Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

GOLI LA STERLING LAMPA WAKATI MGUMU BALOTELLI, APOROMOSHEWA MATUSI NA MASHABIKI...

Balotelli Atukanwa Na Mashabiki Wa Liverpool

Mshambuliaji kutoka nchini Italia na klabu ya Liverpool, Mario Balotelli usiku wa kuamkia hii leo, alikua na wakati mgumu baada ya kumpongeza mshambuliaji mpya wa klabu ya Man City, Raheem Sterling.

Balotelli, alijikuta akiporomoshewa matusi na mashabiki wa klabu ya Liverpool kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, kutokana na kuonyesha kufurahishwa na kilichofanywa na Sterling katika siku yake ya kwanza ya kuitumikia klabu ya Manchester City kwa kufunga bao.

Balotelli aliandika katika mtandao wa Twitter: “Hongera @sterling31 ! naona umewajibu, ongeza bidii.”

Ujumbe huo uliwakera mno mashabiki wa klabu ya Liverpool ambao hawakupendezwa na mpango wa Sterling kuondoka Anfield, kwa kumtukana na wengine kufika mbali kwa kuutaka uongozi kumuondoa Balotelli kikosini mwao na ikiwezekana kumuuza kabisa.



Sterling aliondoka Liverpool juma lililopita baada ya kushinikiza kwa kipindi cha siku kadhaa, kutaka kujiunga na klabu ya Man Citya mbayo ilikubali kutoa kiasi cha paund million 49, kama ada yake ya usajili.

Katika mchezo wa jana Man City walikua wakipambana na As Roma katika mchezo wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi na matokeo ya mchezo huo ni kwamba klabu hiyo ya Etihad Stadium iliibuka kinara kwa ushindi wa penati 5-4, baada ya kulazimishwa sare ya mabao mawili kwa mawili.







Sehemu ya ujumbe uliokua unajibiwa na mashabiki wa Liverpool kwa Balotelli.







Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top