Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Wananchi hawana huruma na waharifu...Aliyetaka kuua kwa panga, auawa kinyama



Na Gregory Nyankaira, Butiama
BULEMO Mugeta (36),  (pichani) mkazi wa Kitongoji cha Kibisa, Kijiji cha Nyamisisi Wilaya ya Butiama, ameuawa kinyama kwa kupondwa na mawe na kupasuliwa kichwa na wananchi wenye hasira kali akituhumiwa kujihusisha na matukio kadhaa ya wizi
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea Julai 17, mwaka huu majira ya saa 1 usiku katika kijiji hicho wamesema kwamba, Bulemo aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba na wananchi kutokana na matukio ya uvamizi na uporaji, alikamatwa akiwa na panga akijaribu kumshambulia mkazi mmoja wa Kijiji cha Singu, Maginga Buseri akimtuhumu mkazi huyo kuwa anamtangazia kwa watu kuwa ni mwizi na jambazi.
Aidha, mashuhuda hao wameeleza kuwa, wakati Bulemo akijiandaa kumshambulia Buseri kwa panga, wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo walipiga mayowe yaliyosababisha umati mkubwa kufika katika eneo hilo na kujichukulia sheria mkononi kwa kumpiga mawe kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.
Shuhuda mmoja wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alilieleza Uwazi kwamba, Bulemo alikuwa akidaiwa kushiriki kwenye matukio ya uvunjaji nyumba na vibanda vya maduka maeneo tofauti wilayani Butiama akiwa na kundi lake la uhalifu.
“Anahusishwa na matukio mengi tu ya kihalifu na kupora vitu likiwemo tukio la hivi karibuni lililotokea katika Kijiji cha Singu ambapo kundi hilo lililokuwa likiongozwa na Bulemo lilidaiwa kuvamia nyumbani kwa mama mmoja mkazi wa kijiji hicho na kupora begi lililokuwa na fedha shilingi milioni 2.5,” alisema shuhuda huyo.
Polisi wa Kituo cha Kiabakari wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa hakuna mtu yeyote aliyehusika kujichukulia sheria mkononi na kumuua Bulemo aliyekamatwa, msako unaendelea.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top