Askari wa JKT wakitoka nje ya uwanja baada ya kumaliza mazoezi.
Askari wa kikosi maalum kutoka Magereza wakitoka nje ya uwanja baada ya kumaliza maandalizi.
KATIKA kuelekea kwenye tukio muhimu la kuwakumbuka maofisa na wapiganaji wa vita Tanzania ambalo hufanyika kila mwaka ifikapo Julai 25, maandalizi yamekamilika ambapo leo baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa katika mazoezi ya mwisho ndani ya Viwanja vya Mashujaa, Mnazi Mmoja jijini Dar.
Maadhimisho hayo ya siku ya mashujaa yanatarajiwa kupambwa na matukio mbalimbali ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dokta Jakaya Mrisho kikwete ambaye itakuwa ni mara yake ya mwisho kuhudhuria tukio la namna hiyo akiwa madarakani.
Pia sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuiriwa na wazee mashuhuri waliopigana vita. Wageni wengine ni mabalozi kutoka nchi mbalimbali.
Pichani juu ni baadhi ya vyombo vya usalama nchini vikifanya maandalizi ya mwisho.


Post a Comment