Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

FAHAMA NJIA HIZI ZAKULINOGESHA PENZI LAKO KWAKE DAIMA...


KUPITIA safu hii uipendayo, leo ninakupa njia nne zitakazolifanya penzi lako liendelee kunoga, hata kama litakuwa limeanza kufubaa utaliamsha upya.

Wengi wamekuwa hawaelewi mambo mengi kuhusu uhusiano ndiyo maana huishia kulalamika kwamba wanapenda sana lakini mwisho wa siku huishia kutendwa.

Hakuna mtu ambaye hahitaji faraja, kila aliyekuwa na mpenzi wake anahitaji kuwa na furaha. Hakuna mtu ambaye anaingia kwenye mapenzi ili apate msongo wa mawazo, kila mtu anayediriki kuutoa moyo wake, kitu cha kwanza anachokitarajia ni faraja kisha furaha.

Ipo hivyo! Watu wengi wanakuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi huku wakiwa na matumaini kwamba hao waliokuwanao inawezekana watakuwa wapenzi wa maisha yao yote. Pasipo kujua, wakati mwingine kuna makosa hufanyika, mtu hajui afanye nini ili penzi alilonalo kwa mpenzi wake linoge, hajui ni njia zipi zitamfanya kupendwa kila siku.

Leo nitakutajia njia chache ambazo kama utazifanya, nakuhakikishia penzi lenu litashamiri zaidi ya lilivyo hivi sasa.

MPE UHURU KWANZA

Kila mtu anapenda kuwa huru, kuachwa afanye mambo yake anayoyapenda. Hakuna mtu anayependa kuingiliwa, hasa kwenye masuala ya kutumia simu yake. Kama kweli unahitaji penzi linoge, usitake kuingilia mambo yake hasa katika matumizi ya simu, unachotakiwa ni kumwambia muda ambao hupendi kuona akizungumza na simu na si kwamba kila unapoona simu yake inaita, unaichukua kwa nguvu.

Mapenzi hayapo hivyo, mpe uhuru mwenza wako. Haimaanishi mtu kama hajatulia basi kuchukua simu muda wote inapoita ndiyo kutamfanya kutulia, hapana, bali kwa kufanya hivyo utampa mbinu nyingine ya kuweza kupambana nawe. Unachotakiwa ni kumfanya kuwa huru, usimuingilie.

CHUKUA MUDA WAKO KUMTOA ‘OUT’

Wengi hukosea hapa, huwa hawapendi kwenda matembezi na wapenzi wao. Wengine hujifanya wapo bize, hata ukimwambia Jumamosi nataka tutoke out atakwambia anataka kufanya hili na lile.

Rafiki yangu, kila mtu anahitaji kuwa karibu na mpenzi wake, hakuna anayependa kuwa na mpenzi ambaye muda wote yupo bize tu. Mchukue, nenda naye sehemu. Kutoka mitoko ya mara kwa mara itawafanya muwe karibu zaidi, itawafanya muda wote mzidi kupendana, ila kama utajifanya upo bize, jua kuna mtu ataitumia nafasi hiyo kutoka na umpendaye.

PENDELEA KUFANYA UTANI

Hakuna mtu anayempenda mpenzi ambaye yupo siriazi saa ishirini na nne. Pata muda wa kukaa na kutaniana naye. Mchombeze kwa vineno vya utani, mpetipeti, mlaze kitandani na uanze kupiganapigana naye vibao vya kimahaba hata kwa kutumia mito ya kulalia.

Unapokuwa siriazi kila wakati inakuwa ni vigumu mwenzako kulifaidi penzi, pendelea kutabasamu inapobidi kila unapokuwa na mpenzi wako, siyo kila atakachokwambia wewe uso wako umekunja ndita kiasi kwamba ataonekana kukuogopa na kumtafuta mtu mwingine ambaye atahitaji kuliona tabasamu lake, atahitaji kuona akifanyiwa utani wa mahaba nk.

HEBU MSIFIESIFIE BASI

Wengi wanaogopa kuwasifia wapenzi wao, hawajui kama kila mtu duniani anapenda kusifiwa. Mpenzi wako anapovaa nguo nzuri zilizomtoa, usikae kimya, mwambie amependeza kwani hilo litamfanya kufurahi sana. Kama utakuwa na mpenzi halafu kila siku humsifii hata akifanya kitu gani, jua kwamba atajisikia vibaya, wakati mwingine atahisi hayupo sawa kwa kuwa tu hujawahi kumsifia.
Unapomsifia mpenzi wako kunamfanya kuongeza umakini katika kuvaa kwake, kununua manukato na hata jinsi atakavyosuka au kunyoa atafanya kwa ubora wa hali ya juu kwa kuwa anajua utamsifia

BREAKING NEWS: MAAMUZI MAZITO YA KISHERIA YAMUWEKA PABAYA KIKWETE HAKUNA ALIEAMNI HILI..


Nimeona kwenye mitandao ya kijamii  baadhi ya wachangiaji wakimdhihaki Tundu Lissu kwamba anachemka kusema Kikwete ahojiwe. Wapingaji hawa wanashangaa uanasheria wa Tundu Lissu kwamba iweje hajui kama Kikwete ana kinga. Tundu Lissu. Wabongo wavivu kusoma, naomba niweke Ibara ya 46 na Ibara ndogo zake tujadili namna ya kumdaka Jakaya Kikwete


46.-(1) During the President’s tenure of office in accordance with this
Constitution it shall be prohibited to institute or continue in court any criminal proceedings whatsoever against him.

(2) During the President’s tenure of office in accordance this Constitution, no civil proceedings against him shall be instituted in court in respect of anything done or not done, or purporting to have been done or not done, by him in his personal capacity as an ordinary citizen whether before or after he assumed the office of President, unless at least thirty days before the proceedings are instituted in court, notice of claim in writing has been delivered to him or sent to him pursuant to the procedure prescribed by an Act of Parliament, stating the nature of such proceedings, the cause of action, the name, residential address of the claimant and the relief which he claims.

(3) Except where he ceases to hold the office of President pursuant to the provisions of Article 46A(10) it shall be prohibited to institute in court criminal or civil proceedings whatsoever against a person who was holding the office of President after he ceases to hold such office for anything he did in his capacity as President while he held the office of President in accordance with this Constitution.

UFAFANUZI
Ibara hii inazungumzia Kinga anayopewa Rais. Ibara ya 46 ibara ndogo ya 3, inasisitiza hatashitakiwa kwa makosa aliyofanya katika kipindi akiwa Rais na si vinginevyo. Hivyo Kikwete anaweza kudakwa kwenye makosa aliyofanya akiwa Waziri wa Nishati na Madini.

NYONGEZA
Kwa hiyo hata kwa katiba hii,hata Rais Magufuli akitolewa madarakani 2020 tunaweza kumuundia kamati na kumshitaki kwa makosa ya MV Dar es Salaam na uuzwaji wa nyumba za serikali.

MY TAKE
Nadhani Magufuli hakujua kama wale ''wahuni'' kina Tundu Lissu watamfikisha huku, matokeo yake anaweza kurudi nyuma ikawa kama zile kamati zingine zilizopita

HABARI NZITO: NI HATARI WEMA SEPETU KUANDIKA HISHORIA NZITO MAHAKANI HII LEO...


Kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayomkabili Wema Sepetu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirishwa hadi Julai 10.

Wema ambaye ni mshindi wa taji la urembo, maarufu Miss Tanzania kwa mwaka 2006 na msanii wa filamu, anakabiliwa na kesi hiyo akidaiwa kutumia na kupatikana na bangi.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa alisema kesi ilipangwa leo (Jumatano) kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka lakini Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba anayeisikiliza kesi hiyo yupo likizo.

Kutokana na hilo, aliomba iahirishwe hadi Julai 10 ombi lililokubaliwa na mahakama.

Wema na wenzake Angelina Msigwa na Matrida Abbas wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na dawa za kulevya na kutumia dawa hizo.

Inadaiwa Februari 4, katika makazi ya Wema, Kunduchi Ununio, walikamatwa wakiwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Wema pia anadaiwa Februari Mosi katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam alitumia bangi.

HOT NEWS: KIMENUKA BUNGENI SPIKA NDUGAI, KAMBI YA UPINZANI WAKABANA MAKOO SHUHUDIA TUKIO HILI HAPA..

Bungeni
Spika wa Bunge, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa upinzani wanaotaka marais wastaafu washtakiwe kuhusu sakata la mchanga wa madini, wakumbuke wanao mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao watahusika pia.

Ndugai amesema hayo leo (Jumanne) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa ya Rais.

"Haiwezekani mzee wangu (Andrew) Chenge na (Nazir) Karamagi walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu. Kinga ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe," amesema Lijualikali.

Baada ya hoja hiyo ya Lijualikali inayofanana na ya Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Ndugai aliwakumbusha juu ya mawaziri wastaafu walionao kwenye chama chao.

"Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena," amesemaNdugai.

ZITO KABWE AKINUKISHA TENA ATUMA UJUMBE MZITO KWA RAIS MAGUFULI HAKUNA ALIEAMINI HAYA...


"Mwisho wa siku historia inaandikwa tu. Uzalendo ni kufanya jambo ambalo wengi hawakuelewi lakini wewe unajua Ni jambo sahihi na unakubali kutukanwa, kususubikwa, kusimangwa, kuzushiwa, nk. Unapambana tu. Mwisho wa siku waliokuita msaliti watakuita shujaa. Waliokuzomea wanashangilia. Wewe unafanya nini? Unakaa kimya kwani kwenye kukaa kimya pia kuna kusema kukubwa zaidi. Muhimu Nchi ifaidike.

Huko nyuma nilipata kusema, hata mungu akinichukua sasa unakwenda ukiwa umetabasamu kwani unakuwa umetimiza wajibu wako duniani. Kina Josina Umm Kulthum wataishi Kwa heshima inshallah"

Ameandika Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook mara baada ya ripoti ya pili ya mchanga wa madini kuwasilishwa

BREAKING NEWS: KIMENUKA RIPOTI YA PILI MCHANGA WA MADINI CHENGE ,NGELEJA NDIO BASI TENA YAWAKUTA MAZITO..


Ripoti ya kamati ya pili kuhusu mchanga wa madini imewaibua Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Sengerema, Wiliam Ngeleja kuhusu mikataba ya madini iliyoingiwa miaka iliyopita.

Mbali na hao pia imewaibua marehemu Dk Abdallah Kigoda aliyekuwa Mbunge wa Handeni na Daniel Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Majina ya viongozi hao yameibuka leo wakati  mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Nehemiah Osoro alipokuwa akiwasilisha matokeo ya ripoti yake.

HABARI NZITO: PAUL MAKONDA KWELI KIBOKA AMWAGA MABILIONI KATIKA JAMBO HILI ZITO MNO..



Ikiwa ni nje ya Zawadi zilizokuwa zimeandaliwa kwajili ya Washindi wa mashindano makubwa afrika ya kuhifadhi na kusoma Qur-an juzuu 30 Kati ya washiriki 17 kutoka nchi 15 Barani Afrika yaliyofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, Tanzania, Katika hotuba yake Mkuu wa mkoa wa jiji hilo Paul Makonda naye kwa upande wake alitamka kuongeza shilingi Milioni 5 kwenye zawadi za washindi watano waliopatikana.

Mohamed Abdullah Aden kutoka Somalia ndiye ameibuka mshindi wa mashindano makubwa Afrika ya kusoma na kuhifadhi Qur-an juzuu 30 amekabidhiwa hundi ya Shilingi Milioni 15 kutoka Amana Bank, halikadhalika amepewa cheti cha ushindi, Ipod na kuchagua kwenda nchi yeyote duniani, kijana huyo wa miaka 12 ametoa wito kwa vijana kujibidisha Katika kusoma Qur-an.

Mashindano hayo ya 18 yaliyo andaliwa na Taasisi ya Al-hikma Foundation yamehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa, Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeiry, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda, Skeikh Mkuu Dar es salaam Alhad Mussa Salum, Rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi Sambamba na ujumbe Maalumu kutoka nchini Saudiarabia.

BREAKING NEWS: HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE RAIS MAGUFULI NDIO BASI TENA AIBUA SAKATA ZITO MNO NCHINI...




Siku chache tangu akabidhiwe ripoti ya mchanga wa madini, Rais Magufuli atapokea taarifa ya kamati ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga wa madini Jumatatu June 12, 2017 Ikulu Dar es Salaam.

AyoTV na millardayo.com zitakuletea tukio hili moja kwa moja  kwenye Youtube ya millardayo kuanzia saa 3:30 Asubuhi.

CRISTIAN BELLA NDIO BASI TENA HUU NDIO UKWELI HALISI JUU YA AFYA YAKE KWA SASA..

Baada ya wiki iliyopita kusambaa picha mitandaoni za muimbaji Christian Bella zikimuonyesha akiwa amelazwa hospitali nchini Congo na kuzua hofu kwa mashabiki wa muziki wake, muimbaji huyo amefunguka kuzungumzia kitu ambacho kilimsibu.

Akiongea Ijumaa hii, Bella amesema alikimbizwa hospitali baada ya kuishiwa nguvu ghafla.

“Namshukuru Mungu anaendelea vizuri, nililazwa kwa muda mfupi kutokana na uchovu lakini baada ya kufanyiwa vipimo nilikutwa nimechoka tu. Kwahiyo baada ya kupumzika niliruhusiwa lakini niliambiwa natakiwa nitenge muda wa kumpumzika kwa sababu nilikuwa na tour ya muda mrefu kwa hiyo mwili ulikuwa umechoka sana,” alisema Bella.

Muimbaji huyo ambaye ni raia wa Congo, kwa sasa amerejea nchini Tanzania kwaajili ya kuendelea na shughuli zake za muziki baada ya kuwa na tour kubwa ya nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kati.

COMFIRMD MAAMUZI YA MWISHO YA MANCHESTER UNITED KUHUSU ZLATAN IBRAHIMOVC



Club ya Man United ya England msimu uliyopita ilimsajili staa wa soka wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kama mchezaji huru kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya staa huyo kumaliza mkataba na club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Zlatan alikuwa anatajwa kwa kiasi kikubwa kuwa mkataba wake uliyokuwa unamalizika mwisho wa msimu huu na Man United, angeongezewa wa mwaka mmoja zaidi lakini kuumia kwake kumeifanya Man United kutangaza maamuzi ya kuachana nae.

Ibrahimovic aliumia goti mwezi April wakati wa mchezo wa Europa League na baada ya kufanyiwa uchunguzi iliripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja hadi mwaka 2018, hivyo kumalizika kwa mkataba wake kumeifanya Man United kuamua kuachana nae jumla.

EBITOKE AFUNGUKA MAZITO KILICHOMUUMIZA MNO BAADA YA KUSIKIA JAMBO HILI LA PEN POL..

Ebitoke
Moja ya story kubwa hivi sasa ambayo ina-make headlines ni kuhusu Mchekeshaji Ebitoke kuweka wazi akieleza hisia zake kuwa siku moja anatamani kuwa mke wa staa wa RnB Bongo Ben Pol.

Kwenye EXCLUSIVE Interview na Ayo TV na millardayo.com Ebitoke ameeleza kila kitu kuhusu anavyohisi kila anapomuona Ben Pol na namna alivyojiweka tayari kuwa mke wa staa huyo Bongofleva akidai kuwa hakuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote kwa ajili ya Ben Pol akisema ameumia baada ya kujua ana mtoto. 

HABARI NZITO: ZITTO KABWE ANNA MGWIRA WATIFUANA BILA HIYANA ZITO AFUNGUKA MAZITO...

Mbunge wa Kigoma Mh Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni kiongozi wa ACT wazalendo amesema kwamba wameamua kumuweka pembeni mwenyekiti wao wa zamani Mama Anna Mghirwa ili kutoa dhana kwamba ACT ni CCM B.

"Sasa tunaweka kanuni ambazo mtu akichaguliwa na uongozi wa juu unaoongozwa na Chama kingine tofauti na ACT basi tufanye kwanza mazungumzo kabla ya mtu kukubali tu bila kutoa taarifa" alisema Mh Zitto Kabwe.

Pia akaongeza kwa kusema kwamba kwa sasa wameshachagua kaimu mwenyekiti wao wa Chama na anaendelea na majukumu kama kawaida.

RAPA KIPENZI CHA WATANZANIA ROMA NDIO BASI TENA HATIMAE AFUNGUKA SIRI NZITO YA KUTEKWA KWAKE HII LEO...


RAPA kipenzi cha Watanzania, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amefunguka kuwa afya yake imeimarika na sasa yupo tayari kupanda jukwaani kukamua shoo kama kawaia yake.

ROMA ameyasema hayo jana wakati akitoa neno la shukrani kwa uongozi na wafanyakazi wa Kampuni ya Glopbal Publishers kwa kuendelea kumsapoti, kufanya naye kazi, kuboresha mahusiano yaliyo mema na kumfariji hasa katika kipindi kigumu alipopatwa matatizo ya kutekwa akiwa na wenzake watatu.

“Nimfika hapa kwa ajili ya kutoa neno la shukrani kwa jinsi ambavyo tmekuwa tukifanya kazi pamoja, pamoja na matatizo yaliyotukuta mimi na wenzangu lakini nyinyi Global Publishers mmeendelea kuwa na mimi katika kipindi chote hicho.

“Mtu akiona nimeweza kutembea kutoka nyumbani mpaka kufika hapa ofisini (Global PUblishers), basi ajue nipo fiti, na ninaendelea vizuri. kama nimeweza kushika maiki, nikazungumza basi hata Dar Live naweza kushika maiki (akimaanisha kufanya shoo).

“Niliona kipindi cha matatizo mlitupigania, magazeti ya Global Publishers yalifanya coverage nzuri na mlikuwa upande wetu. Kiukweli tulifarijika kuona watu wengi wakitutia moyo na kutupatia neno la faraja,” alisema Roma.

NOMA SANA NI KUFURU YA KARNE MSANII NISHA AKIRI YU MAPENZI NA MNYAMA HUYU...

Salma Jabu aka Nisha
WAKATI waumini wa Dini ya Kiislam wakiendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, msanii wa filamu, Salma Jabu ‘Nisha’ ametoa kali ya mwaka kufuatia kukiri kuwa na uhusiano na mbwa.

Nisha alifanya hivyo juzikati baada ya kuweka picha kwenye ukurasa wake wa Facebook akiwa amevaa gauni jeupe la harusi huku mkononi akiwa ameshika mkanda wa mbwa na kuandika kuwa, mnyama huyo ndiye mpenzi wake, jambo ambalo liliwachefua baadhi ya marafiki zake.



Dada acha kukufuru halafu huu ni Mwezi Mtukufu, Kiislam mbwa ni najisi halafu wewe ni Muislam unashika mbwa na kusema ndiyo mpenzi wako, tangu lini mbwa akawa na uhusiano na binadamu?” aliandika mmoja wa mashabiki aliyeonekana kukerwa na kitendo hicho. Jitihada za kumtafuta Nisha kuzungumzia kitendo alichokifanya hazikuzaa matunda baada ya simu yake kutopokelewa na hata alipotumiwa SMS hakujibu.

MAAMUZI MAZITO YA JUMA KASEJA BAADA YA KUAMUA KUSTAAFU SOKA AFUNGUKA MAZITO MNO LEO HII..


Mlinda mlango mkongwe hapa nchini ambaye sasa anachezea Kagera Sugar Juma Kaseja amepanga kuwa mtangazaji wa radio au televisheni baada ya kustaafu kucheza soka.

Juma Kaseja amesema hayo alipokuwa akihojiwa na kusema atakapostaafu kucheza soka ataingia rasmi katika kiwanda cha utangazaji, ambapo awali ataanza kwa kutumia kipaji chake lakini kadri siku zinavyozidi kwenda itabidi aingie shule ili kuwa mtangaji mzuri zaidi na bora.

"Kila kitu kinahitaji elimu, ila mimi kwanza nitaanza hivi hivi nilivyo halafu kadri nitakavyozidi kwenda nitakuwa najiendeleza na shule ili niwe mtangazaji mzuri" alisema Juma Kaseja 

Mbali na hilo Juma Kaseja amesisitiza wachezaji wadogo wanaokuja kwenye soka wanapaswa kuwa wavumilivu, wasikivu kwa walimu wao na kuwa na nidhamu kama wanapokuwa kwa wazazi wao.

MSANII MADEE NA MKE WA ROMA NDIO BASI TENA WAFANYA MAZITO UKO...

Mke wa msanii Roma Mkatoliki Nancy Mshana ameonesha kukerwa kwa kitendo cha msanii Madee kutoa kauli iliyojaa udhalilishaji kwa kusema Roma apone na aache kujilegeza.

Hayo yameibuka baada ya Nancy ku-post picha ya pamoja yeye na Roma katika mtandao wa kijamii wa instagram na kuandika maneno yenye kumtia faraja mume wake kwa kusema 'Be a friend encourage someone take time to care. Let your words heal and not wound'

"Apone basi na yeye asijilegeze kha! wanaume wa tanga bana" Ali-comment Madee

Akajibu Nancy...."Nimewaona marafiki na baadhi ya wasanii wakija kumuona, nilitegemea wewe ungekuwa wa kwanza kuja kumuona rafiki yako, ndugu yako, mtani wako lakini huu ni mwezi umekatika sijaona hata ukimpigia simu ! wala kuja kumjulia hali, hakika nimejifunza mengi sana kipindi hiki, ubarikiwe sana shemeji yangu Hamad, msalimie mtoto wetu Saida".

HABARI NZITO: KABWE AKINUKISHA CHADEMA AWAPA MAKAVU LIVE CDM..


Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa amesikitishwa sana na matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) uliofanyika jana usiku bungeni mjini Dodoma kwa upande wa Chadema.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto ameandika kuwa kuchagua watu bila kuangalia uwezo, uzoefu na uhusika wao kulingana na sehemu wanapotakiwa kuwepo ni kuliangamiza taifa, hasa ukizingatia changamoto zilizopo katika nchi hizo Afrika Masahriki.

Amesema kuwa nchi kama Rwanda, Burundi na Uganda zimepeleka wawakilishi mashuhuri na wenye uzoefu mkubwa katika bunge hilo kulingana na umuhimu wa shughuli zinazofanywa na bunge hilo.

“Jana usiku nilikuwa na hasira sana, kufuatia matokeo ya uchaguzi wa wawakilishi wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki (EALA) haiwezekani kuchagua wabunge ambao hawana uwezo wa kwenda kujenga hoja, huku tukitegemea kupambana na changamoto za muungano wa nchi hizi za Afrika Mashariki”ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Facebook.

ALIKIBA AUWASHA MOTO ATUA NCHINI KWA KISHINDO ATUMA UJUMBE MZITO KWA DIAMOND...

Habari njema za Mastaa wa bongo kutengeneza njia za kujiongezea kipato zaidi kwa kutengeneza bidhaa zenye majina yao zinaendelea kuongezeka ambapo leo ni zamu ya Alikiba.
Zikiwa zimepita wiki mbili toka Mwimbaji mwingine staa wa Bongofleva Diamond Platnumz kuzindua Perfume yake, leo May 11, 2017 kupitia 255 ya XXL Mwimbaji staa wa ‘aje’ Alikiba ameweka wazi kuwa moja ya mipango yake ni kutoa mavazi aina ya jeans, miwani, viatu na vinywaji vya energy vyenye jina lake.
Alikiba amesema kuwa hiyo ni mipango mizito na hatarajii kuifanya kiholela kwani hata mwanzo alifanya kama promotion lakini sasa hivi hayupo tayari kuikosea serikali na amejipanga kufungua na duka ili watu wake waweze kupata kwa urahisi.
“AK ni Brand ya Alikiba nashukuru imekuwa kubwa watu wanavaa lakini pia ipo na ya King Kiba nayo ni brand yangu na zipo official kabisa na kazi zitakapoanza watapata product zote’ – Alikiba
“Kuna Malengo makubwa sana tumeyaweka lakini siwezi kusema sasa hivi ila kuna Jeans Viatu na Glasses tayari zishatoka soon wataziona maana hizi zitakuwa za kwanza sababu tayari zishatoka na kuna energy drink” – Alikiba

KIMENUKA BUNGENI: SIRI NZITO YAFICHUKA KITWANGA AFUNGUKA MAZITO YA BASHITE NA SERIKALI YA MAGUFULI..



Mbunge wa Misungwi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi katika serikali ya awamu ya tano, Charles Kitwanga ameijia juu serikali na kusema kuwa inamhujumu ili apoteze jimbo katika uchaguzi ujao kwa kuamua kutokupeleka maji jimboni kwake.

Kitwanga alisema kuwa serikali imeamua kutokupeleka maji jimboni Misungwi kwa sababu wanamuandaa mtu anayeitwa Bashite kwenda kugombea katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.

Kitwanga aliyasema hayo jana bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambapo Waziri Mhandisi Gerson Lwenge aliliomba Bunge kuidhinisha TZS bilioni 672.2 kwa ajili ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Akichangia hotuba hiyo, Kitwanga alieleza hali ngumu ya upatikanaji wa maji wanayopitia wakazi wa kijiji cha Kolomije ambapo ndipo alipozaliwa Bashite.

Kuonyesha kukerwa na serikali kupuuza kupeleka mradi wa maji jimboni humo, Kitwanga alisema kuwa atahamasisha wananchi wa Misungwi kwenda kuzima mitambo ya maji ambayo ipo katika Kijiji cha Ihelele anachodai kuwa kimesahaulika katika miradi ya maji iliyopangwa kwenye bajeti ya 2017/28.

Kitwanga alisema kuwa wakati alipokuwa waziri alikuwa anashindwa kuibana serikali lakini kwa vile sasa ni mbunge tu, basi patachimbika.

Very unfair (si haki), nazungumza kutoka moyoni mwangu, haiwezekani mradi unakwenda Tabora unatumia 600 bilioni alafu watu wangu wanakosa maji hata ya bilioni 10, alisema Kitwanga
Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top