha kuelewa endapo mpenzi wako huyo ni kweli anakupenda ama lah.

Ikiwa unahisi mpenzi wako hakupendi, hiyo si lazima ikawa ticket ya maamuzi ya kusonga mbele. Unaweza chukua baadhi ya hatua ili kuboresha hayo mahusiano na yakaenda kwa mtindo ambao wote wawili mnaweza yafurahia. Ikumbukwe kuwa kila mmoja anapo ingia katika mahusiano huingia na mtu mwenye tabia mpya, jamii iliyomsunguka mpya na kadhalika; na hivyo kuanza upya kuyajenga mahusiano mengine. Hivyo ni bora ukajitahidi kurekebisha ulipo (hasa kama kweli unampenda) na pale inaposhindikana yapaswa ukubali na kusonga mbele.

Ndugu msomaji naona maoni yako, mitazamo yako, kama kuna mahala hukubaliani, kama kuna mahala pa kuongeza ama lolote lile ushiriki katika huu mjadala.
Usikose kukutana namimi katka makala ijayo….
Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top