Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KIMENUKAA..Chadema Wamtolea Wema Tamko! Wafuasi Wadai Anawasaliti..!!!



Baada ya staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu kuvaa nguo zenye rangi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) alipotinga mahakamani hivi karibuni angali ni mwanachama damu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kisha baadhi ya wafuasi kudai anawasaliti, uongozi wa chama hicho umemtolea tamko.

ILIKOANZIA

Wema hivi karibuni akiwa ameongozana na mama yake, Miriam Sepetu na mashosti zake wengine, alitinga kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kwenye ile kesi yake ya ‘unga’ akiwa amevaa gauni refu la njano, juu akiwa amevaa ‘koti laini’ lenye rangi ya kijani na wekundu kwa mbali, hali iliyoibua mjadala kwa wafuasi wa Chadema waliokuwa mahakamani hapo.

“Huyu mbona leo katuvalia nguo hizi? Hizi si rangi za CCM kabisa? Mh! Kwa hili siyo sawa kabisa,” alisikika akisema mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa magwanda ya Chadema.

Mwingine akadakia: “Ni kweli rangi siyo ishu lakini kwa yeye ambaye juzijuzi alitangaza kuwa sasa ni Chadema damu, mavazi ya rangi hizi angeyachukia, sasa ona, utadhani ni kada wa CCM bwana.”

Kutokana na suala hilo kuibua maswali mengi kwa baadhi ya wanachama wa Chadema waliokuwa mahakamani hapo, Risasi Jumamosi liliwatafuta baadhi ya viongozi wa Chadema na kuwauliza kuhusiana na suala hilo ambapo kila mmoja alitoa tamko lake.

Meya wa Ubungo ambaye ndiye mlezi mkuu wa Wema Sepetu, Boniphace Jacob alisema; “Chadema siyo nguo, ni imani na itikadi kwani mahakamani lazima avae sare za Chadema? Hizo ni nguo tu kamanda, siyo ‘big deal’ sana.” Kwa upande wa msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene alieleza; “Hivi wale mashabiki au wanachama wa Simba wakivaa nguo za njano au kijani kwa sababu yoyote ile huwa ni ‘puppets’ (vibaraka) wa Yanga? Nadhani majibu hayo yamejitosheleza.”

BREAKING NEWS: HATIMAE MH KINANA ATOKA MAFICHONI ATOA KAULI HII NZITO KWA WANACCM WOTE..

Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa Katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahman Kinana alikuwa akiugulia afya yake pindi yupo kazini hivyo alichukua muda wa kutosha kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu.

Polepole amezungumza na AZAM NEWS ambapo alisema tangu Mzee Kinana akiwa hata kwenye mkutano mkuu wa CCM Dodoma hakuwa sawa kiafya.

“Tangu akiwa kwenye mkutano mkuu maalumu wa CCM Dodoma hakuwa sawa kiafya, alikuwa anafanya yote haya akiugulia afya yake kwahiyo ikakubalika achukue muda wakutosha wa kuitizama afya yake nje ya nchi na anapo rejea mgonjwa akitoka hospitali huwa hakimbii kazini, shambani moja kwa moja inashauriwa kitaalam atumie muda wa kupumzika ili kuimarisha afya yake na nimezungumza nae anaendelea vizuri yuko madhubuti kabisa kuliko jana,” alisema Polepole.

Katibu mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana hajaonekana hadharani kwa muda tangu Rais Magufuli aliposema kuwa yuko India.

HABARI NZITO NCHINI: YULE WAZIRI MWENYE UMRI MDOGO ZAIDI AUWA KIKATILI AKINGIA IKULU HIVI PUNDE




Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu. 
Abas Abdullahi Sheikh Siraji aliyekuwa na miaka 31 ameuawa karibia na ikulu ya Rais. 

Abas Abdullahi Sheikh Siraji hakuwa waziri wa kawaida nchini Somalia. 
Alipata umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge na kuiwakilisha Jubbaland. 

Amewahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo nchi jirani ya Kenya akiwa mtoto na kisha kurejea nchini mwake mwaka jana alipokwenda kwa ajili ya uchaguzi mkuu. 

Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi huku watu wengi wakimtaja kama mtu machachari sana miongoni mwa mawaziri. 

Saa chache kabla ya kuuawa kwake alizindua mradi wa ujenzi wa jengo kwa ajili ya watumishi wa umma. 

Waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo wamekamatwa.

BREAKING NEWS:HAKUNA ALIEAMINI HILI HIV NDIVYO RAIS MAGUFULI ALIVYOINGIZWA CHAKA SAKATA LA VYETI..

Mhadhiri huyo maarufu na mkereketwa wa chama cha kijani ameyazungumza haya maneno akiwa anahojiwa na kipindi cha mizani ya week Azam two television .Aliongeza na kwenda mbali zaidi kwa kushauri kungekua na utaratibu mwingine wa kulishugulikia suala la kughushi vyeti aidha kwa kupewa muda wakutimiza sifa zinazohijika au vinginevyo na sio adhabu kali waliyopewa.

Akiwa anazungumza kwa mifano na masikitiko alinukuliwa kuwa kuna daktari mmoja anayemfahamu alisoma clinical officer kwa kughushi cheti cha form four lakini ni daktari mbobezi tu ameokoa na anatibu watu wengi tu ila yumo kwenye list ,tutafute njia au namna nyingine ya kuwapima watu ,mtu kama dereva unahitajia nini elimu ya form four?ikiwa kusoma na kuandika na kuzielewa alama za barabani anaweza"?alihoji

"Alienda mbali zaidi na kusema unaweza ukakuta hawa baadhi ya watumishi walioghushi kwenye appraisal za kila mwaka kwa mujibu wa taratibu za serikali walikua wanapata daraja la kwanza"
Hakusita kutoa la moyoni kuwa hakubaliani kuwa suala walilolifanya ni jinai ,pia alilaumu kwanini uhakiki uishie kwa watumishi wa kawaida tu bila wakuu wa wilaya ,mikoa,wabunge na madiwani

Hakusita pia kui kosoa report ya ukaguzi wa vyeti kwa kuuliza idadi ya watu 1500 ambao vyeti vyao vinafanana ,ufanano wake upo kwenye credits,majina au shule na vyuo?hii report haijakaa sawa alikazia"

Mwisho kabisa aliishauri serikali ifanyie reform utumishi wa umma

BREAKING NEWZ LOWASSA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU JINA LA MWANAYE KUWA KWENYE LIST YA VYETI FEKI

habari inayo Gonga vichwa vya watu ni kuhusu vyeti feki kubwa zaidi ni Pale Jina la mtoto wa Lowassa kuwemo kwenye List ya wenye vyeti feki kiendo ambacho kime Mfedhehesha sana Lowassa na kusema kuwa Hata lifumbia macho hili swala la Mwanaye kuwekwa kwenye List ya vyeti feki
Lowassa Nitalitolea Ufafanuzi Jina la Godfrey Ngoyai Lowassa lililopo kwenye list ya watu wenye vyeti feki Muda sio Mrefu

BREAKING NEWS: HAIKUWAHAI KUTEGEMEWA RAIS MAGUFULI ATOA MSAMAHA KWA MH MBOWE HADHARINI NIZ ZIDI YA ISHU HII NYETI MNO...

Rais John Magufuli  amewaambia wakazi wa mji wa Bomang’ombe katika Jimbo la Hai kuwa amewasamehe.

Alitoa kauli hiyo akiwa katika jimbo hilo la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe baada ya kuwaona baadhi ya wananchi wakiwa wameshika jani la “Sale” ambalo hutumiwa na wenyeji kuomba msamaha.

Jani hilo linaloheshimiwa sana na wachaga wa mkoa huo, ndilo ambalo mtu akimpelekea mtu aliyemkosea na kumuomba yaishe, anayeombwa kupitia jani hilo hana jinsi lazima akubali.

“Nawashukuru sana wote mliokuja na haya majani ya mti. Nafahamu maana yake na mimi nimewasamehe wote. Najua na ninyi mmenisamehe wote,”amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa.

Ingawa Rais Magufuli hakuweka bayana walichomkosea, lakini katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, Rais Magufuli alipata kura 29,341 wakati mpinzani wake wa karibu, Edward Lowassa akipata kura 49,125.

“Tushikamane kwa pamoja tujenge nchi yetu. Hakuna Mtanzania anayekula vyama, Mtanzania anataka maendeleo, anataka hospitali, barabara, anataka madawa, maji yapatikane umeme,”alisema Rais.

“Hii ndio maana niko hapa kwa ajili yenu, naomba mniamini na Serikali yangu tuko kwa ajili ya kuijenga Hai na Tanzania kwa ujumla. Aika mae, Aikambe (Asanteni sana),”alisisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwashukuru wakazi wa Jimbo hilo kwa kura alizosema ni nyingi na ambazo zilimuwezesha kuwa Rais na akawaahidi kuwa atawaletea maendeleo bila kujali vyama.

“Ninawashukuru sana nataka niwaahidi mimi nitawafanyia kazi Watanzania wote bila kujali vyama vyao, bila kujali makabila yao, bila kujali dini zao bila kujali hata sura zao,” alisema

HABARI NZITO: HII NDIO JEURI NA KIBRI YA PAUL MAKONDA ATUMA SALAMU NZITO KWA WABAYA WAKE.

AMEPONYOKA! Matumaini ya baadhi ya watu kuwa arobaini ya sakata la kigogo anayedaiwa kutumia cheti cha mtu mwingine kuwa imewadia, yameyeyuka.

Matumaini hayo yalitoweka baada ya kigogo huyo anayedaiwa kujiendeleza kielimu kwa jina la mtu mwingine na kuachana na matokeo mabovu ya kitaaluma yatokanayo na jina lake halisi la Bashite kutoguswa katika ripoti ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma.

Aidha, maswali mapya yanayodaiwa kuibuka sasa kuhusiana na hatima ya sakata la Bashite ni pamoja na nia ya baadhi ya kutaka kujua suala hilo litashughulikiwa vipi kwa sasa baada ya ripoti iliyowasilishwa jana kwa Rais John Magufuli kutotoa majibu.

Hivi karibuni, sakata la Bashite lilitikisa katika vyombo mbalimbali vya habari hadi kutungiwa nyimbo. Baadhi ya wabunge katika vikao vya Bunge la Bajeti vinavyoendelea mjini Dodoma waliibua pia jambo hilo, wakitaka Serikali itoe ufafanuzi kutokana na kuwapo kwa tuhuma kuwa mmoja wa wateule wa Rais John Magufuli kwa nafasi za ukuu wa mikoa alitumia vyeti vya mtu mwingine kujiendeleza kielimu na kuachana na jina lake la Bashite.

Katika ufafanuzi ulioonekana kutotoa hatima ya kuhusu suala la Bashite, Serikali ilisema uhakiki wa vyeti uliofanyika kwa watumishi wa umma nchini kote haukuhusisha viongozi wa kisiasa.

Akizungumza kabla ya kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais Magufuli wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 10 ya Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), mjini Dodoma jana, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki, alisema kazi ya uhakiki haikuwagusa viongozi wa kisiasa wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa, wabunge na madiwani bali watendaji pekee wakiwamo makatibu wakuu, walimu pamoja na watumishi wengine wasio na vyeo vya kisiasa.

“Uhakiki huu hauwahusu viongozi wenye vyeo vya kisiasa kama Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Madiwani,” alisema Kairuki.
Kwa mujibu wa Waziri Kairuki, uhakiki ulihusisha vyeti vya watumishi zaidi ya 400,000 na kati ya hivyo, 9,932 vilibainika kuwa ni vya kufoji, sawa na asilimia 2.4.

Vyeti vingine vya majina zaidi ya 15,00 vilibainika kutumiwa na watumishi zaidi ya mtumishi mmoja na watumishi 11,596 walibainika kuwa na vyeti vya kitaaluma pekee bila ya vile vya kidato cha nne na sita.

Aidha, vyeti vya watumishi 376,969 (asilimia 94.2) vikionekana kuwa halali na havina shaka.

WABUNGE WANENA

Wakizungumza na Nipashe kuhusiana na suala la Bashite, baadhi ya wabunge walisema kiitaratibu, uhakiki uliofanyika usingeweza kugusa viongozi wa kisiasa kama Waziri Kairuki alivyosema na hivyo, kazi iliyobaki ni kutumia njia nyingine za kusaka ukweli wa jambo hilo.

“Ni kweli kwamba viongozi wa kisiasa hawabanwi sana kuhusu suala la vyeti vya kitaaluma, lakini linapokuja suala la mtu kutumia cheti cha mtu mwingine, ni wazi kwamba hapo kuna kughushi… na hilo ni kosa kubwa linaloweza kumfunga mtu jela. Hivyo suala la Bashite linapaswa kufanyiwa kazi zaidi.

Hatutaacha kulifuatilia,” mmoja wa wabunge wa kambi ya upinzani aliiambia Nipashe jana.

Mbunge mwingine aliyekataa jina lake kutajwa aliipongeza serikali kwa uhakiki uliofanyika kwa sababu utatoa fursa za ajira kwa vijana wenye sifa ili wazibe nafasi zitakazoachwa na pia kukomesha vitendo vya udanganyifu katika elimu.

“Hata hivyo, hili suala la Bashite linapaswa pia kutolewa ufafanuzi wa kina. Ni kwa sababu linahusisha uvunjifu wa sheria na kwa utaratibu wetu hakuna mtu aliye juu ya sheria. Serikali inapaswa kutoa ufafanuzi wa kina ili kumsafisha anayetuhumiwa au kumchukulia hatua,” mbunge mwingine aliongeza.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, akizungumza baada ya uamuzi huo, alisema anaipongeza serikali kwa mcakato mzima walioufanya kuhusu kuwafurumusha watumishi hewa na wale wenye vyeti vya kughushi.

Waitara alisema ilichofanya serikali ni kitu cha kupongezwa, lakini hawezi kukubaliana na kutowahusisha viongozi wa kisiasa ambao baadhi yao wanatuhumiwa kutumia majina bandia wakiwamo wakuu wa mikoa.

“Naungana na serikali kwa mchakato mzima walioufanya hata kuwabaini watumishi hewa pamoja na wenye vyeti ‘feki’, lakini wapo wakuu wa mikoa wanaotuhumiwa kutumia majina ambayo si yao, wameachwa,” alisema Waitara.

Alisema mkuu wa mkoa mmoja katika mji mkubwa, anatuhumiwa kutumia majina ambayo si yake, lakini amekingiwa kifua kwa madai uhakiki hauwahusu wanasiasa, anapingana na hilo.

Waitara alisema kuachwa kwa Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Madiwani, kunajenga matabaka na chuki kati yao na watumishi waengine wa umma.

“Kama Mkuu wa Mkoa anatuhumiwa kaghusi vyeti na kutumia majina ambayo si yake, sasa akiitwa awe mgeni rasmi kwenye mahafali ya chuo, atazungumza kitu gani mbele ya maprofesa….jambo hilo liangaliwe,” alisema.

Alisema uhakiki haupaswi kubagua viongozi kwa sababu wote wanawajibika katika tume ya maadili ya umma, hivyo kuwaacha wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa kisiasa, kunataleta mtafaruku.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), alisema uhakiki huo ulipaswa kuzingatia malalamiko ya wananchi kwa kuhusisha pia wanasiasa..

“Hiyo ni double stanbard. Ni vizuri kama malalamiko ya wananchi yangetazamwa na kuhusisha sisi wanasiasa katika uhakiki,” alisema Zitto.

HAKUNA MATATA NAPE AZIDI KUITEKA CCM ATUMA UJUMBE HUU MZITO KWA RAIS MAGUFULI...

Leo April 26, 2017 Tanzania inaadhimisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe zinazofanyika mjini Dodoma ambapo viongozi mbalimbali wamekuwa wakitoa pongezi kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kutimiza miaka hiyo.
Mmoja wa watu walioguswa na maadhimisho hayo ni Mbunge wa Mtama ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akitumia account yake ya Instagram na kuandika: CCM bado ni chama bora cha mfano kwa Afrika!!! Ni imara na kina historia ndefu, nzuri iliyotukuka sana!! Ndio waasisi wa Muungano wetu, TUUDUMISHE!!!!
#miaka53yamuunganowatanganyikanazanzibar.” – Nape Nnauye

BREAKING NEWS: HAKUNA ALIEAMINI HATIMAE MH NAPE AFANYA MAAMUZI MAZITO UPINZANI WAMLILIA VIKALI NAPE.

Usiku wa April 25 2017 Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia tiketi ya CCM Nape Moses Nnauye ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe wake wa wazi aliyowahi kuandika kipindi cha nyuma kuhusu CCM, lengo likiwa ni kuweka kumbukumbu sawa kwa watu kuhusu CCM.
Nape ametumia ukurasa wake wa twitter kupost screen shot za tweet zake za zamani na kuandika neno KUWEKA KUMBUKUMBU SAWA “Watu wengi wanaamini nimeisaidia sana CCM lakini ukweli ni kuwa CCM imenisaidia sana mimi kuliko mimi nilivyoisaidia, CCM ni SHULE” >>> Nape
Screenshot ya pili ya Nape Nnauye ambapo zote zinaonesha ni tweet ambazo aliziandika December 15 2016 ila usiku wa leo ameamua kuzikumbushia akisema ni kuweka kumbukumbu sawa “Bahati niliyopata kwa kuwa muenezi CCM ni kufanya kazi na ndg Kinana ni mwema, mzalendo, hodari, uwezo mkubwa, upendo na maarifa mengi” >>>Nape

BREAKING NEWS: SIRI NZITO YAFICHUKA PROF LIPUMBA AUMBUKA VIBAYA ABAINIKA KUHUSIKA TUKIO HILI ZITO LA KIKATILI.

Sasa si siri tena,kuwa wale waliovamia mkutano wa CUF-Maalim pale Vinna Hotel Mabibo,ni wafuasi wa Profesa Lipumba na zoezi zima liliongozwa na Kambaya toka ofisi za chama Buguruni.

Walioshiriki zoezi hilo,wengi ni wale waliohusika "kuuvuruga" mkutano wa CUF pale Ubungo Plaza wakati Prof Haruna Lipumba alipoamua kuingia kwa nguvu,kuvuruga mkutano,kuvunja viti na kuzabua watu makofi.

Aliyevunjwa mguu kwa kudhaniwa ni "jambazi" na wale "wananchi wenye hasira kali" ni mlinzi wa Prof Lipumba ambaye amekuwa naye katika mikutano na misafara mingi azungukayo Dsm na nje ya Dsm.Hata alipopigwa na kupigika,aliomba msamaha kwa kusema yeye aliyumwa tu na Prof Lipumba,anaomba raia wasimuuwe.

Gari mbili aina ya Land Cruiser zilizotumika kuvamia eneo la Hotel na kutokomea mara baada ya wananchi kuingilia kati,zimekutwa ofisi za CUF-Buguruni ambazo kwa sasa zipo chini ya himaya ya CUF ya Lipumba na wafuasi wake chini ya Abdul Kambaya.Magari yote yamevunjwa vioo na kujaa damu zilizotokana na vipigo toka kwa wananchi.
Msemaji wa CUF ya Lipumba ndugu Kambaya yeye alipoulizwa,kwanza alikubali kuwa magari hayo ndiyo yalikuwa Vina Hotel-Mabibo,na walioanza kuyavamia ni wafauasi wa Chadema waliokodishwa toka Arusha kuja kuivuruga CUF ya Lipumba,anasema ni kweli magari hayo na watu waliokuwa ndani yake walivamiwa na wahuni wa CHADEMA walioletwa toka Arusha kwa ufadhiri wa Meya wa Ubungo kuja kumuondoa Lipumba ofisini.

Kambaya anasema vijana wa CHADEMA waliotolewa Arusha kuja kuleta vurugu Buguruni,ndio walianza kuwavamia walinzi wa CUF waliokuwa katika doria ya kawaida ya kuangalia wapi CHADEMA na vijana wao wanakutana ili kutengeneza fitna za kumuondoa Prof Lipumba kwa nguvu pale Buguruni.

Kambaya anasema wao kama CUF hawatakubali uhuni huo uliofanywa na CHADEMA na Meya wa Ubungo kwa kushirikiana na Maalif Seif,wao kama vijana wapo tayari kukilinda chama chao kwa nguvu zote,wapo tayari kulipa kisasi na kusimamia chama chao.

Abdul Kambaya anasema magari hayo ya chama yapo ofisi za CUF Buguruni na wanayaacha kama ushahidi wa namna wahuni wa CHADEMA toka Arusha wakishirikiana na Meya wa Ubungo wanavyotaka kuivuruga CUF kwa pesa za mafisadi.

HABARI NZITO: HAKUNA ALIEAMINI HUU NDO MUUJIZA ANAOTUMIA MBOWE KUIONGOZA CHADEMA.

Mbunge wa Ulanga Mh.Mlinga amemjibu Mbowe kuwa CCM haitumii miujiza kutawala bali inatumia mpango mkakati kutekeleza ilani yake.

Vile vile ameeleza kuwa ni Mbowe ndiye mwenye kutumia miujiza kuongoza chama kwani amepata division sifuri form six lakini anatawala wafuasi wenye elimu za juu wakiwamo madaktari na maprofesa

KIKAOA CHA RAIS MAGUFULI NA WABUNGE CCM CHAZUA SINTOFAHAMU ZITO WABUNGE WANENA MAZITO MNO.

Ikiwa ni takriban siku 40 baada ya kikao kizito kilichofanyika Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma, wabunge wa CCM watakuwa na mkutano mwingine keshokutwa ulioitishwa na mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.

Hata hivyo, wabunge hawajaelezwa mahali wala muda utakaofanyika mkutano huo, kwa ahadi kuwa watataarifiwa baadaye.

Pia , wabunge hao hawajaelezwa ajenda za kikao hicho ambacho kwa kawaida huwa cha siri na ambacho hutumika kuweka misimamo ya chama katika masuala yanayojadiliwa au yanayotarajiwa kujadiliwa bungeni.

Katibu wa wabunge hao, Jasson Rweikiza ndiye aliyetuma ujumbe huo mfupi wa simu kwa wabunge ambao baadhi yao wameithibitishia Mwananchi suala hilo.

Ujumbe huo umemtaka kila mbunge awepo na hata wale waliosafiri, wajitahidi kurudi Dodoma kuhudhuria kikao hicho.

Alipohojiwa na gazeti hili jana, Rweikiza alisema Rais anaruhusiwa kuzungumza na wabunge wake muda wowote kwa hiyo hilo lisiwe nongwa linapotokea kwa CCM.

“Kwani (mwenyekiti wa Chadema, Freeman) Mbowe akiwataka wabunge wake inakuwa nongwa? Yeye ni mwenyekiti. Wabunge ni watu anaofanya nao kazi pamoja, hivyo kuwaita ili kuteta nao kujadili kazi isiwe nongwa,” alisema Rweikiza.

Rweikiza alisema Magufuli kama mwenyekiti wa CCM anaruhusiwa kuwaita wabunge na kukaa nao, kuongea au kuteta jambo lolote linalohusu mustakabali wa chama hicho.

“Mkumbuke yeye ni mwenyekiti wa chama tawala,” alisema.

Viongozi wa juu wa CCM na Serikali wanatarajiwa kuwepo katika kikao hicho, hasa kutokana na ukweli kuwa siku inayofuata itakuwa ni sherehe za Muungano ambazo mwaka huu zinafanyika mjini hapa.

Kwa maana hiyo, Rais Magufuli, Dk Ali Mohamed Shein (Rais wa Zanzibar), Samia Suluhu Hassan (Makamu wa Rais) na Phillip Mangula (makamu mwenyekiti CCM) na Abdulrahman Kinana (katibu mkuu wa CCM) wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho.

Vigogo hao wataungana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye yupo mjini hapa kuongoza shughuli za Serikali bungeni.

Vikao hivyo huwa vinaongozwa na Waziri Mkuu katika siku za kawaida za mikutano ya Bunge kwa kuwa mtendaji huyo mkuu wa Serikali huwa Dodoma kwa ajili ya mikutano ya Bunge.

Mara ya mwisho kikao baina ya Rais na wabunge hapo kilifanyika Machi 12, mwaka huu na Rais alitumia muda mwingi wa hotuba yake kuwaelekeza wabunge jinsi ya kuenenda, ikiwa ni pamoja na kuwaonya wasimpinge Waziri Mkuu.

Maelekezo ya Rais

Katika kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Kinana na Mangula, kiongozi huyo wa nchi aliweka bayana kuwa iwapo wabunge watampigia kura ya kutokuwa na imani naye (Waziri Mkuu Majaliwa), atamrudisha kwenye chombo hicho na iwapo watamkataa tena, atalivunja Bunge.

Rais aliwaambia watunga sheria hao kutoka CCM kuwa amepata taarifa kwamba wapo baadhi yao wanaotishia kuanzisha hoja ya kutaka Majaliwa apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye na kuwaambia wenye lengo hilo hawatafanikiwa kwa kuwa wakithubutu kufanya hivyo, atapeleka tena jina lake na wakirudia, atalivunja Bunge ili wote warudi katika uchaguzi.

Mbali ya kumkingia kifua Majaliwa, mwenyekiti huyo wa CCM pia aliwaonya wabunge dhidi ya vitendo vya kushirikiana na wapinzani kuishambulia Serikali, akitoa mfano wa mbunge wa chama tawala aliyemgawia muda wake wa kuchangia hoja mbunge wa upinzani.

Kwa kauli hiyo, alikuwa akirejea kitendo cha mbunge wa CCM, Boniface Getere kumpa dakika tano mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Ryoba wakati wa kuchangia taarifa ya Kamati za Bunge za Ardhi, Maliasili, Kilimo na Utalii.

Pia alieleza kukerwa na wabunge wa CCM wanaofifisha vita dhidi ya dawa za kulevya na mmoja akimtuhumu kutoa siri za chama kwa upinzani.

Rais Magufuli pia alieleza kuwa yeye ndiye aliyeamua kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya televisheni kwa baadhi ya shughuli za Bunge.

Pia, mwenyekiti huyo wa CCM alionya kitendo cha baadhi ya wabunge wa chama hicho waliotaka kumtembelea gerezani Arusha, mbunge wa Chadema, Godlbess Lema kwa madai kuwa kitendo hicho ilikuwa ni sawa na usaliti kwa chama.

Katika kikao hicho, wabunge pia walimweleza Rais kuhusu uhusiano wao na baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya, wakisema si mzuri na bado suala hilo limeendelea kujitokeza katika mijadala ya Bunge la Bajeti.

Baada ya kuwasikiliza, Rais Magufuli alianza kuwapa taarifa za mafanikio ya Serikali yake pamoja na mipango kabambe katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, akiwataka waiunge mkono Serikali katika maeneo yao huku suala la ujenzi wa reli pana, ambao tayari umezinduliwa, likipewa kipaumbele zaidi.

Kikao moto cha Bunge

Kikao cha keshokutwa kinakuja wakati Bunge likiwa limetawaliwa na mijadala inayoonyesha Serikali haijafanya kazi yake vizuri baada ya hotuba tatu za bajeti kusomwa.

Bajeti hizo ni ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo ilitawaliwa na majadiliano kuhusu vitendo vya utekaji, uvamizi na kuihusisha Idara ya Usalama wa Taifa na matukio hayo.

Suala la kutekwa kwa msanii Roma Mkatoliki, kitendo cha mteule wa Rais kuvamia studio za televisheni za Clouds Media, kutishiwa bastola kwa mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na kutoweka kwa kada wa Chadema, Ben Saanane yalitawala mijadala ya hotuba hiyo.

Bajeti nyingine ni za Ofisi ya Rais (Tamisemi) na Utumishi wa Umma na Utawala Bora, zilizojadiliwa kwa pamoja na kutawaliwa pia na hoja za utekaji na pia vitendo vya unyanyasaji unaofanywa na wakuu wa wilaya na mikoa.

Mawaziri pekee watetea

Tofauti na inavyokuwa wakati wa bajeti hizo, ni wabunge wachache wa CCM waliosimama au kuomba mwongozo wakati wapinzani walipokuwa wakiishambulia Serikali.

Badala yake, mawaziri watatu; George Simbachawene (Tamisemi), Angela Kairuki (Utawala Bora) na Jenista Mhagama (Bunge) ndio waliosimama mara kwa mara kutoa taarifa au kuomba mwongozo.

Hoja dhidi ya Serikali zinazotolewa na wabunge wa upinzani pamoja na wa CCM zinaweza kuchukua nafasi kubwa katika kikao cha keshokutwa, hasa ikizingatiwa kuwa shughuli nyingi za maendeleo hazikupata fedha za kutosha kama ilivyopangwa katika bajeti iliyopita.

Hadi wiki mbili zilizopita, miradi ya maendeleo ilikuwa imepewa asilimia zisizozidi 40 ya fedha zilizotengwa. Bajeti ya mwaka 2016/17 ilitenga asilimia 40 ya fedha zake kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Bajeti hiyo ya mwaka 2016/17 ilikuwa ya Sh29.5 trilioni na Sh11.8 trilioni zilitengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Wabunge wamekuwa wakiilalamikia Serikali kuwa fedha zinazotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali haziendani na kiwango kilichoidhinishwa na Bunge hilo na kusababisha nakisi ya zaidi ya asilimia 50 katika miradi ya maendeleo.

Hali ya uchumi inaweza kuibua mijadala mikali katika hotuba za bajeti za wizara zinazofuata, kutokana na malalamiko kuzidi kuongezeka, hasa sekta binafsi ambayo wadau wanadai kuwa mazingira ya biashara hayajakuwa rafiki.

Suala jingine ambalo limekuwa linazungumzwa na wabunge kutoka vyama vyote ni uhakiki wa vyeti vya mteule mmoja wa rais anayedaiwa kufeli kidato cha nne na kutumia vyeti vya mtu mwingine ambavyo vimeghushiwa jina ili vilingane na jina lake la sasa.

Suala hilo pia lilihojiwa na wabunge wa CCM katika kikao chao cha kwanza cha ndaniokabla ya mkutano wa bajeti kilichoongozwa na Waziri Mkuu.

Vilevile, zimekuwapo taarifa za wabunge kutaka masilahi yao yaongezwe, lakini hoja zao zimekuwa zikigonga mwamba na taarifa za ndani zinasema safari hii huenda kilio chao kikaongezeka.

Bunge, ambalo mwaka jana lilirejesha salio la Sh6.5 bilioni, mwaka huu limejikuta na nakisi ya Sh8.5 bilioni ambazo wabunge wameeleza hofu kama zitaweza kukifikia chombo hicho kabla ya kumaliza shughuli zake za bajeti.

HABARI NZITO: MZEE MTEI ACHARUKA VIKALI AFUNGUKA HATMA YA LOWASSA NDANI YA CHADEMA.

MWASISI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei, ameeleza kufurahishwa kwake na mwenendo wa uongozi wa kushtukiza na utekelezaji wa sera za Chadema unaofanywa na Rais John Magufuli. RAI linaripoti.

Tangu alipoingia madarakani Novemba 5, mwaka 2015, Rais Magufuli amekuwa akifanya ziara za kushtukiza katika idara na taasisi mbalimbali za umma, huku baadhi ya wachambuzi wa kisiasa wakidai kuwa anatekeleza Ilani ya Chadema.

Katika mazungumzo yake na RAI, Mzee Mtei ambaye pia alikuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), alisema Rais Magufuli amewafungulia njia wapinzani, hivyo wanamsubiri kwa hamu katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

“Tena nikuambie kwamba kama kuna jambo ambalo tunajivunia sisi ni pale ambapo serikali inatekeleza sera ya chama changu ambacho nilikianzisha. Hili linanipa furaha, pamoja na udhaifu uliopo ndani ya serikali ya Awamu ya Tano. Ukiangalia elimu, afya, barabara, kufufua reli, viwanda pamoja na mambo kadha wa kadha, najivunia kwamba chama changu ni chama bunifu, kila siku tunabuni mambo mapya kulingana na mabadiliko ya teknolojia.

“Chadema kinasikiliza maoni ya Watanzania, bila kujali ukanda wala kabila. Chadema ni wapenda amani, tutaendelea kumwenzi hayati Baba wa Taifa hili na mwaasisi wetu aliyetukomboa mikononi mwa wakoloni. Alionyesha uzalendo na siyo chama. Hakutaka madaraka, alitanguliza uzalendo wake, tofauti na viongozi wa chama tawala ambao mawazo yao yametawaliwa na uongozi na siyo uzalendo wa kuipenda nchi yao. Hili ni jinamzi linalolitafuna Taifa hili.

“Sasa hivi mimi siwezi kupambana kwenye majukwaa ya siasa, ila nitaendelea kuwaonya viongozi wa chama changu kwa kutumia  mitandao ya kijamii whatAspp na mitandao  mingine, ili waendelee kuyaenzi yale yaliyomema ya kulijenga Taifa hili,” alisema.

HALI YA KISIASA

Akizungumzia hali ya kisiasa nchini, Mzee Mtei alisema hali inabadilika badilika kutokana na mtindo wa Rais Magufuli anaoutumia kuongoza nchi.

“Hivi sasa nchi inaongozwa na Rais ambaye anafanya mambo yake kwa kushtukiza shutukiza na sisi tunamwangalia tu, tuone atafika wapi. Pili nchi haiwezi kuendeshwa kwa mtindo wa namna hii, nchi inatakiwa kuendeshwa kwa kufuata sheria na Katiba.

UJIO WA LOWASSA

Aidha, akizungumzia ujio wa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ndani ya Chadema na kupewa nafasi ya kukiongoza chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Mzee Mtei alisema ujio huo ulionyesha ni jinsi gani Watanzania, pamoja makada wa walioko ndani ya CCM walivyochoshwa na mambo ambayo yaendelea ndani ya Serikali.

“Lowassa alikuja kuunga mkono, ili kuleta ukombozi wa Watanzania ambao bado wako kwenye giza nene na hawajui wanakwenda wapi, mbali kuwa nchi yao imesheheni rasilimali nyingi na ardhi zenye rutuba.

“Lowassa pia alikuja ili atusaidie kuchukua nchi, lakini niwaambie kwamba bado tutaendelea kuwa na Lowassa hatutaweza kumtupa. Alileta mabadiliko makubwa sana aliwachangamsha vijana, aliweza kuamsha ari mpya.

SLAA ALINIVUNJIA HESHIMA
Akizungumzia uamuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa kuondoka ndani ya chama hicho katika kipindi cha mwisho cha mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2015, Mzee Mtei alisema hilo ni jambo lililomsitikisha sana.

“Kwanza aliondoka kipindi ambacho tuko kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu. Binafsi Dk. Slaa ni rafiki yangu wa karibu sana, kwa jina lingine namfananisha kama kijana wangu, kabla ya kuondoka kwake nilimsihi sana lakini hakunisikia, nilimwandikia ujumbe mbalimbali kumtaka anieleze juu ya kuachana kwake na siasa, hakunijibu. Nikamwandika barua, hakujibu nikajisikia vibaya sana. Sikutegemea kama angenifanyia hivyo.

“Ukimya wake wa kutonijibu niliona mimi kama rafiki yake msiri wake, tena mtu mzima, moja kwa moja nikaona kama amenivunjia heshima.

“Siwezi kumsahau kwani alikuwa chachu kwa vyama vya upinzini, alikuwa mwanamapinduzi wa kweli, bila kujali ni nani anapambana nae. Kwenye siasa alikuwa akiisema Serikali bila kuogopa, tena kwa hoja. Alikuwa mtu ambaye aliipenda nchi yake, alikuwa akikisema chama tawala kwa kuwataja mafisadi waliokuwa wanatafuna nchi bila kuwaangalia usoni, tena kwa ushahidi. Pia alikuwa akishirikiana na viongozi wa wake katika kila hali, ni mtu asiyependa kuonewa wala kuwaonea wengine.

“Ila nina imani Dk Slaa bado ni mwanaChadema na ataendelea kuwa mwanamapinduzi, hata ukiangalia siyo yeye pekee yake aliyeondoka, waliondoka wengi wazuri pia, akina Zitto Kabwe na wengine, lakini heshima yake inabaki pale ambapo alibaki bila kujiunga na chama kingine. Huo ndiyo uzalendo wa kweli, hata akija nchini nitamwita, maana najua hatokataa mwito wangu,” alisema.

MWELEKEO WA CHADEMA 2020

Akizungumzia Uchaguzi Mkuu ujao wa 2020, Mzee Mtei alisema hivi sasa chama hicho kimejipanga, kwa kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kilishiriki na kufanya vizuri kuanzia ngazi za udiwani, ubunge na urais, lakini CCM kwa uzoefu wao waliiba kura kwa kutumia nguvu ya dola.

“Kwa kuwa Chadema ni chama makini na kinaongozwa na watu ambao ni wasomi, wenye maadili, hatukutaka kwenda kufanya maandamano. Pili, kwa kulinda heshima ya Watanzania waliotuamini, hatukutaka kufanya mikutano ya kupinga matokeo ya urais. Tatu, Watanzania walio wengi, hawakuwa tayari kwa mabadiliko uongozi wa juu kwa kuhofia huenda ingeleta vita endapo mgombea wa Chadema, Edward Lowassa angetangazwa kuwa rais.

“Ila uchaguzi ujao mwaka 2020, Chadema tutashinda kiti cha urais kwa kishindo kwani tumejipanga, hatutaogopa chochote siwezi kuweka wazi mkakati wetu tuliyopanga.

“Kwa sababu tunaona pia kijana wetu Zitto Kabwe amedhamiria kuongeza nguvu, jambo ambalo ni jema na linaonesha jinsi gani vijana wangu niliowalea, wamekomaa kisiasa. Zitto bado ni mwanachadema, kuihama Chadema haimzuii Zitto kuipenda Chadema. Bado ana mapenzi ya dhati, kwani ndiyo chama ambacho kilimleta na kilimpa umaarufu kwenye nyanja za kisiasa ndani na hata nje ya Tanzania.

Naamini muungano wa UKAWA utasaidia kuimarisha upinzani kuingia madarakani mwaka 2020, pia utasaidia kuua nguvu za chama tawala, kwani ndicho kilichokuwa kikiwagharimu na kushindwa kufanikiwa kutokana na mgawanyiko wa upinzani. Umoja ni muhimu sana katika kudai haki na kujenga Taifa, hasa kwa nchi kama Tanzania ambayo haijawahi kutawaliwa na vyama vya upinzani.

Licha ya muungano huo, Mzee Mtei anasema bado hawajaweka mikakati ya kuainisha jina la mgombea urais katika uchaguzi wa 2020.

“Naweza nikasema ni sahihi au la, lakini Lowassa bado ni wa kwetu, siwezi kuiweka wazi mikakati ya chama kwani maamuzi yatakuja wakati ukifika, kwa sasa bado ni mapema mno na kama mnavyojua, Chadema ndiyo chama pekee nchini kilichosheheni vichwa vilivyojaa ubunifu na sera ambazo hazikopiki.

Pili Chadema ni chama ambacho kinasikiliza maoni ya Watanzania na kuyafanyia kazi kulingana na mabadiliko hali ya kisiasa katika nchi kwa wakati husika.

Tatu tutaangalia ni kwa namna gani tutaboresha, ili kuchukua nchi mwaka 2020 kwa kushirikiana na vijana wetu walioko ndani ya chama. Na imani yetu kubwa ni kuchukua nchi mwaka 2020, kwani sasa wananchi wako tayari kwa maamuzi yoyote na kuna kila dalili, hata ukisema uchaguzi ufanyike leo, lazima tuchukue nchi. Watanzania wa leo sio wale wa jana. Ndio maana nasema Tanzania mpya inakuja.



SERIKALI YA AWAMU YA TANO

Aidha, akizungumzia mwenendo wa Serikali ya awamu ya Tano, Mzee Mtei anasema kiujumla Rais Magufuli ni kiongozi mzuri kwa kiasi, ila anadhani Watanzania wataamua kwa kuwa ni mtu wa kufanya mambo kwa kushtukiza.

“Amekuwa akifanya maamuzi yake kwa matukio na siyo kuwasikiliza Watanzania wanasemaje, nini mahitaji ya watu wake, hivyo sisi kama wapinzani tunaangalia tu tuone ataifikisha wapi nchi kwa miaka mitano. Sasa hivi tayari amebakisha miaka mitatu tu,” alisema.

Pamoja na mambo mengine, alisema ni kosa kubwa kumfananisha Mwalimu Nyerere na Magufuli kwa kuwa Nyerere alikuwa analipigania Taifa kutoka kwenye makucha ya wakoloni.

“Huwezi kumfananisha na wanasiasa vijana, tena wanaoliharibu Taifa, Mwalimu Nyerere alikuwa anapigania haki na kuikomboa nchi mikononi mwa wakoloni, leo hii watu kumfananisha na wanasiasa ni jambo la kusikitisha sana,” alisema.

Anasema sera ya kufufua viwanda ni sera ambayo haitekelezeki kwa kuwa jukumu hilo ni jambo linalohitaji maandalizi makubwa.

“Kwanza lazima uwaandae wananchi unaowaongoza, pia kushirikiana na pande zote pili bila kuangalia itikadi ya vyama, kuandaa mazingira ya wawekezaji wa ndani na wa nje, upatikanaji wa malighafi pamoja watalaamu wa masuala kiuchumi na viwanda. Tatu, lazima uandae au kutenga ardhi kwa ajili ya viwanda  kwani hakuna njia rahisi bila kufuata hatua zote.

Aidha, alisema uamuzi wa Rais Magufuli wa kufuta mikutano ya kisiasa hadi 2020, ni jambo ambalo limewafungua macho wapinzani kwa kutumia mitandao ya kijamii kufanya siasa za kimyakimya.

“Ni utashi wa kiongozi aliyeko madarakani na chama chake, na sisi kwetu ni fursa, ametupa mwanga wa kuona mbali zaidi. Pili amevisaidia vyama vya upinzani kuongeza ubunifu, kubadilisha namna ya kufanya siasa na kwamba siyo lazima kufanya siasa kwenye majukwaa.
Ametupa fursa nyingine nzuri ya kufanya siasa badala kutumia gharama kubwa kuandaa mikutano na watu, tunatumia mitandao ya kijamii kuwaeleza Watanzania na tumegundua njia hii ni bora zaidi, kwani tumeweza kuwafika idadi kubwa ya vijana, wamama pamoja na wababa.
“Sasa hivi ukirusha kitu kwenye mitandao ya kijamii baada ya dakika tano tayari unapokea zaidi ya komenti za watu 1000 kutoka mikoa yote Tanzania na hata nje ya nchi, imetusaidia kufanya siasa za kimya kimya, kuliko kuandaa mkutano ya hadhara. Binafsi na namshukuru kwa utashi wake ametufungua macho na ufahamu zaidi. Siasa hazizuiliki kamwe,” alisema. 

Credit - Rai
Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top