Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KIMENUKA HUKO; VIGOGO WA SIMBA NA YANGA WAPARANGANA BAADA YA TIMU ZAO KUGONGANA HUKO GOR MAHIANA KUPEWA ONYO KALI

Mshambuliaji Michael Olunga.
Nicodemus Jonas,  Dar es Salaam
JEURI ya fedha za usajili kwa timu kongwe za Tanzania, Simba na Yanga kwa kuweza kumsainisha mchezaji yeyote wakati wowote huenda ikawaweka pabaya, hiyo ni baada ya uongozi wa Gor Mahia kutoa onyo kwa vigogo hao juu ya wachezaji wao wawili.

Kipa Boniphace Oluoch pamoja na mshambuliaji Michael Olunga wamekuwa gumzo kubwa kwenye michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea jijini Dar, huku Olunga akijikuta kwenye rada za Yanga na Simba ambazo hivi karibuni zilijikuta zikigongana kwenye kambi ya Gor Mahia, usiku.

Katibu Mkuu wa Gor Mahia, David Kilo katika mahojiano maalum na Championi Ijumaa, amefunguka mkasa mzima wa kuvamiwa, lakini akasema: “Hawampati ng’o.

“Baada ya mechi yetu na Yanga (Jumamosi), walikuja viongozi walijitambulisha kuwa ni wa Simba wakisema kuwa wanataka tuongee dili kuhusu Olunga na Oluoch. Sikuwajua kwa majina na bahati mbaya tulikuwa hatujaweka utaratibu wa wageni wetu kuandika majina yao pale mapokezi.

“Kesho yake kuna jamaa alikuja anasema ni kiongozi wa Yanga akisema ikiwezekana tufanye dili la Olunga.
“Kwanza hatukutaka kumsikiliza, tukamwambia akili zote kwa sasa zipo kwenye michuano, maana vitu kama hivi vinasababisha wachezaji wapungukiwe morali.

“Unajua Olunga ni mwanafunzi, anachukua Shahada ya Uhandisi Chuo Kikuu Nairobi, kwa hiyo haiwezekani akasitishe masomo kipindi hiki.”

Aliongeza: “Walipokuja ishu kubwa walisema wanataka wachezaji wawili; Olunga na Oluoch, sisi hatukatai kuuza wachezaji lakini hiki siyo kipindi chake. Wasubiri hadi usajili kwetu utakapoanza, vinginevyo wakithubutu kumfuata kwa sasa na tukapata ushahidi, tuna haki ya kufuata sheria.” Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amethibitisha mara kadhaa kuwahitaji nyota hao.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top