Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

BREAKING NEWS: MKUU WA SHULE YA LUCKY VICENT AFUNGUKA MAZITO NA SIRI HII NZITO YA SHULE YAKE..

Wakazi wa Rhotia, wilayani Karatu mkoani Arusha
Wakazi wa Rhotia, wilayani Karatu mkoani Arusha wakitazama basi dogo lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Lucky Vicent ya jijini Arusha baada ya kutumbukia kwenye korongo la Mto Marera, Kata ya Rhotia jana. Picha na Mpiga picha wetu 

By Waandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Arusha/Mikoani. Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Lucky Vicent Academy waliyokuwa wanasoma wanafunzi 32 waliofariki dunia kwa ajali jana, Longino Vicent amesema ndiye aliyesimamia safari iliyosababisha vifo vya watoto hao na wafanyakazi watatu.
Vicent amesema wanafunzi hao na walimu wawili pamoja na dereva waliofariki, walianza safari yao saa 12:30 asubuhi kuelekea Karatu ambako watoto hao walipaswa kufanya mtihani wa kujipima uwezo na wale wa Shule ya Tumaini.
“Mimi ndiye niliyesimamia safari hiyo na niliwasafirisha waliondoka hapa saa 12; 30 asubuhi, sikufikiri kama yatatokea haya. Kila kitu kilikuwa salama tu,” alisema akisimulia walivyoanza safari watoto hao kabla ya gari walilopanda aina ya Toyota Costa lenye namba za usajili T 871 BYS kupinduka korongoni na kusababisha vifo hivyo.
Mwalimu Longino alisema shule hizo mbili zimekuwa na tabia ya kufanya mitihani ya ujirani mwema na kuwa hiyo ni mara ya tatu.
“Huu ni mwaka wa tatu, hata shule ya Tumaini huwa inakuja Arusha,” alisema.
Mwalimu huyo alisema shule hiyo ilikuwa ya kwanza kimkoa mwaka 2004 na ya 20 kimkoa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.
Wanafunzi hao waliofariki dunia walikuwa wakisoma shule hiyo ya bweni ambayo kwa mujibu wa wakazi wa Arusha ni miongoni mwa shule bora na iliyotoa mwanafunzi bora katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga alisema eneo la ajali lina kona nyingi na mteremko mkali na kwamba, kuna maeneo ambayo yamekuwa yakisababisha ajali kutokana na miundombinu yake ilivyokaa.
Aliyataja eneo jingine kuwa lipo barabara ya Morogoro kwenda Dodoma linaloitwa Makunganya lina utelezi mwingi na kuwasihi madereva kuwa makini sana wakati wa mvua. Wanafunzi waliofariki ni wa darasa la saba.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro alisema miili ya wanafunzi hao itaagwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid leo.

HABARI NZITO NCHINI: YULE WAZIRI MWENYE UMRI MDOGO ZAIDI AUWA KIKATILI AKINGIA IKULU HIVI PUNDE




Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu. 
Abas Abdullahi Sheikh Siraji aliyekuwa na miaka 31 ameuawa karibia na ikulu ya Rais. 

Abas Abdullahi Sheikh Siraji hakuwa waziri wa kawaida nchini Somalia. 
Alipata umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge na kuiwakilisha Jubbaland. 

Amewahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo nchi jirani ya Kenya akiwa mtoto na kisha kurejea nchini mwake mwaka jana alipokwenda kwa ajili ya uchaguzi mkuu. 

Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi huku watu wengi wakimtaja kama mtu machachari sana miongoni mwa mawaziri. 

Saa chache kabla ya kuuawa kwake alizindua mradi wa ujenzi wa jengo kwa ajili ya watumishi wa umma. 

Waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo wamekamatwa.

RAIS MAGUFULLI KIBOKO ATUMA UJUME HUU MZITO KWA MPOTO BAADA YA KUTUKAMWA...

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amedai kuwa amekuwa akitukanwa matusi pamoja na kutupiwa maneno ya kejeli tangu aonyeshe nia yake ya kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli.

Msanii huyo ambaye huwa anafanya sho nyingi za Ikulu, amesema yeye ataendelea kumuunga mkono Rais huyo kwa kuwa ni kiongozi ambaye anawapigania wananchi wa chini.

“Nimepokea matusi mengi, kebehi, na maneno machafu juu ya mimi kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli, kitu ambacho nakiamini kuna “KUKUBALIANA KWA KUTOKUBALINA” lakini kumtukana mtu mwingine sio busara hata kidogo, kwa kuwa tu hakusema au hakufanya ambacho nafsi yako ilipenda kusikia,” ameandika Mpoto kupitia mtandao wa Instagram.

“Kilichonifanya niandike ujumbe huu ni kuwa nisiwekewe maneno mdomoni yakuwa nimesema Rais Magufuli ni Mungu, kwa wale ambao hawakuangalia sherehe za MEI MOSI jana, naomba niseme kuwa hayo maneno siyo kweli na yamebadilishwa kutoka kwenye ukweli wa nilioyasema. Mimi ni mtu mwenye hofu na Mungu siwezi kusema hivyo,” ameongeza.

Mpoto amedai kuwa imekuwa ni tamaduni kwa baadhi ya watu kuwashambulia watu ambao wameonyesha nia ya kumsapoti Rais Magufuli.

“Kumekuwa na utamaduni ikitokea mtu anauunga mkono utendaji wa Rais kunaibuka kundi la wapinga maendeleo na kuanza kutukana. Naomba ijulikane kuwa sababu za kumunga mkono Rais, yale niliyokua nayaongea huko nyuma naona yanafanyiwa kazi hivi sasa!! MRISHO MPOTO mpaka sasa namuunga mkono Rais MAGUFULI.  Iwe nachumia tumbo kama inavyosemwa au nimevimbilwa kwa shibe,” ameongeza Mpoto

BREAKING NEWS: UJIO MPYA WA ROMA MKATOLIKI WAITIKISA SERIKALI AANZA NA UJUMBE HUU MZITO MNO..

Staa asiyechuja wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amefunguka kuwa katika maisha yake ya kimuziki, hajawahi kuwa na nidhamu ya uoga kama ambavyo baadhi ya watu wanavyomponda.

Roma alifunguka hayo wikiendi iliyopita alipokuwa akipiga stori na Uwazi Showbiz kufuatia maneno kutoka kwa mashabiki wake kuwa muziki wake utachenji kutokana na hofu, tofauti na alivyozoeleka kuwa na mashairi makali ya kuikosoa serikali.

“Kamwe sijawahi kuwa na nidhamu ya uoga maishani mwangu, kinachotokea kwa sasa ni mabadiliko tu ya muziki wangu, siwezi kuimba siasa kila siku, ukweli ni kwamba kwa kuimba siasa kila siku zinafanya muziki wangu usiwe wa kimataifa na uwe ni muziki wa ndani,” alifunguka Roma ambaye bado hajapona makovu aliyoyapata

TAARIFA NZITO: HAKUNA ALIEAMINI HAYA HUKUMU YA BABU SEYA,PAPII MAPYA YAIBUKA LEO HII.


Tumaini jipya! Mtoto wa kiume wa mfungwa anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking ‘Babu Seya’, Mbangu Nguza ameibuka na kusema kuwa, mwaka 2017 ndiyo wa mwisho kwa baba yake na mdogo wake, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kuendelea kutumikia kifungo chao cha maisha jela.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Amani mwanzoni mwa wiki hii, Mbangu alisema kuwa, turufu ya mwisho ya hukumu ya ndugu hao ipo kwenye mikono ya Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR) yenye makazi yake jijini Arusha ambayo kimsingi vikao vitatu vya awali vimeshakaa na kubaini kuwa, hukumu ya Babu Seya na Papii ilikuwa na kasoro.

“Unajua watu hawafahamu, kule ambako hukumu ya mzee na bwana mdogo (Papii), ilipelekwa kuna hatua. Kwanza kabisa, wale majaji wanatoka nchi mbalimbali, kwa hiyo siyo kwamba wanakwenda tu Arusha na kupitia hukumu, hapana.

“Kilichofanyika ni kwamba, kuna watu walikaa mara tatu kupitia hukumu ili wajiridhishe kama kuna makosa ambayo majaji wakikaa watayaona?



“Kwa hiyo vile vikao vimeshakaa mara tatu zote na kubaini kuwa, kweli hukumu ya baba na bwana mdogo ilikuwa ina kasoro.

“Sasa ndiyo majaji wameitwa ili kupitia na kutoa hukumu yao ya haki. Hii kazi ingekuwa imeshafanyika muda mrefu ila sasa, kilichotokea ni kwamba, kuanzia Novemba mwaka jana kama sikosei, watu wa mahakamani walikuwa likizo ndefu mpaka kwenye Februari mwaka huu, ndiyo wamerudi.

“Kingine kimechelewesha ni mwaka jana kustaafu kwa rais wa ile mahakama, Jaji Augustino Ramadhani (kutoka Tanzania), kukawa na kitambo cha kusubiri kumpata rais mpya, tayari yupo (Sylvain Ore kutoka Cote d’Ivoire).

“Kwa hiyo bwana, baada ya sasa, wakati wowote ule, majaji watatua Arusha na kukaa kupitia, naamini, tena narudia kusema, naamini, baba na bwana mdogo wangu mwaka huu watakuwa huru.

“Hili suala la wao kuwa huru liko pia kiroho, hata kama mahakama hiyo isingekaa, bado wale ndugu wangetoka tu, lazima. Kwani Mungu ninayemtegemea mimi ameshaniambia watatoka,” alisema Mbangu ambaye kwa sasa ni Mwinjilisti wa Neno la Mungu.


TUMEFIKAJE HAPA?

Nguza na wanawe watatu walikamatwa Oktoba 12, mwaka 2003 na kufikishwa Kituo cha Polisi Magomeni, Dar, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16, mwaka 2003 wakituhumiwa kubaka na kunajisi watoto 10.

Baada ya kusikilizwa kesi hiyo Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye kwenda jela maisha kwenye Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.

Januari 27, mwaka, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu.

Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao, Mabere Nyaucho Marando walikata rufaa ya pili ambayo ilitupiliwa mbali.

Mwaka 2010 waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari, 2010. Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha, ikawaachia huru watoto wake, Mbangu na Francis Nguza.

BREAKING NEWS: SIRI NZITO YAFICHUKA PROF LIPUMBA AUMBUKA VIBAYA ABAINIKA KUHUSIKA TUKIO HILI ZITO LA KIKATILI.

Sasa si siri tena,kuwa wale waliovamia mkutano wa CUF-Maalim pale Vinna Hotel Mabibo,ni wafuasi wa Profesa Lipumba na zoezi zima liliongozwa na Kambaya toka ofisi za chama Buguruni.

Walioshiriki zoezi hilo,wengi ni wale waliohusika "kuuvuruga" mkutano wa CUF pale Ubungo Plaza wakati Prof Haruna Lipumba alipoamua kuingia kwa nguvu,kuvuruga mkutano,kuvunja viti na kuzabua watu makofi.

Aliyevunjwa mguu kwa kudhaniwa ni "jambazi" na wale "wananchi wenye hasira kali" ni mlinzi wa Prof Lipumba ambaye amekuwa naye katika mikutano na misafara mingi azungukayo Dsm na nje ya Dsm.Hata alipopigwa na kupigika,aliomba msamaha kwa kusema yeye aliyumwa tu na Prof Lipumba,anaomba raia wasimuuwe.

Gari mbili aina ya Land Cruiser zilizotumika kuvamia eneo la Hotel na kutokomea mara baada ya wananchi kuingilia kati,zimekutwa ofisi za CUF-Buguruni ambazo kwa sasa zipo chini ya himaya ya CUF ya Lipumba na wafuasi wake chini ya Abdul Kambaya.Magari yote yamevunjwa vioo na kujaa damu zilizotokana na vipigo toka kwa wananchi.
Msemaji wa CUF ya Lipumba ndugu Kambaya yeye alipoulizwa,kwanza alikubali kuwa magari hayo ndiyo yalikuwa Vina Hotel-Mabibo,na walioanza kuyavamia ni wafauasi wa Chadema waliokodishwa toka Arusha kuja kuivuruga CUF ya Lipumba,anasema ni kweli magari hayo na watu waliokuwa ndani yake walivamiwa na wahuni wa CHADEMA walioletwa toka Arusha kwa ufadhiri wa Meya wa Ubungo kuja kumuondoa Lipumba ofisini.

Kambaya anasema vijana wa CHADEMA waliotolewa Arusha kuja kuleta vurugu Buguruni,ndio walianza kuwavamia walinzi wa CUF waliokuwa katika doria ya kawaida ya kuangalia wapi CHADEMA na vijana wao wanakutana ili kutengeneza fitna za kumuondoa Prof Lipumba kwa nguvu pale Buguruni.

Kambaya anasema wao kama CUF hawatakubali uhuni huo uliofanywa na CHADEMA na Meya wa Ubungo kwa kushirikiana na Maalif Seif,wao kama vijana wapo tayari kukilinda chama chao kwa nguvu zote,wapo tayari kulipa kisasi na kusimamia chama chao.

Abdul Kambaya anasema magari hayo ya chama yapo ofisi za CUF Buguruni na wanayaacha kama ushahidi wa namna wahuni wa CHADEMA toka Arusha wakishirikiana na Meya wa Ubungo wanavyotaka kuivuruga CUF kwa pesa za mafisadi.

HABARI NZITO: SIRI NZITO YABAINIKA WALIOVAMIA MKUTANO WA CUF WANASWA WAFUNGUKA MAZITO MNO.


KUFUATIA Kundi la watu wasiofahamika waliokuwa wamevalia kininja wakiwa na MAPANGA na BASTOLA moja kuvamia mkutano wa Chama Cha Wananchi (CUF) na kudaiwa kuwapiga viongozi na wanahabari. 

Katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kinondoni na Mjumbe wa Baraza Kuu Mhe. Juma Mkumbi alikuwa anazungumza na Vyombo vya Habari katika Hoteli ya Vina iliyoko kata ya Mabibo, Dar ambapo baada ya tukio hilo la kutisha, wananchi na wafuasi wa CUF waliokuwa eneo la tukio walitaharuki. 

KUHUSU KUNDI LA LIPUMBA KUVAMIA VIONGOZI WA CHAMA… Wengi mmeniuliza kuhusu viongozi wa CUF kuvamiwa, ni kweli. Leo Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kinondoni na Mjumbe wa Baraza Kuu Mhe. Juma Mkumbi alikuwa anazungumza na Vyombo vya Habari katika Hoteli ya Vina iliyoko kata ya Mabibo, Dar. 

Ghafla mkutano wake ukavamiwa na kundi la Lipumba liitwalo MUNGIKI. Wavamizi hao walivalia kininja wakiwa na MAPANGA na BASTOLA moja. Wavamizi wakaanza kuwapiga viongozi na wanahabari wakiwatuhumu kuwa kwa nini hawamuungi mkono Lipumba.Waandishi Na kadhaa na viongozi kadhaa wamejeruhiwa, kuporwa simu zao, kamera, vitendea kazi, fedha n.k. Wananchi wa Mabibo waliposikia mayowe na kelele za kuomba msaada walipandisha ghorofani (kwenye PRESS) ili kutoa msaada. 

Kuona wananchi wanakuja kwa wingi, kundi la MUNGIKI likaanza kushuka mbio kuelekea kwenye magari mawili waliyokuja nayo. Baadhi ya Mungiki hawakuyafikia magari na wakazidiwa nguvu na wananchi. 

Huyu aliyeko pichani ni Mungiki mmojawapo aliyedhibitiwa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kumkimbiza na kumkamatia mitaanu ambapo inasemekana amevunjwa kisigino na mfupa umetokea nje (So sorry and sad). Huyu wa pichani pia ni mmoja wa walinzi wa Lipumba na mara nyingi huwa pamoja na Lipumba. Bahati nzuri, vyombo vya habari vimemhoji mbele ya wananchi na amekiri kuwa UVAMIZI walioufanya umetokana na maagizo ya LIPUMBA. 

Chama chetu kimekwishatoa taarifa rasmi kwenye vyombo vya habari (unaweza kuisoma kwenye ukurasa wangu wa FB). Tumestushwa na kusikitishwa sana na tukio hili baya na la aibu kabisa. 

Chama chetu kimetoa pole kwa waandishi wa habari na viongozi wa majukwaa ya waandishi na kimelitaka jeshi la Polisi lichukue hatua za haraka dhidi ya LIPUMBA na genge lake lijiitalo MUNGIKI. 

#Mtatiro J 


annayesayaDuuu inasikitisha hapo lipumba hayupo wewe unavunjwa kiuno nyie vijana acheni siasa chafu on a sasa umepata chai ya kutoshajr.huseniNae process uchwara ama kweli kisicho riziki hakilikimmahmoudjabirMasikini roho yake

HABARI NZITO: JAJI LUBUVA TABOA SIRI ILIYOKUWA NZITO UCHAGUZI 2015 ADAI ALITISHIWA MAISHA AMTANGAZE...


MWENYEKITI Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva amefichua mambo mbalimbali aliyokumbana nayo katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. 

Jaji mstaafu  Lubuva, aliteuliwa kushika wadhifa huo mwaka 2011 na kustaafu Disemba mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage, amebainisha kuwa uchaguzi huo wa mwaka 2015 hatousahau kutokana na kuwapo kwa ushindani mkubwa.

Akizungumza  nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam, alisema mazingira ya ushindani wa kivyama katika uchaguzi huo yalimsababishia hata baadhi ya ndugu zake kumnunia.

Alisema tangu mfumo wa vyama vingi uanze mwaka 1992, uchaguzi wa 2015 ulikuwa na ushindani mkubwa kuliko chaguzi zote zilizofanyika nchini.

“Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, Agustino Mrema alileta changamoto kama mtu binafsi si chama, mwaka 2015, hali ilikuwa ni nzito kwa kuwa ushindani ulikuwa wa vyama zaidi. Hata hivyo nashukuru Mungu tulimaliza kwa amani, hata watazamaji waliona uchaguzi uliisha kwa amani na baadhi yao nilikuwa nashirikiana nao. Nakumbuka walipokuwa wanaona kampeni walinieleza kuwa ushindani utakuwa mkubwa, najivunia kumaliza uchaguzi ule kwa amani.

“Wakati naingia NEC tulianzisha uandikishaji wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa BVR. Mfumo huo ulikuwa na changamoto zake mojawapo ikiwa ni ucheleweshwaji wa vifaa kwa kuwa vilichukua muda kufika nchini huku Oktoba ilikuwa inakaribia, hata hivyo tulijitahidi kuandikisha kwa kutumia mashine  zilizofika kwa kuhamisha hamisha. Hata wadau wetu walishangaa tumefanikiwa vipi kuandikisha watu milioni 23 kwa muda mfupi ule,” alisema.

 KUNUNIWA NA NDUGU

Alisema kutokana na ushindani huo wa kivyama, baada ya matokeo baadhi ya ndugu zake walimnunia kwa kudhani kuwa haki hakutendeka jambo ambalo halikuwa na ukweli.

“Hata watu wengine ambao ni ndugu zangu walinuna, waliona hawakutendewa haki, lakini ndio kura kwani kwa mujibu wa kura Magufuli ndio kashinda.

“Katika uchaguzi wowote kuna mawili kushinda na kushindwa, anayeshindwa mara nyingi hawezi kuzungumza vizuri juu ya uchaguzi. Ila niseme uchaguzi ule uliendeshwa kwa taratibu na kanuni za uchaguzi, si kweli kwamba kura ziliibwa, kwa sababu tuliendesha uchaguzi kwa uwazi. Kwa mara ya kwanza kura za rais ziliwekwa wazi kwani vituo vyote vilibandika matokeo, hivyo mpiga kura anajua mgombea wake amepata nini ndipo tunaletewa huku Dar es Salaam tunajumlisha na kutangaza.

“Pia mawakala wao wanakuwapo na wanajua mgombea wao amepata kiasi fulani, hivyo niseme kuwa hakuna sehemu jimbo wala wilaya kwamba kura za mgombea urais ambazo zilitangazwa makao makuu hapa Dar es Salaam  ambazo zilikuwa batili. Hivyo unaposema kura zimeibiwa ushahidi upo wapi? Ndio hicho ninachozungumza wakati wote kuwa kadiri matokeo yanapokuja ndivyo nilivyokuwa nayasoma,” alisema.

KUTISHIWA MAISHA

Aidha, Jaji Lubuva alisema licha ya kuwapo baadhi ya kundi la vijana waliomtishia kumuua iwapo kungetokea matokeo wasiyoyataka, anamshukuru Mungu uchaguzi huo ulifanyika kwa amani bila vurugu na kamwe hakuwa na hofu.

“Sikuwa na hofu, tunajua baadhi ya vyama walikuwa na sehemu zao wanaita Ngome, walikuwa wamejiandaa sana kwamba labda kufanya fujo ila nilikuwa nimejiandaa vizuri kwani hata hivi vyama vya upinzani kwa ujumla walishirikiana na chama tawala baada ya matokeo. Kama kweli wangedhamiria kufanya fujo basi wangewachochea vijana wao, na kwa sababu sikufanya lolote baya ndani ya utendaji wangu hapakuwapo na uvunjifu wa amani. Kuna baadhi ya vijana walikuwa wanatishia kuniua iwapo ningetangaza matokeo tofauti na walivyokuwa wakitaka lakini bahati nzuri hapakuwapo na lolote uchaguzi uliisha kwa amani,” alisema.

Licha ya baadhi ya Watanzania kudai kuwa NEC si huru, Jaji Lubuva alisisitiza kuwa Tume hiyo ni huru kwani hata katika kipindi cha uongozi wake hapakuwahi kutokea wito wa Rais kuwataka viongozi hao wafike Ikulu.

 “Nimelizungumza sana tangu nimeingia pale, kwamba yapo madai kwamba Tume si huru, nimesema kwamba hizi ni hisia kwamba Jaji Lubuva ni mteule wa rais na mkurugenzi na makamishna ni wateule wa rais, pia wakati rais huyohuyo ni mwenyekiti wa chama. Lakini siku zote nilisema tume inafanya kazi zake kwa uhuru, hakuna siku yoyote tumeingiliwa na rais na hata sasa nimeicha NEC ikiwa huru. “Kwa sababu tumekuwa tukishirikiana na tume za nchi za EAC na SADC baadhi yao wanajiita tume huru, ila sisi hatukujiita jina hilo ila niwahakikishie kuwa tume yetu ni huru kabisa.

 “Kama mtakumbuka Tume ilikwenda kwa Jaji Warioba kipindi cha kuandaa rasimu ya Katiba, tukawasisitizia kuwa tunafanya kazi kwa uhuru ila kuondoa hayo maono ni vyema kuangalia namna ya kubadilisha kidogo vifungu vya sheria. Kwa sababu pamoja na rais kuteua makamishna, mkurugenzi na hata Jaji mkuu hapakuwapo kabisa na mwingiliano wowote, tangu niwapo pale hata siku moja hatukuwahi kuitwa na rais Ikulu,” alisema

KALI KULIKO KAULI YA ZITO BAADA YA MAUWAJI YA ASKARI KIBITI YAZUA GUMZO ZITO BUNGENI.



Baada ya vifo  vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha tarehe 13 Aprili, 2017 katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Jana Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe  kupitia akaunti yake ya Twitter amesema haya juu ya Polisi 8 waliouawa

Mkuranga, Kibiti na Rufiji ( #MKIRU ) ni eneo ambalo lazima kazi kubwa ya ujasusi wa kiusalama ifanyike. @mwigulunchemba1 simamia hili haswa
Nimetazama magazeti makuu Leo, English and Swahili, naona uzito wa usalama wa eneo la #MKIRU unakuwa mdogo. Makosa makubwa @mwigulunchemba1

HABARI NZITO: UJUMBE WA MH LOWASSA WALITIKISA TAIFA AFUNGUKA MAZITO JUU YA TUKIO HILI ZITO NCHINI.

Mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP), Ernest Mangu, jana wameshiriki ibada ya Pasaka katika Kanisa la Azania Front na kuwataka Watanzania kudumisha upendo na amani.

Pia, viongozi hao walionyesha kusikitishwa na vifo vya polisi wanane na kuitaka jamii kulisaidia jeshi hilo liweze kupambana na uhalifu.

Alhamisi iliyopita, polisi wanane waliuawa na watu wasiofahamika katika eneo la Jaribu wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akizungumza jana mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sikukuu ya Pasaka katika kanisa hilo, Lowassa alisema tukio hilo ni la kutisha na kusikitisha.

“Natoa pole kutokana na vifo vya askari polisi vilivyotokea hivi karibuni lakini nawaomba wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuwabaini waliofanya uhalifu huo,” alisema.

Alisema Polisi wasikatishwe tamaa na vitendo hivyo vya kihalifu bali wajiimarishe ili waweze kukabiliana na uhalifu kwa kuwashirikisha wananchi.

Akitoa ujumbe wa Pasaka, Lowassa aliwataka wananchi kudumisha upendo na amani kama ambavyo mafundisho ya dini zote yamekuwa yakielekeza.

“Tusherehekee Sikukuu ya Pasaka kwa upendo na amani,” alisema.

Akizungumza mara baada ya ibada hiyo, IGP Mangu aliwataka wananchi kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa amani na utulivu huku akiwahakikishia usalama wa kutosha.

“Tumeimarisha ulinzi wananchi wasiwe na wasiwasi washerehekee sikukuu hizi wakifahamu kuwa tuko pamoja nao,” alisema.

Hata hivyo, Mangu alisema wananchi bado wana mchango mkubwa kulisaidia Jeshi la Polisi kukabiliana na uhalifu kwa kutoa taarifa.

“Wananchi wema ni wengi kuliko wahalifu. Tushirikiane na Jeshi la Polisi kukabiliana na vitendo vya kihalifu kwa kutoa taarifa zinazohusu mienendo ya watu tunaowatilia shaka,” alisema.

Waziri mkuu aliyetumika kwa miaka yote kumi katika Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye, aliwataka wananchi kuishi bila kubaguana na kudumisha upendo.

“Wakati tukisherehekea sikukuu ya Pasaka naomba niwaase wananchi kuishi kwa upendo, tusibaguane na tuimarishe mshikamano wetu,” alisema.

Alisema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuwaunganisha wananchi ili waishi kwa kushirikiana.     

HABARI NZITO: HII NI NOUMA SANA MBOWE NA SIRI NZITO MNO YA MAUWAJI YA ASKARI POLISI KIBITI.

Juzi Mh Mbowe katoa hoja ya bunge kujadili usalama wa wananchi kutokana na kushamiri kwa matukio ya kihalifu ya mauaji na utekaji.

Wabunge wa CCM wakiongozwa na Jenista Mhagama wakapinga na kusema Tanzania ni salama kuwa bunge lina mambo mengi ya kujadili. Hayajapita hata masaa 12 askali 8 wamevamiwa na kuuawa, bado kina Mhagama wanasema Tanzania ni Salama.

Nataka kuwaambia CCM kuwa endeleeni na dharau zenu, mnayoyataka soon mtayapata na siku yakiwakuta hakutakuwa na mtu wa kuwasemea wala kuwaonea huruma.

HII NOUMA SANA AGIZO LA RAIS MAGUFULI LAMUIBUA PAUL MAKONDA AFUNGUKA MAZITO MNO.

MAGUFULI
RAIS John Magufuli ameagiza maeneo yote zilipokuwa nyumba za kota yarudishwe katika miliki ya serikali ili zijengwe nyumba kwa ajili ya makazi ya wananchi. Aidha, amezitaka Halmashauri zilizopanga kuuza maeneo hayo kwa kigezo cha uwekezaji kutafuta maeneo mengine.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akiweka jiwe la msingi katika eneo la Magomeni Kota, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 644 za waliokuwa wakazi wa eneo hilo na kusema wakati akiahidi baadhi ya watu walidhani hatatekeleza.
“Niliamua kutoa maagizo kwenye maeneo yote yaliyokuwa yakifanana na Magomeni Kota, Ilala na kwingine yawe chini ya serikali, maana yake yawe chini yangu na pasitokee wa kuyauza. Temeke walianza mchezo wa kutaka kummilikisha mchina kwa kisingizio cha uwekezaji wanaingia uwekezaji, nimesema wakatafute maeneo mengine,” alisema.
Alisema nyumba hizo zitakapokamilika wakazi 644 waliokuwa wakiishi katika eneo hilo kila mmoja atakabidhiwa funguo yake. Alisisitiza kuwa wakazi hao watakukaa bure kwa miaka mitano. “Haiwezekani ndani ya Tanzania inayoheshimu uhuru wa masikini na tajiri ifikie mahali ambapo masikini akikaa mahali pazuri aambiwe aondoke.
Matajiri na masikini wote wanahitaji kuishi mjini,” alisema. Rais alisema hakuna Mtanzania wa daraja la kwanza, la pili au la tatu, ndio sababu majengo hayo yakajengwa katika maeneo hayo na kipaumbele kitakuwa ni watu hao 644.
Akizungumzia maeneo mengine alisema serikali itakayoyachukua itafanya vivyo hivyo, kwani Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume aliweza kujenga nyumba kama hizo katika miaka ya 1970 hivyo haiwezekani wanaojenga sasa washindwe.
Rais Magufuli alisema, Serikali itaanza kujenga nyumba kwa mtindo huo katika maeneo mengine yakiwemo Ilala, Temeke, Iringa, Mwanza, Dodoma na maeneo mengine nchi nzima.
Alisema Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inamuagiza kuimarisha makazi ya wananchi na haikubagua mwananchi wa aina gani na nia yake ni kuleta maendeleo bila kujali itikadi za vyama vya siasa.
Aliupongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kazi unayoifanya nakuongeza kuwa kwa Sh bilioni 20 kujenga majengo hayi ni jambo kubwa. “Ukikuta majengo mengine yanazungumzwa yamejengwa kwa mabilioni mengi ndugu zangu mjue hapo tumeliwa, kwa sababu kama haya majengo ya ghorofa nane, hapo tisa na 12 halafu bilioni 20 zinajenga awamu ya kwanza, mnaweza mkaona ni kwa namna gani ninaposimamia serikali hii kubana matumizi.
Hii ndio maana yake,” alisema. Alisema kama tenda hiyo angekuwa amepewa mtu angeweza kudai bilioni 300. Awali, Waziri Lukuvi alisema tayari ameshaunda timu ya watumishi wa wizara hiyo kutembelea maeneo yote kwa ajili ya kuyaainisha yaweze kutengezewa hati na kukabidhiwa kwa Rais Magufuli kufikia Mei mwishon

HABARI NZITO:HAKUNA ALIEWEZA KUAMINI TUKIO HILI TENA BEN SAANANE ALITIKISA TAIFA SOMA WARAKA HUU MZITO.



SIKU chache baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, kuliambia Bunge kuwa Serikali haijui kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ben Saanane aliko na zaidi akipinga taarifa za kutekwa, familia ya kijana huyo imesema juhudi zao za kumtafuta zimegonga mwamba.

Akizungumza Jumamosi, baba mzazi wa Ben Saanane, Focus Saanane, ameiomba Serikali pamoja na vyombo vya dola kusaidia juhudi za kumtafuta, kwani  juhudi zao zimegonga mwamba na suala hilo lipo nje ya uwezo wao kwa sasa.

"Toka mwanangu Ben apotee imepita miezi sita na hakuna jitihada zilizofanyika za kumtafuta, hata kama zimefanyika basi nguvu ni ndogo sana, hivyo basi, sisi kama familia tunaiomba Serikali pamoja na vyombo vya dola kusaidia juhudi za kumtafuta,” alisema.

Suala la kutoweka kwa Ben Saanane liliibuka kwa mara nyingine wiki hii kiasi cha kutikisa mhimili wa Bunge, kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, hajahitimisha kwa kusema kuwa Serikali inachunguza vitendo vyote vya utekaji.

Kuibuka kwa suala la Ben Saanane kulichochewa na tukio la kutekwa kwa mwanamuziki wa Bongo fleva, Roma Mkatoliki na wenzake.

Wakati Roma na wenzake wakichukuliwa mateka kwa siku tatu na kisha kuachiwa, Saanane tangu atoweke Novemba mwaka jana hadi sasa hakuna yeyote wala chombo cha dola kinachofahamu mahali alipo.

Baba huyo wa Ben ameiomba Serikali kuongeza jitihada za kumtafuta mtoto wao.

Alisema hadi sasa familia hiyo imejitahidi kufanya uchunguzi wa sababu za kupotea kwa mtoto wao, lakini jitihada hizo hazijazaa matunda na kwamba tegemeo lao kubwa limebaki kwa vyombo vya dola na Serikali kwa ujumla.

“Sisi kama familia tumeshafanya jitihada mbalimbali, lakini hatujafanikiwa, kilichobaki ni kuiangalia Serikali ili itusaidie, maana hata tukiamua kutumia vyombo vya nje kumtafuta Ben bado tutapitia mikononi mwa Serikali, hivyo ni dhahiri kuwa Serikali ina nafasi kubwa ya kutusaidia kumtafuta,” alisema.

Pamoja na hilo, baba mzazi wa Ben aliliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano kuendelea kutumia vyema vikao vinavyoendelea sasa bungeni kuisisitiza na kuishauri Serikali juu ya umuhimu wa kumtafuta mtoto wao, kwani ni tegemeo kubwa kwa familia hiyo na taifa kwa ujumla.

Mapema wiki hii akijibu kauli za wabunge ambao walipiga kelele za kuitaka Serikali imtafute Saanane, huku wengine wakidai kuwapo kwa kikundi ndani ya taasisi za usalama ambacho kinatekeleza vitendo vya utekaji na utesaji, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alipuuza taarifa hizo.

Masaju alisema taarifa kwamba Ben Saanane ametekwa hazina ukweli, kwa sababu hakuna ushahidi wowote.

Alisema ili kuthibitisha kuwa mtu amekufa kwa mujibu wa sheria ya ushahidi lazima iwe imepita miaka mitano.

“Hatuna taarifa za Ben na haijulikani kama ametekwa au amejificha au yupo wapi. Huwezi kusema Ben Saanane ametekwa wakati huna ushahidi, inawezekana watu wasiokuwa na nia njema na Serikali hii wanafanya uhalifu kwa sababu huwezi kusema kwamba Ben Saanane amekufa.

“If you have serious information juu ya mambo ya uhalifu, pelekeni kwenye vyombo vya dola… hatuwezi kufanya hivi, sheria yetu ya ushahidi inasema ili kuthibitisha kuwa mtu amekufa miaka mitano iwe imepita, kifungu cha 100 cha sheria ya ushahidi kinaeleza hilo,” alikaririwa Masaju.

HII NDIO KAULI YA MWIGULU NCHEMA YAIBUA HISIA KAULI MNO JUU JUU YA MAUWAJI YA ASKARI POLISI.



WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi,Mwigulu Nchemba,amesema hawatokubaliana na mtandao,kundi ama mtu anaehusika na kugharimu maisha ya askari ama wananchi wasio na hatia.


Aidha amebainisha kwamba kilichombele kwa sasa ,wanaendelea kuhakikisha kuwa wanarudisha silaha zinazochukuliwa katika matukio mbalimbali ya mauaji ya askari na kuendelea na mapambano na wahalifu hao.


Nchemba ameyasema hayo jana  ,wilayani Kibiti,mkoani Pwani,na kumtaka mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo kupambana na matukio ya mauaji yanayoendelea katika baadhi ya wilaya mkoani hapo.


Waziri huyo wa mambo ya ndani ,alieleza kwamba,amepokea taarifa ya kuuwawa kwa askari nane wilayani Kibiti  kwa mshituko mkubwa .


Nchemba aliwaomba watanzania kwa kipindi hiki wawe watulivu wakati jeshi la polisi likiendelea kukabiliana na mambo hayo.


“Hii ni changamoto kwa wizara ya mambo ya ndani kuanza upya kuboresha mbinu zake za ki intelensia zinazoendana na mazingira ya sasa kwa mahitaji ya sasa”alisema.


Alibainisha kwamba,ni ngumu kuingia akili kwa watu wachache kuuwa hovyo askari ambao ndio walinzi wa raia na mali zao


“Kuna jambo lipo nyuma limejificha ambalo mwisho wake umefika kwani hatutoweza kulifumbia macho”alisisitiza.


Nchemba aliomba jamii iendelee kulinda amani ya nchi na kuheshimu askari polisi ambao wapo kwa ajili ya kuwalinda katika usalama wao.

HABARI NZITO: MAZITO YAIBUKA HAKUNA ALIETEGEMEA MKE WA ROMA NA SIRI NZITO MNO YA KUTEKWA KWA ROMA

ya madai ya mumewe ambaye ni staa wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ kutekwa na kuteswa kisha kutelekezwa akiwa na wenzake watatu baada ya siku kadhaa, mke wa jamaa huyo aitwaye Nancy ameacha gumzo kufuatia ujasiri aliouonesha katika tukio hilo.
Kwa mujibu wa watu wa karibu na familia ya Roma, Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na Roma aitwaye Ivan, alionesha ujasiri wa aina yake kwani alikuwa halali badala yake alizunguka kila kona jijini Dar akimsaka mumewe, jambo ambalo baadhi ya wanawake wasingeweza kulifanya.
“Nancy siyo wa mchezomchezo, tangu mumewe alipotekwa alikuwa halali. Alichokifanya aliomba msaada kwa ndugu zake wa kumtafuta mumewe kila kona hadi alipopatikana.
“Unaambiwa alizunguka kila sehemu bila mafanikio akimtafuta mume wake tangu aliposikia taarifa za kutekwa usiku wa Jumatano (wiki iliyopita). “Nancy alianzia Studio za Tongwe Records (Masaki), baada ya hapo hakulala, alizunguka karibia vituo vyote vya polisi Dar.
Alituma watu hadi mochwari kumuulizia mumewe na wakati huohuo akiviomba vyombo vya habari kumsaidia hadi mumewe alipopatikana, tofauti na wanawake wengine ambao wangejifungia tu kusubiri taarifa.
“Unajua watu wengi walikuwa hawamjui Nancy ni mtu wa aina gani lakini tukio la Roma limemfanya awe gumzo sana kwa ujasiri aliounesha kwenye kipindi kigumu alichopitia,” alisema mtu huyo wa karibu wa familia ya Roma. Akizungumza na Amani juu ya ujasiri aliouonesha kwenye tukio hilo, Nancy alisema kuwa, tukio hilo lilimfanya achanganyikiwe na kujikuta akihangaika kwenye vituo vingi vya polisi jijini Dar. Alisema kuwa, kilichokuwa kinamfanya achanganyikiwe na kushindwa kupata usingizi ni kwamba, kabla, hakuwahi kumpatia taarifa yoyote kama anatafutwa na polisi achilia mbali kuwa na tatizo na mtu yeyote.
Hata hivyo, Nancy aliwashukuru wadau mbalimbali pamoja na Watanzania kwa ujumla kumuunga mkono katika jitihada za kumtafuta mume wake hadi alipopatikana na bado wameendelea kutoa pole hivyo kuonesha upendo mkubwa walionao kwa baba mtoto wake.

HABARI NZITO: KIMENUKA BUNGENI BUNGE LAZIDI KUFUKUTA MOTO NAIBU SPIKA AMCHINJIA ROMA BAHARINI.

MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), amedai kupewa taarifa na mawaziri kuwa muda wowote anaweza kuuawa na kikundi maalumu kinachoendesha utekaji nchini.

Aidha, Bashe amedai kuwa mbali na yeye kuwa katika hatari hiyo, pia ameambiwa na mawaziri hao wa serikali kuwa kuna wabunge wengine 10 ambao wanawindwa na kikundi hicho na wametahadharishwa 'kuwa makini barabarani'.

Bashe (41), aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana asubuhi aliposimama na kukiomba Kiti cha Spika kuahirisha shughuli za Bunge ili kujadili hoja ya dharura akitumia Kanuni ya 47(1),(2)na (3) vya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016.

Huku akiungwa mkono na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) na kushangiliwa na baadhi ya wabunge, Bashe alisema kumekuwa kukitokea matukio ya sintofahamu yanayowahusu wabunge na raia wa kawaida yanayoendeshwa na kikundi hicho ambacho alidai kinatoka idara nyeti serikalini.

Katika kujenga hoja yake, Bashe alisema Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku (CCM), mbunge wa zamani Mkuranga mkoani Pwani, Adam Malima (CCM), msanii Roma Mkatoliki na yeye mwenyewe ni miongoni mwa watu waliowahi kutekwa huku akikumbushia pia madai ya kupotea kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Aliliomba shughuli za Bunge ziahirishwe ili wabunge wajadili jambo la dharura ambalo limekuwa likitokea kwa muda mrefu katika nchini.

"Miongoni mwa watu waliowahi kutekwa ni Mheshimiwa Musukuma (Joseph Kasheku), Mheshimiwa Bashe kwenye mkutano mkuu wa CCM, ndugu Malima, Ben Saanane amepotea... (makofi), juzi amepotea Roma Mkatoliki," alisema Bashe huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge kwa kugonga meza.

Alisema zaidi: "Nasema ni jambo la dharura kwa sababu hawa ni wale ambao wanafahamika. Hatujui Watanzania wangapi hawafahamiki katika ngazi za chini.

"Na zipo taarifa ambazo binafsi nimezipokea kutoka kwa baadhi ya mawaziri, wakinitahadharisha mimi binafsi kwamba 'Bashe kuwa makini, wewe ni mmoja kati ya wabunge 11 ambao wamewekwa katika 'list' (orodha). Mkikaa barabarani vibaya, mnaweza kupoteza maisha yenu'.

"Nasema jambo hili ni dharura kwa sababu kikundi hiki kilichomo ndani ya idara ya ... (alitaja idara nyeti), ambacho kimeamua kuchukua mamlaka haya ya kuteka watu, kinaharibu heshima ya serikali yetu, kinaharibu heshima ya chama changu ambacho mimi na wabunge wenzangu wa CCM, tuliomba ridhaa ya kutaka kuwaongoza Watanzania na siyo kuwahatarishia maisha yao."

Bashe alimuomba Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, kuruhusu jambo hilo lijadiliwe na wabunge na ikiwezekana chombo hicho cha kutunga sheria kiunde kamati maalumu ya kuchunguza jambo hilo.

Bashe pia alimuomba Naibu Spika kutumia mamlaka yake kuiagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Usalama na Mambo ya Nje kufanya kazi changamoto hiyo na kulipatia Bunge taarifa kwa ajili ya usalama wa nchi.

"Hali ya nchi siyo salama, Watanzania wana taharuki, Watanzania wanajadili mambo haya katika mitandao na 'there is no statement' (hakuna kauli) toka serikali.

Waziri wa Mambo ya Ndani..." Bashe alisema huku akikatishwa na Naibu Spika ambaye alimtaka aketi ili Kiti cha Spika kiangalie Kanuni ya 47 inaeleza nini kuhusu madai yake.

Kabla ya kutoa uamuzi wa Kiti kuhusu madai ya Bashe, Naibu Spika alitoa nafasi kwa Sugu kueleza hoja yake bungeni baada ya mbunge huyo kusimama na kuomba kupewa nafasi ya kuwasilisha hoja ya dharura bungeni.

Akitumia Kanuni ya 47, Sugu aliunga mkono hoja ya Bashe kwamba Bunge liahirishe shughuli zake za jana na kujadili hoja ya dharura ya kadhia ya utekaji na kupotea kitatanishi kwa watu nchini.

"Taifa limekuwa gizani kwa utamaduni mpya uliozuka wa kuteka watu, utamaduni ambao si wa kwetu, ni utamaduni wa kimafia, utamaduni ambao kwa mara ya mwisho kwenye mipaka ya Bara na visiwani, tuliusikia alipotekwa Mzee Kassim Hanga kule Zanzibar miaka hiyo," Sugu alisema.

"Lakini tangu kipindi hicho haujakuwapo tena. Toka operesheni hii ya kuteka watu nyara ianze, kila anayehusika na usalama likiwamo Jeshi la Polisi, 'always' (mara kwa mara) wanasema 'hatujui, hatujawaona kwenye vituo vyote'.

Nchi inabaki kwenye tahayari, kapotea Ben Saanane, mara miili sita, saba imeopolewa kwenye Mto Ruvu ikaenda kuzikwa bila kufanyiwa 'post-mortem' (uchunguzi) kwa amri ya ambaye hatujui ni nani.

"Bashe alitekwa, Nape (Nnauye) alitekwa, akaokolewa na Maulid Kitenge, vinginevyo pengine angekuwa ametekwa, hakuna mtu aliyezungumza kitu."

Kutokana na changamoto hiyo mpya nchini, Sugu alimshauri Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kuachia ngazi ili kulinda heshima yake kama kweli bado ana matumaini ya kuwa Rais wa Tanzania.

"Waziri wa Mambo ya Ndani yuko kimya mpaka najiuliza kama anabanwa kiasi hicho, huyu ni mtu 'potential' (muhimu) ambaye alifikia hatua ya kugombea urais na bado ana 'future'," Sugu alisema.

"Kwanini asijiuzulu, akalinda heshima yake kuliko kukaa kwenye 'mess' (aibu)? Alihoji Sugu. "Kujiuzulu ni utamaduni mzuri.

Mzee (Alhaji Ali Hassan) Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani miaka hiyo, mwaka '76, ikatokea messy (kuboronga), 'aka-bounce back' (akarejea), miaka ya '80 akaja kuwa Rais wa nchi hii.

"Ndugu yangu Mwigulu, nikushauri kama hushirikishwi, mambo yanafanyika, hamna mtu anakuja na majibu.
"Lakini juzi baada ya kutekwa Roma Mkatoliki, tumepata mwanga. Yupo mtu Dar es Salaam alituambia anajua Roma aliko na angerudi kabla ya Jumapili.

"Kama Waziri Kivuli (wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo), nikatoka Jumamosi na 'ku-demand' (kuagiza) kwamba aachiwe siku ileile na akaachiwa, nashukuru Mungu. Sasa basi, hatujui nani 'next' (anayefuata) atatekwa. Yawezekana Sugu ingawa mimi 'I don't care much' (sijali) kwa sababu Mbeya wataziba nafasi yangu.

"Lakini Naibu Spika 'it could be you' (yaweza kuwa wewe). 'It is the war' (ni vita), 'no body is safe' (hakuna aliye salama. Kwanini Bunge hili lisijadili na hatimaye limlazimishe Bashite kama alivyojua kwamba Roma Mkatoliki yuko wapi na angemrudisha Jumapili, tumlazimishe sasa Bunge hili tujadili na baadaye tumlazimishe Bashite atutajie aliko Ben Saanane na atutajie kwamba ili miili iliyotupwa Ruvu na kuzikwa haraka haraka bila kufanyiwa 'post-mortem' ni ya kina nani kwa sababu huyu anaonekana anajua undani wa mambo haya."

KULIPATIA UFUMBUZI
Akijibu maombi ya wabunge hao, Naibu Spika alikataa kuruhusu jambo hilo kujadiliwa bungeni kwa kupitia utaratibu wa hoja ya dharura kwa kuwa vyombo vya sheria vinaweza kulipatia ufumbuzi.

Dk. Acskon alisema jambo la dharura linaloweza kusababisha kuahirishwa kwa shughuli za Bunge kulijadili ni lile lenye maslahi kwa umma na iwapo utatuzi wake unategemea zaidi ya utekelezaji wa kawaida wa sheria.

"Waheshimiwa Bashe na Sugu wameeleza kwa kirefu kuhusu jambo ambalo limetokea hapa na pale, lakini pia tumeliona kwenye vyombo vya habari na tumelisoma," Dk. Ackson alisema.

"Maelezo yao kwa ujumla yanahusu mambo ambayo yanawapata wananchi ambayo watu kadhaa wametajwa kama mifano kwamba wamekuwa wakitekwa ama wamekuwa wakikamatwa.

"Sasa, nadhani wote tunafahamu matakwa ya Kanuni ya 47, hili jambo la hawa watu kukamatwa ama kutekwa kwa sababu sasa hata wale waliokamatwa, na wao wamewekwa kwenye kundi la kutekwa. Sasa sijui kama tunaweza kuyatenganisha haya mambo mawili; nani amekamatwa na nani ametekwa?

"Lakini maelekezo yaliyotolewa kwa kirefu ni kwamba wakati mwingine mtu akiwa haonekani, polisi ndiyo sehemu ya kwanza ambayo inaulizwa na yapo mazingira polisi haijatoa maelezo kwamba hawa watu wako wapi na mifano imekwishatajwa.

"Mheshimiwa Bashe amekwenda mbali zaidi akisema kwamba kipo kikundi ambacho kinafanya kazi hiyo.

Na Mheshimiwa Joseph Mbilinyi na yeye ameeleza kwamba hili jambo sasa limekuwa kama utamaduni kwa maana ya kwamba linatokea kila wakati na akaenda mbele zaidi na kumshauri Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Nchemba) kwamba aweze kujiuzulu akiona inafaa.

"Kanuni ya 47 huwa ni lazima isomwe pamoja na (Kanuni ya) 48 kwa sababu 48 ndiyo inayoweka masharti ya matumizi ya Kanuni ya 47.

Sasa kwa kuwa Kanuni ya 48(4) nitaisoma, inasema hivi 'jambo lolote litahesabiwa kuwa ni lenye maslahi kwa umma iwapo utatuzi wake unategemea kuwa zaidi kuliko zile za utekelezaji wa kawaida wa sheria peke yake.

"Masuala haya yaliyoulizwa na Mheshimiwa Bashe na pia yaliyoulizwa na Mheshimiwa Mbilinyi yako chini ya utaratibu wa kisheria na Bunge hili litashughulika na mambo ambayo ni yenye maslahi ambayo sheria haina uwezo wa kuyatolea majibu.

Kwa sababu hiyo, sitalihesabu hili jambo kwa mujibu wa Kanuni ya 47(4) kwamba ni jambo la dharura lakini ni jambo ambalo utaratibu wa kawaida wa kisheria unaweza ukafanya kazi. Hayo ndiyo majibu yangu kuhusu matumizi ya Kanuni ya 47.

Matukio ya kupotea, kutekwa na kuuawa kwa wanasiasa nchini ni nadra, ingawa Juni 12, mwaka jana, chama cha ACt-Wazalendo kilidai kiongozi wake mkuu, Zitto Kabwe, alikuwa hajulikani alipo kwa zaidi ya saa 12 huku akiwa anasakwa na Jeshi la Polisi.
Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top