Emeka Ezeugo (Abdul-Salam Bilal) huyu ni kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria yeye alibadilisha dini mwaka 2012 baada ya kuvutiwa na maisha aliyoishi mtume Mohammad.
Eric Abdali (Bilal) mchezaji wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya Ufaransa yeye alibadilisha dini kutoka Katoliki mwaka 2007 baada ya kuoana na binti wa kiislam Hayet Kebir
Frank Ribery (Bilal) yeye alibadilisha dini mwaka 2002 baada ya kuamua kufunga ndoa na mke wake Wahiba Belham
Mchezaji raia wa Togo anayechezea klabu ya Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Togo Emmanuel Adebayor hivi karibuni aliweka video kwenye mtandao wa Youtube ikiwa na maneno ya kumshukuru mungu pia akiwa amevalia Kiislam.
Kutokana na video hiyo inaaminika kuwa mchezaji huyo amehamua kujiunga na dini hiyo.
Thierry Henry mchezaji huyu wa zamani wa timu ya taifa ya ufaransa yeye aliwahi kusema anaipenda sana dini ya kiislam na mara nyingi henry upenda kutumia ishara za kiislam wakati anapokuwa anaomba sala pia marafiki zake wengi ni waislamu.
Van Persie huyu ni nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce, mchezaji huyu aliwahi kusema kuwa yeye ni muumini wa dini ya kiislam au kikristo ingawa amemuoa binti wa kiislam kutoka Morocco Bouchra
Blum huyu ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani yeye alitangaza rasmi kujiunga katika dini ya Kiislam januari mwaka huu.
Nicolaus Anelka huyu kwasasa ni kocha mkuu wa kikosi cha Mumbai city yeye alibadilisha dini mwaka 2004 na kupewa jina la Abdul-Salam Bilal.


Post a Comment