Mhe. Freeman Mbowe (katikati) kulia kwake ni Regina Lowassa (mke wa Lowassa) na kushoto kwake ni Edward Lowassa baada ya kukabidhiwa kadi cha Chadema.
Mhe. Freeman Mbowe (katikati) kulia kwake ni Regina Lowassa (mke wa Lowassa) na kushoto kwake ni Edward Lowassa baada ya kukabidhiwa kadi cha Chadema.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akimpongeza Edward Lowassa punde baada ya kujiunga na CHADEMA chama kimojawapo kinachounda umoja wa UKAWA.
Mke wa Edward Lowassa, Regina Lowassa akikabidhiwa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba akimpongeza Mhe. Edward Lowassa baada ya kujiunga na CHADEMA chama kimojawapo kinachounda umoja wa UKAWA.
Mkutano ukiendelea.
WAZIRI Mkuu wa zamani, Mhe. Edward Lowassa ametangaza rasmi kuondoka CCM na kujiunga rasmi na UKAWA kupitia Chadema baada ya kutafakari kwa kina akiwa katika mkutano wa chama hicho uliofanyika Bahari Beach jijini Dar es Salaam leo.
Mhe. Lowassa pamoja na mkewe, Bi. Regina Lowassa wamekabidhiwa kadi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka kwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Lowassa akitoa hotuba fupi katika mkutano huo amesema hausiki kwa lolote na skendo ya Richmond na kama kuna mtu mwenye ushahidi apeleke mahakamani, asema yeye alishauri kwa nafasi yake lakini maamuzi yalitoka ngazi za juu.
Mhe. Lowassa ameongeza kuwa hakutendewa haki katika mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM maana alipuuzwa, hakusikizwa, katiba haikuzingatiwa huku mkachakto huo ukiwagubikwa na mizengwe na chuki dhidi yake.
Aidha ameongeza kuwa CCM siyo mama yake wala baba yake na atakuwa mnafiki kama akiendelea kuwa ndani ya chama hicho.
Pia ameongeza kuwa hakuchukua maamuzi hayo kwa kupaniki, amejiridisha kuwa ndani ya UKAWA watashinda katika uchaguzi ujao huku akiwashukuru viongozi wa UKAWA kwa mualiko wao.


Post a Comment