Waandishi wa habari wamejaribu kumuulza Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya kuhusu kile alichotaka kukizungumza mwenyekiti wao, Prof. Lipumba lakini Sakaya kwa amewajibu kuwa wao hawajui kitu alichotaka kuwaambia wananchi.
Sakaya amesema kuwa, sababu kubwa ya kusitishwa mkutano huo ni wazee wa CUF wametaka kujua kwanza ni kitu gani Mwenyekiti anataka kuongea.
Sakaya amesema kuwa, sababu kubwa ya kusitishwa mkutano huo ni wazee wa CUF wametaka kujua kwanza ni kitu gani Mwenyekiti anataka kuongea.
Wananchi nje ya ofisi za CUF wameshangilia wakiimba kwa kusema ‘Si mnaona, muziki wa Lipumba kuuzima hamuwezi’
Mmoja wa wananchi wanaoshangilia amesema wamefurahia kwakuwa wanaamini Mwenyekiti wao Lipumba hajiuzulu na yuko pamoja na wananchi.
Mmoja wa wananchi wanaoshangilia amesema wamefurahia kwakuwa wanaamini Mwenyekiti wao Lipumba hajiuzulu na yuko pamoja na wananchi.
Wananchi mbalimbali wanaoshangilia wanasema wanamuamini Lipumba na dalili iliyopo ni kuwa hawezi kujiuzulu maana anawasikiliza na ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CUF.
Wapambe na mashabiki wa chama hicho mpaka sasa wamejazana nje ya ofisi kuu za chama hicho, wakiimba nyimbo za kumsifu Lipumba ambaye baadhi ya vyombo vya habari leo vimeripoti kwamba Prof Lipumba ametofautiana na maamuzi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Shariff Hamad juu ya ushiriki wa Chama hicho katika UKAWA.

Post a Comment