Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

CRISTIAN BELLA NDIO BASI TENA HUU NDIO UKWELI HALISI JUU YA AFYA YAKE KWA SASA..

Baada ya wiki iliyopita kusambaa picha mitandaoni za muimbaji Christian Bella zikimuonyesha akiwa amelazwa hospitali nchini Congo na kuzua hofu kwa mashabiki wa muziki wake, muimbaji huyo amefunguka kuzungumzia kitu ambacho kilimsibu.

Akiongea Ijumaa hii, Bella amesema alikimbizwa hospitali baada ya kuishiwa nguvu ghafla.

“Namshukuru Mungu anaendelea vizuri, nililazwa kwa muda mfupi kutokana na uchovu lakini baada ya kufanyiwa vipimo nilikutwa nimechoka tu. Kwahiyo baada ya kupumzika niliruhusiwa lakini niliambiwa natakiwa nitenge muda wa kumpumzika kwa sababu nilikuwa na tour ya muda mrefu kwa hiyo mwili ulikuwa umechoka sana,” alisema Bella.

Muimbaji huyo ambaye ni raia wa Congo, kwa sasa amerejea nchini Tanzania kwaajili ya kuendelea na shughuli zake za muziki baada ya kuwa na tour kubwa ya nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kati.

USIJIVUNIE MWILI:KIJANA WA MIAKA 21 AKIWA NDANI YA MWILI WA MZEE WA MIAKA 160 AFUNGUKA STORI NZITO YA MAISHA YAKE TAZAMA PICHA HIZI ZAIDI.

 Mshukuru Mungu kwa kila Kitu, Usijivunie Mwili wala Muonekano maana ni zawadi ambayo Ulipewa sio kweli kwamba huyu Dogo alipenda yeye, Au sisi ni Bora kuliko yeye machoni pa Mwenyezi Mungu.

1:Anakuwa mara nane zaidi ya Ukuaji wa Mwanadamu wa kaidia
2:Wazazi wake walitaka kumuuza kwenye maonyesho.

HABARI NZITO YA HIVI PUNDE:RIPOTI NZITO YA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU KULIPASUA TAIFA VIPANDE VIPANDE HAKUNA ALIETEGEMEA MAJIBU YA SAKATA HILI NYETI...

Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania ni nchi ya 4 barani Afrika kwa kuwa na vifo vya mama na mtoto huku ikiwa ya 6 duniani kwa vifo hivyo hivyo, suala ambalo wadau wa afya wanaishinikiza serikali kuwekeza katika huduma za dharura wakati wa kujifungua

Akiongea leo jijini Dar es salaam katika uwasilishwaji wa ripoti ya miradi ya afya katika mikoa ya Morogoro, Kigoma na Pwani Mkurugenzi wa shirika la Thamini Uhai Dkt. Nguke Mwakatundu amesema jitihada za makusudi za ujenzi wa huduma za dharura karibu na makazi ya watu hasa maeneo ya vijijini iongezwe ili kutatua changamoto hiyo.

“Nchi inayoongoza kwa vifo hivyo Afrika ni Nigeria, Democratic Republic of Congo, Ethiopia, Tanzania, na nje ya Bara la Afrika ni pamoja na India na Pakistan, kuna nchi nyingine zimeendelea lakini mila na desturi nayo nikikwazo kikubwa katika kuokoa maisha ya mama na mtoto” amesema

Dkt. Nguke amesema, wakati umefika kwa serikali kuhakikisha inatekeleza mipango mbalimbali iliyojiwekea katika kuhakikisha inapunguza vifo vya mama wakati wa kujifungua kutoka wanawake 332 kufikia idadi ya wastani ya wanawake 250 kama ilivyo ainisha katika mpango wa maendeleo wa Taifa ili kujiletea maendeleo.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Kinga ya Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia Wazee na Watoto Dr. Kaholeth Winani amesema, Asilimia 15 ya vifo vya mama na mtoto hutokana na matatizo yasiyo tabirika wakati wa uzazi hivyo ni jukumu la Jamii kutambua dalili za hatari na kuwawaisha kina mama kwenye vituo vya afya kwani asilimia 85 ya wajawazito hujifungua salama bila matatizo.

Jamaa Ampiga Daktari Risasi...Kisa Kaona Uchi wa Mke wake Alipokuwa Akijifungua

SAUDI ARABIA: Mwanamume mmoja akamatwa na Polisi kwa kumpiga risasi mwanaume mtaalamu wa afya ya uzazi aliyemsaidia mkewe kujifungua, akisema ni haramu kwa mwanamume kuona uchi wa mkewe.

Inasemekana kuwa mtuhumiwa alikasirishwa na wasimamizi wa hospitali waliomruhusu daktari Muhannad al Zabn kumsaidia mkewe kujifungua.

Dozi ya Ukimwi kutosubiri muda Hupewa papo hapo

South Africa makes headway on the AIDS epidemicKUANZIA Oktoba mwaka huu, watu watakaogundulika kuwa na virusi vinavosababisha Ukimwi, watapewa dawa ya kupunguza makali hapo hapo badala ya kusubiri kinga zao za mwili kupungua,anaandika Dany Tibason.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi imeitaka serikali kuongeza fedha katika kupambana na ugonjwa huo baada ya wahisani kupunguza misaada yao.
Costantine Kanyasu, mwenyekiti wa kamati hiyo akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho amesema,  wafadhili wengi wamepunguza misaada katika kuwahudumia wagonjwa hao hivyo serikali inatakiwa kuongeza fedha.
Amesema, utafiti unaonesha kuwa, walioambukizwa Virusi vya Ukimwi mpaka sasa ni watu milioni 2,400,000 lakini wanaopata dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo ni 700,000 pekee.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, serikali imesema itaongeza idadi ya utoaji wa dawa na kufikia wagonjwa milioni 1,1000,000 ifikapo Oktoba mwaka huu na kwamba, bado watu zaidi wa milioni 1.3 watakosa dawa.
“ Kamati imeomba serikali kuongeza fedha kutokana na wafadhili kujitoa au kupunguza misaada yao katika ugonjwa huu, vinginevyo itoe dawa bure kwa wale wanaohitajika kupata bure na iruhusu watu binafsi kuagiza nje na kuziuza kwa bei nafuu ili kufikia malengo,’’ amesema.
Awali, akizungumzia masuala ya chanjo kwa kamati hiyo Dk.Mpoki Ulusubisya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema, chanjo dhidi ya ugonjwa huo bado inahitajika.
Amesema, utafiti uliofanyika unaonesha kuwa, maambukizi  kwa wanawake ni makubwa kwa asilimia 6.25 ikilinganishwa na wanaume wenye  maambukizi asilimia 3.8.

Dalili 5 za kansa, ambazo watu wengi wanazipuuzia

Kugundua dalili za awali ni njia bora zaidi ya kutibu huu ugonjwa. Kuna baadhi ya dalili ambazo zinaonekana moja kwa moja, ingawa idadi kubwa ya wanaume na wanawake wanazipuuzia.
Hizi ni baadhi ya dalili za saratani:
1.Kupungukiwa na pumzi
Moja ya dalili ya kansa ya mapafu, ambapo wagonjwa wengi wanasema waligundua awali ni kubana kwa pumzi na kutoka kwa sauti fulani wakati wakivuta pumzi.Kwa kutogundua watu wengi wanafikiri kuwa wana asthma.

2.Kikohozi kisichoisha na maumivu ya kifua
Aina tofauti za saratani, ikiwa ni pamoja na leukemia na kansa ya mapafu, zinaweza kugundulika kwa kikohozi.
Tofauti ni kwamba hili tatizo linaweza kuwa la mda mrefu au kwa mda mfupi alafu linapotea.Kama una maumivu yasiyoisha au kikohozi kisichoisha, nenda kafanye uchunguzi.

3.Ugumu katika kumeza
Kupata ugumu kumeza ni moja ya dalili inayohusiana na kansa ya kizazi au ni dalili za awali za kansa ya mapafu.

4.Kupungua uzito
Kama ukigundua uzito wako umepungua bila ya kufanya diet au kubadilisha mfumo wako wa maisha,yakupasa kujiuliza kwanini.Kupungua uzito ni moja ya dalili ya colon cancer, ambayo inaathiri hamu ya kula na mwili kushindwa kutoa uchafu vizuri.

5.Kucha kubadilika rangi
Kubadilika kwa kucha ni moja ya dalili za aina tofauti za saratani. Mistari ya Brown au weusi au vidoa kwenye kucha, ni alama ya kansa.Kucha rangi ya Pale au nyeupe ni alama kwamba ini lako alifanyi kazi vizuri, na ni moja ya dalili ya saratani ya ini.
Ukiona mabadiliko yeyote yasiyo kawaida katika mwili wako,ni vyema ukaenda katika vituo vya afya ukafanyiwe uchunguzi

Katibu mkuu afya, aongoza kusomba meza Muhimbili kupata wodi ya wazazi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Dar es Salaam. Agizo la Rais John Magufuli la kubadili matumizi ya Jengo la Wizara ya Afya, Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto lililopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jana lilimfanya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulisubisya kushiriki kubeba samani kupisha uwekaji wa vitanda ili kuanza kuwa wodi ya wazazi.
Rais Magufuli alitoa agizo hilo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Wazee wa Dar es Salaam na kutoa siku mbili kwa maofisa 70 waliokuwa wakitumia jengo hilo kuhamishwa kuwapisha kinamama ambao wamesongamana katika jengo la wazazi lililopo.
Jana licha ya kuwa siku ya mapumziko, Dk Ulisubisya alifika Muhimbili mapema asubuhi na kushirikiana na madaktari, wauguzi na wafanyakazi wengine kuondoa samani za ofisi na kuziweka nje ya jengo hilo.
Hakusimamia kazi hiyo tu, bali alishiriki moja kwa moja kubeba meza, viti, kabati na kompyuta na kuvitoa kwenye ofisi hizo ili kupata nafasi ya kuweka vitanda vya wagonjwa kazi ambayo ilikuwa ikifanywa kwa kasi huku yeye na watumishi wengine wakipishana bila kupumzika kama wafanyavyo nyuki.
Kasi hiyo ilimfanya katibu mkuu huyo kutokwa na jasho kiasi cha shati alilovaa kuloa chapachapa.
Dk Ulisubisya alisema kazi hiyo ingekamilika jana jioni na kwamba shughuli ya uwekaji wa vitanda itaendelea leo.
Alisema kati ya vitanda 250 hadi 300 vitawekwa katika jengo hilo huku akisema maofisa waliokuwa hapo watatafutiwa ofisi wizarani huku taratibu nyingine zikiendelea.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MNH, Profesa Lawrence Mseru alisema, jana kusingekuwa na mgonjwa ambaye angelala chini: “Mbali na lile jengo ambalo alituagiza Rais, pia jengo letu la uzazi na mtoto tumepata sehemu ambayo tunaweza kuweka vitanda 50, kwa hiyo leo wagonjwa wote watalala kwenye vitanda.”
Alisema kulikuwa na wagonjwa 50 waliokuwa wakilala chini na kwamba tatizo hilo lingemalizwa jana. Profesa Mseru alisema wamefanya hivyo, kwa kuwa jengo hilo lina huduma muhimu kama vyoo na bafu za kutosha.
Alisema ili kupata nafasi hiyo, wamehamisha kliniki ya wajawazito na kuipeleka katika jengo la afya uzazi na mtoto.

SIKU 100 ZA JPM: Kasi ya Rais Magufuli Ilivyowaliza Waliojenga Mabondeni D’Salaam

Polisi wakisimamia kazi ya ubomoaji wa nyumba
Leo zimetimia siku 100, tangu Rais John Magufuli alipoingia katika Ikulu kuwatumikia wananchi, lakini baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Serikali yake zimewaachia vilio na majonzi baadhi ya wananchi, hasa wale walioathiriwa na uamuzi wa kubomoa nyumba zilizojengwa katika maeneo yasiyostahili kuishi binadamu kama vile mabondeni.
Majonzi hayo yalikuja baada ya Serikali ya Magufuli kutangaza kiama cha kubomoa nyumba zote zilizo ndani ya mita 60, kutoka kwenye kingo za mito na mabondeni, lengo likiwa ni kuondokana na majanga ya mafuriko yanayoweza kutokea.
Agizo hilo lilianza kutekelezwa Desemba mwaka jana, ikiwa ni mwezi mmoja na siku kadhaa tangu kuapishwa kwake na kuacha wakazi zaidi ya 200,000 wakiwa hawana makazi.
Operesheni ya kubomoa nyumba ilianzia maeneo ya Mwenge, Kinondoni na Temeke Jijini Dar es Salaam na baadaye iliendelea mikoa mingine, ikiwamo Arusha na Iringa huku ikisimamiwa na Baraza la Taifa la Uhifadhi Mazingira (NEMC), halmashauri na Jeshi la Polisi.
Wananchi ambao nyumba zao zilikumbana na kadhia ya ubomoaji, wanasema kuwa siku 00 za Rais Magufuli madarakani, hazijawasaidia lolote zaidi zimewaongezea hali ngumu ya maisha huku wakijutia kumchagua.
“Kiukweli siku 100 za Magufuli nimeziweka kwenye rekodi yangu, zimenifanya maisha yangu kuwa tofauti, kwani nalala nje kitu ambacho nilikuwa ninakisikia tu kwenye vyombo vya habari,” anasema Erasto Majani mkazi wa bonde la Mkwajuni.
Wanasema wamekuwa ombaomba kwa kukosa makazi, wengine wamebadilisha mtindo wa maisha yao kwa kulala juu ya vifusi, wamepoteza ndugu na jamaa zao kwa mstuko wa kubomolewa nyumba zao.
“Haya ni maisha mapya aliyotuletea Magufuli, mpaka najuta kwa nini nilimchagua, nilijua atakuwa mtetezi wa wanyonge kama alivyokuwa anatuahidi kwenye kampeni zake, lakini ametugeuka ,” anasema Isabela Philipo, mkazi wa Hananasifu.
Wananchi hao wanasema uwepo wa Magufuli kumewafanya wamkumbuke Rais mstaafu Jakaya Kikwete, kwani alikuwa na huruma na wananchi wake.
“Magufuli amenifanya nimkumbuke Kikwete pamoja na mapungufu aliyokuwa nayo, lakini alikuwa na roho ya utu, hakutaka kabisa tuvunjiwe nyumba zetu,” alisema Ally Gambo.

Operesheni ilivyokuwa
Operesheni ya bomoabomoa iliendeshwa kwa awamu mbili, ya kwanza ilihusisha wakazi wa Mwenge, Pugu Mnadani na Temeke na nyumba zaidi ya 700 zilibomolewa.
Awamu ya pili ilihusisha ubomoaji wa nyumba za bonde la Msimbazi maeneo ya Kigogo, bonde la Mkwajuni, kata ya Hananasifu Manispaa ya Kinondoni.
Awamu hii ilihusisha ubomoaji wa nyumba zaidi ya 8,000 huku ikiacha vilio simanzi na majonzi kwa wakazi wa maeneo hayo, watu wakipoteza maisha na wengine kupata maradhi ya kupooza.

Bomoabomoa yasitishwa
Kutokana na kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali , Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na NEMC ilisimamisha shughuli ya ubomoaji kwa muda wa siku 14 ili kuwapa nafasi ya kuhamisha mali zao wenye nyumba zilizotakiwa kubomolewa huku ikiwataka wananchi hao kubomoa wenyewe nyumba zao.
“Kama unafahamu umejenga nyumba yako eneo ambalo halitakiwi kisheria, tafadhali vunja mwenyewe kwa kuwa bomoabomoa itarudi kwa nguvu,” alisema Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
Aliongeza: ”Ukibomoa mwenyewe utaondoka salama na vyombo vyako, milango, madirisha hata matofali lakini ukisubiri , vyote hivyo vitaharibiwa.’’
Januari 5 shughuli ya ubomoaji iliendelea maeneo ya Bonde la Msimbazi, Mlalakua, Mbezi Beach na Kawe.

Bomoabomoa yapingwa
Wakati NEMC ikianza tena kazi ya kubomoa nyumba zilizoko katika maeneo hatarishi kwa makazi ya binadamu baada ya kusimamishwa kwa muda wa siku 14, Mahakama Kuu ilizuia kuendelea kwa zoezi hilo baada ya wakazi 674 waliovunjiwa nyumba zao kufungua kesi kupinga ubomoaji .
Aidha, aliyekuwa Meneja Kampeni wa Magufuli, Abdallah Bulembo, alipinga ubomoaji wa nyumba hizo akidai kuwa utamjengea chuki Rais kwa wananchi .
“NEMC wasiwe kama wameshuka kutoka mbinguni..., wasituharibie imani ya wananchi kwa Rais... kwani walikuwa wapi siku zote mpaka wasubiri Rais Magufuli kuingia madarakani? Sikubaliani na bomoabomoa hiyo,” alisema.

Mabomu yarindima
Baadhi ya vijana na wananchi ambao nyumba zao zilibomolewa walifunga barabara na kuchoma mataili kupinga uwekaji alama ya X kwenye nyumba zilizoko mabondeni.
Vurugu hizo zilisababisha askari kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wamefunga barabara.
Tangu ubomoaji usitishwe na mahakama, hali imetulia kidogo, wananchi wanaendelea na maisha yao mabondeni na bado hawataki kuhama pamoja na kuwa baadhi nyumba zao tayari zimeshabomolewa, waliosalia wanasubiri hatima ya kesi yao.

HIKI NDIYO CHANZO CHA KIJANA HUYU KUJIKATA ULIMI

KATIKA hali isiyo ya kawaida raia mmoja wa India alijikata ulimi wake ili kukidhi matakwa ya kuonana na Mungu wa imani yake.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni lilipelekea raia huyo kutokwa na damu nyingi ambazo zilimfanya awaishwe hospitalini kwa ajili ya kuongezewa damu

Njia Rahisi Za Kukupa Hamasa Ya Mafanikio Wakati Mipango Yako Inapokwenda Vibaya

Kuna wakati ambapo katika safari yetu ya mafanikio, mambo huwa hayaendi sawa kama tulivyopanga. Ni kipindi ambacho kinakuwa kigumu kwa wengi na kupelekea hata hali ya kukata tamaa kuingia ndani mwetu. Natambua umeshawi kukutana na hali kama hii wakati fulani kwenye maisha yako.

Je, mipango na malengo yako ilipokwenda hovyo ni kipi ulichokuwa ukikiwaza? Ilifika mahali ulikata tamaa au ulifanyaje? Kitu kikubwa cha kuelewa hapa, mambo yako yanapokwenda hovyo isiwe sababu ya kukata tamaa, dawa ni kusonga mbele. Na utaweza kusonga mbele ikiwa utakuwa na hamasa kubwa ya kufanikiwa. Na hamasa hiyo utaipataje?

Zifuatazo Ni Njia Rahisi Za Kukupa Hamasa Ya Mafanikio Wakati Mipango Yako Inapokwenda Vibaya.

1. Tambua upo kwenye kipindi ambacho utakipita.
Pamoja na kwamba unaweza ukawa unaona mipango yako imeenda vibaya kuliko kawaida, lakini tambua upo kwenye kipindi cha mpito. Hautaweza kukaa katika hali mbaya uliyopo siku zote. Ni lazima utavuka, hivyo kama ulikuwa umeanza kukata tamaa nyanyuka ulipo kwani ushindi upo mbele yako unakusubiri.

2. Kuwa na watu chanya.
Mipango yako unapojikuta imeenda hovyo kinyume na ulivyotarajia, njia bora nyingine ya wewe kuweza kujihamasisha na kusonga mbele ni kuwa karibu na watu chanya. Hawa ni watu watakaokusaidia kukupa hamasa na hamu ya kuendelea mbele. Pia watakusaidia kukufariji na kukunyanyua zaidi pale ulipo kwama.

3. Panga malengo yako tena upya.
Najua kama umekwama sehemu, ni rahisi sana ‘kupaniki’ na kuona kila kitu basi hakiwezekani tena. Lakini ukweli wa mambo ulivyo inapotokea mambo yako yanapokwama, tuliza akili na weka mipango yako upya. Kushindwa kwako mara moja kusikufanye ukashindwa kupanga malengo mengine. Panga mambo upya ya kukufanikisha tena.

4. Ondoa hofu zote ulizonazo.
Haina haja ya kubeba wasiwasi mwingi ndani yako eti kwa sababu umeshindwa mara moja.  Vaa moyo wa ujasiri na kuamua kwamba ni lazima usonge mbele hata iweje. Kama kupanga malengo yako yapange tena. Kushindwa kwako mara moja haimaanishi kwamba huo ndio mwisho wa mafanikio yako tena. Unayo nafasi ya kujaribu na kufanikiwa. Usiruhsu kabisa hofu ikawa kikwazo kwako.

Ukiamua unaweza kufikia mafanikio yako makubwa bila ubishi.

Virusi vya Zika vyapatikana katika mate na mikojo

Image copyrightEdmar Melo JC Picture
Image captionMtoto aliyeathirika ka virusi vya Zika
Virusi hai vya Zika vyapatikana katika mate na mikojo ya wagonjwa,wanasayansi wa Brazil wamesema.
Matokeo hayo hayamaanishi kwamba ugonjwa huo unaweza kusambazwa kupitia maji maji hayo ya mwilini.Sababu kuu ya kuenea kwa virusi hivyo ni kupitia kuumwa na mbu,lakini wanasayansi wanachunguza njia nyengine.
Huku maambukizi ya Zika yakiwa sio makali,ugonjwa huo umehusishwa na maelfu ya watoto waliozaliwa na kasoro.
Image copyrightEPA
Image captionHarakati za kukabiliana na Zika
Virusi vya Zika pia vimepatikana katika majimaji mengine ya mwilini katika mripuko mwengine uliotokea eneo la Polynesia,lakini mamlaka ya Brazil inasema kuwa hii ni mara ya kwanza virusi hai vya Zika kupatikana.
Paula Gadelha,mkuu wa taasisi ya Fiocruz ambayo inashirikiana na wizara ya Afya amesema:''Virusi hivyo vya Zika vimepatikana katika Mate na mikojo''.
Image copyrightAP
Image captionWanasaynsi wa Brazil
''Lakini hiyo hainamishi kwamba kuna uwezekano wa kuenea kwa virusi hivyo kupitia mate na mikojo.Hatari ya kuenezwa kwa virusi hivyo kupitia maji maji ya mwilini uliangaziwa nchini Marekani ambapo kituo cha udhibiti wa magonjwa kinaamini kisa kimoja kilisambazwa kupitia ngono''.
Hatahivyo kumekuwa na kesi mbili pekee za usambazaji wa virusi hivyo kupitia ngono.

BREAKING NEWS:...JUMA NKAMIA AMUUMBUA KIGWANGALLA BUNGENI KUHUSU MASHINE YA CT-SCAN ILIYONUNULIWA KUMBE HAIJANUNULIWA ILA IMETOLEWA KATIKA HOSPITALI HII..

Mashine  mpya ya CT-Scan iliyodaiwa kuwa imenunuliwa na serikali na kufungwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ilitolewa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, iliyoko katika Chuo Kikuu cha Dodoma, imeelezwa.

Hayo yalibainika jana baada ya Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia, kueleza wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini hapa.

Katika swali lake la nyongeza, Nkamia aliitaka serikali ikiri kuwa  mashine hiyo ambayo inatumika Muhimbili ni ile ambayo  imechukuliwa katika hospitali hiyo, badala ya kudai kuwa imenunuliwa mpya.

Kutokana na kubanwa huko, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla, alikiri kuwa mashine ilitoka katika hospitali hiyo.

Hata hivyo, alisema si kweli kwamba iling’olewa baada ya kuwa imefungwa bali ilikuwa kwenye mchakato wa kufungwa.
“Ni kweli mashine hiyo ilikuwa ifungwe Dodoma katika hospitali ya Benjamin Mkapa lakini majengo yalikuwa hayajakamilika hivyo serikali ikaamua ipelekwe Muhimbili,” alisema.

Dk. Kigwangalla alisema serikali iko katika mchakato wa kununua mashine mpya kwa ajili ya kufunga hospitali ya Benjamini Mkapa na majengo ya kufunga mashine hiyo kwa sasa yanaelekea kukamilika.

Katika swali la msingi, Nkamia alihoji mpango wa serikali wa kununua mashine mpya ya CT-Scan kwa ajili ya hospitali ya Muhimbili.
Akijibu swali la msingi, Dk. Kigwangalla alisema serikali imefuatilia mwenendo wa huduma ya vipimo vya radiolojia inayotolewa  Muhimbili na kubaini ina upungufu.

Alieleza upungufu huo ni kuharibika mara kwa mara kwa CT-Scan na kusababisha usumbufu kwa baadhi ya wagonjwa kutopata huduma ya kipimo hicho kwa wakati.

INASIKITISHA:..MWANAUME AOTA MIZIZI MWILINI MWAKE, SERIKALI YATOLEA KUMHUDUMIA...PICHA ZINATISHA

Abdul BajandarImage copyrightAFP
Image captionFamilia ya Abdul Bajandar ilishindwa kugharimia matibabu yake
Serikali ya Bangladesh imesema itagharimia upasuaji wa kumtibu mwanamume ambaye anaugua ugonjwa unaofanya mtu kupata dutu zinazofanana na mizizi ya mti mwilini.
Waziri wa afya wa Bangladesh Mohammad Nasim alitangaza hilo baada ya kumtembelea Abul Bajandar, hospitalini Alhamisi.
Bw Bajandar anaugua ugonjwa ambao kisayansi unajulikana kama epidermodysplasia verruciformi.
Ni ugonjwa wa kinasaba ambao humfanya mtu kuota vidutu kwenye ngozi. Hujulikana sana kama “ugonjwa wa binadamu mti”.
Alianza kuota vidutu miaka 10 iliyopita.
“Awali, nilidhani hazina madhara,” Bw Bajandar ameambia AFP.
Image copyrightAFP
"Sasa zimeongezeka na nyingine zina urefu wa inchi mbili hadi tatu katika mikono yangu miwili. Kuna nyingine miguuni,” amesema.
Bw Bajandar alisafiri India kutafuta matibabu lakini familia yake haingemudu gharama.
Sampuli za damu yake na ngozi zitapelekwa kwenye maabara moja Marekani kuchunguzwa zaidi, profesa Abdul Kalam, ambaye ni mtaalamu wa upasuaji wa ngozi ameambia BBC.
Atatibiwa nchini Bangladesh baada ya matokeo ya uchunguzi kutolewa.
Bw Bajandar ni mmoja wa watu watatu wanaougua “ugonjwa wa binadamu mti” duniani, mkurugenzi wa hospitali ya chuo cha Dhaka, Samanta Lal Sen ameambia AFP.
Ni mara ya kwanza kwetu kupata kisa kama hicho hapa Bangladesh.

Kisa nadra cha Zika charipotiwa Marekani

ZikaImage copyrightReuters
Image captionMgonjwa aliyeambukizwa hakuwa amesafiri nje ya Marekani
Kisa nadra sana cha virusi vya Zika kuambukizwa kupitia kushiriki ngono, badala ya kuumwa na mbu, kimeripotiwa nchini Marekani.
Mgonjwa aliyeambukizwa virusi hivyo Dallas, Texas, sana huenda aliambukizwa kupitia kufanya mapenzi, Kituo cha Udhibiti wa Maradhi (CDC) kimeambia BBC.
Mtu huyo hakuwa amesafiri maeneo ambayo yana virusi hivyo lakini mpenzi wake alirejea majuzi kutoka Venezuela.
Virusi vya Zika vinaenezwa sana na mbu na vimehusishwa na visa vya watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo na ubongo kudumaa.
Vinaenea kwa kazi Amerika na Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza hali ya tahadhari duniani.
ZikaImage copyrightGetty
Image captionVirusi vya Zika vinaaminika kuwafanya watoto wazaliwe na vichwa vidogo
Shirika la msalaba mwekundu nchini Marekani limewahimisha watu waliotoka maeneo yaliyoathirika na Zika, na ambao wanataka kutoa damu, wasubiri angalau siku 28, kabla ya kutoa damu.
Ushauri huu umeelekezwa kwa watu waliorejea Marekani kutoka Mexico, visiwa vya Caribbean au Amerika ya Kati na Kusini katika kipindi cha wiki nne zilizopita, shirika hilo limesema kupitia taarifa.
Katika tukio jingine, visa viwili vya maambukizi ya Zika vimethibitishwa Australia.
Maafisa wanasema wakazi wawili wa Sydey waliopatikana na virusi hivyo walirejea kutoka Caribbean majuzi.
Kisa hicho cha maambukizi ya Zika Dllas, kitakuwa ndicho cha kwanza kuthibitishwa kutokea Marekani bara, ingawa jimbo la Texas limeripoti visa vingine ssaba, vyote kwenye watu waliorejea kutoka nje.
Anne Schuchat, naibu mkurugenzi mkuu wa CDC amesema hicho ndicho kisa cha kwanza kinachohusisha mtu ambaye hakusafiri.
"Hatudhani aliambukizwa baada ya kuumwa na mbu, lakini tunaamini aliambukizwa kupitia kushiriki ngono.”
Taarifa ya CDC imesema njia bora zaidi ya kujikinga na “kujikinga usiumwe na mbu na kutokumbana na manii kutoka kwa mtu aliyekumbana na virusi vya Zika”.
Kisa hicho hata hivyo sicho cha kwanza kabisa cha maambukizi kupitia ngono kuripotiwa.
Shirika la CDC linasema kwenye tovuti yake kwamba mwaka 2013 kulilipotiwa kisa cha maambukizi kupitia kushiriki mapenzi katika jimbo la French Polynesia.
Shirika hilo linawashauri wanawake wajawazito kutosafiri mataifa mengi yaliyoathiriwa sana na virusi hivyo.

Askofu Pengo kutoka hospitali leo



Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amesema afya ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo imeimarika na leo ataruhusiwa.
Kardinali Pengo alifikishwa katika hospitali hiyo Desemba 31, mwaka jana kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Profesa Janabi alisema Pengo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo. Hata hivyo, hakueleza kwa undani.
Jana, kwa mara ya kwanza tangu afikishwe katika hospitali hiyo, Pengo alijitokeza hadharani na kuzungumza na wafanyakazi wa taasisi hiyo na waandishi wa habari, huku akishukuru kwa huduma alizopata.
Alisema amepatiwa huduma nzuri na kumfanya afute kichwani mwake habari za watu mbalimbali wanaodai kuwa MNH haiwahudumii vizuri wagonjwa.
“Nataka niwashukuru wahudumu wote walionifikisha katika hali hii, hasa Profesa Janabi na Mkuu wa Kitengo cha Dharura na Ajali, Dk Juma Mfinanga,” alisema.
Akiwa hospitalini hapo jana, Kardinali Pengo alitembelewa na maaskofu wasaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe na Eusebius Nzigilwa pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea, Damian Dallu.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu alisema Serikali imejipanga kuhakikisha wagonjwa wa moyo hawapelekwi nje ya nchi kutibiwa.
Alisema tangu kuanza kwa mpango wa kuwatibu wagonjwa hao nchini Taifa limeokoa takribani Sh5 bilioni.
“Tutatoa vibali kwa wagonjwa kutibiwa nje ya nchi ikiwa itathibitishwa na madaktari kuwa huduma husika haiwezi kutolewa nchini,” alisema. Jana, Profesa Janabi alisema waliwahudumia wagonjwa 500 na mwaka huu wanatarajia kupokea kundi la madaktari bingwa kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutoa mafunzo.

Waziri Mkuu Atoa ONYO Kali Kwa Madaktari Wanaotoa Mimba Wanawake.....Aapa Kuwafukuza Kazi Na Kuwafunga Jela

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Josephine John  ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu. Alikuwa katika ziara ya mkoa huo Januari5, 2016.

********

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya Madaktari vinara wa Hospitali ya Rufaa ya Songea ambao wanasifika kwa kufanya biashara ya kutoa mimba wanawake na wanafunzi kuacha tabia mara moja,lasivyo  atawafukuza kazi na kuwafunga jela.

Waziri Mkuu alitoa onyo hilo jana wakati alipotembelea Hospitali hiyo na kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuwasisitiza kutoa huduma bora kwa wagonjwa,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 mkoani Ruvuma.
Alisema Hospitali ya mkoa huo inasifika kwa kutoa mimba wanawake na kuwalaza wagonjwa wao wodi namba 5, kitendo ambacho serikali haikuruhusu wala haikubaliani nacho.
"Naomba mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktati hao wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo," alisisitiza majaliwa.
Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo,Dr. Daniel Malekela na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dr. Phils Nyimbi kuwafuatilia madaktari wanaojihusisha na vitendo hivyo na kutoa taarifa ili wachukuliwe hatua kali.
Pia, alimuagiza mganga mkuu Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lililo jirani na hospitali hiyo ili kuondo hisia kwamba dawa zinaibiwa na kupelekwa kwenye maduka ya watumishi.
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Thabiti Mwabungu na kulia ni Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na bibi Antonia Moyo ambaye alikuwa akipata matibabu katika chumba maalum cha waze katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma wakati alipoitembelea hositali hiyo akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Thabiti Mwabungu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akimsalimia mtoto Flora Mapunda (1) ambaye amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambayo  Waziri Mkuu aliitembelea na  kuzungumza na watumishi  akiwa ktika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.

HABARI YA HIVI PUNDE:..TAARIFA MUHIMU HATIMAYE DAWA YA UKIMWI YAPATIKANA HUKO HISPANIA, NCHI YAFURIKA MAMILIONI YA WATU KILA KONA KUFUATA HIYO DAWA NA WANAZIDI KUMIMINIKA BAADA YA KUTANGAZA DAWA HIYO..WANANCHI MNAOMBWA MTULIE KWANI DAWA HIZI ZITALETWA NCHINI KWETU



Vidonge vya kufifisha virusi vya Ukimwi.
Dar es Salaam. Wakati dunia ikiwa na zaidi ya watu 34 milioni wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), madaktari nchini Hispania wametangaza kugundua tiba ya ugonjwa huo wanayodai ni uhakika.
Kwa kutumia damu ya kupandikiza kutoka kwenye kitovu mwana (umbilical cord) cha mtu ambaye ana vinasaba ambavyo havipokei virusi hivyo vya Ukimwi, wataalamu hao wa tiba wa Hispania wanaamini kuwa wanaweza kutibu ugonjwa huo baada ya mafanikio waliyopata kwa mgonjwa mmoja.
Madaktari hao wa Kitengo cha Taifa cha Upandikizaji (ONT) cha Hispania walichukua damu ya vitovu mwana vya watu wenye vinasaba ambavyo havipokei VVU na kuipandikiza kwa mtu anayeishi na virusi hivyo. Baada ya miezi mitatu, mgonjwa huyo alipimwa na kuonekana hana virusi.
Daktari wa Programu ya Upandikizaji kutoka Taasisi ya Tiba ya Catalan, Barcelona, Rafael Duarte alisema mgonjwa aliyetibiwa kwa njia hiyo, Timothy Brown (37), alikuwa anaishi na VVU tangu mwaka 2009 na madaktari hao walithibitisha kuwa amepona baada ya kupandikizwa damu hiyo. Mgonjwa mwingine aliyefanyiwa majaribio ya tiba hiyo alipona VVU, lakini miaka mitatu baadaye alifariki kwa ugonjwa wa saratani.
Timu ya madaktari wa Hispania ililiambia gazeti la kila siku nchini humo la El Mundo kuwa wana uhakika kuwa wameleta mapinduzi katika mapambano ya Ukimwi na magonjwa yanayofanana na hayo.
Dk Duarte alisema mwaka 2015 umekuwa wa kujivunia ugunduzi huo mkubwa duniani, ingawa alitahadharisha kuwa tiba kamili haiwezi kupatikana katika siku za usoni.
Kaimu mkurugenzi wa mwitikio wa Taifa wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Dk Morris Lekule alisema utafiti kama huo hauna budi kufuata taratibu zote na kuthibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kabla ya kutangazwa kuwa ni tiba sahihi.
“Kila mara taarifa zinakuja zikisema tiba ya Ukimwi imepatikana, lakini tiba kupata uthibitisho kwamba ni sahihi, ni mchakato mrefu unaotakiwa kuhakikisha kama kweli dawa hiyo inatibu na ni lazima WHO wathibitishe hilo,” alisema. Alisema ni vizuri kama wataalamu hao wakapata uhakika kutoka WHO badala ya kuwapa watu matumaini kuwa kuna tiba na baadaye matumaini hayo yanapotea.
Daktari wa kitengo kinachoshughulika na masuala ya Ukimwi cha WHO, Richard Banda alisema hana taarifa za tiba hiyo.
Tiba inavyofanya kazi
Madaktari wa ONT walitumia damu ya mtu mwenye vinasaba vya ‘CCR5Delta’ ambavyo seli zake haziathiriwi na virusi hivyo vya Ukimwi.
Dk Duarte alisema kwanza huziua seli za damu ya mgonjwa kwa kutumia mionzi halafu seli mpya (kutoka kwenye damu ya mtu mwenye seli zisizoathiriwa na VVU hupandikizwa.
Damu hiyo ilipandikizwa kwa mgonjwa mwenye virusi hivyo na saratani ya damu.
Baada ya seli hizo kupandikizwa, Virusi vya Ukimwi vilivyo kwenye damu ya mgonjwa hushindwa kujipenyeza katika seli mpya zilizopandikizwa. “Siku 11 baada ya upandikizaji, mgonjwa wa Barcelona alianza kupata nafuu na baada ya miezi mitatu, tulimpima na kukuta hana VVU,” alisema.

CHANZO: MWANANCHI

HOT NEWS:.GET YOUR APP NOW..PHARMABITS:a Special Web Based Application For Pharmacy:




PHARMABITS:a special Web Based Application for Pharmacy:

Does the following:

1. Sales
2. Store (Stock management)
3. Report Printing (Dynamic stock & Original stock)

Features:

1. Expire List
2. Danger Zone Products
3. Sales Statistics
4. Administrator Panel (Monitor Sales and Stock)
5. Add list of suppliers and customers for further reference

Users:

1. Teller
2. Store Keeper
3. Administrator

PHARMABITS application has been developed by the SkyBits Technology team of developers to help owners and workers of the Pharmacy to keep and track sales, stock, and report printing (Dynamic stock & Original Stock).

The application can give you the notification of the list of products that are nearly to expire that gives an assurance to the safe products and unsafe products for health purposes. It can also give the notification of the Danger Zone products (Products that are under quantity according to owners preference amount in stock).

The PharmaBits application has the ability to specify the most out going products (Sales Statistics).

Together with the admin panel, the owner or the administrator can keep monitoring of the  sales and stock that helps in avoiding loss. 

The PharmaBits application also allows the owner or admin to add the list of suppliers and customers for further reference. Using this method, it is easy to track the suppliers that supplied you with defects products. 

The PharmaBits application has been sold to several Pharmacies like the Crown Pharmacy and has been praised for its quality.

We will be glad if you would like to speak with us personally.

Stop using old ways (pen, paper and calculator) to record your important data, use PHARMABITS.

Contact: 

BENARD NYABENDA 
SkyBits C.T.O
0719260701
Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top