Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Mgosi: Msiogope njooni Taifa muone kazi

musa-hassan-mgosiIbrahim Mussa, Dar es Salaam
SIMBA leo inacheza mechi ya kirafiki dhidi ya SC Villa ya Uganda katika maadhimisho ya Tamasha la Simba Day kwenye Uwanja wa Taifa Dar, straika wa timu hiyo Mussa Mgosi amesema wamejipanga kutowaangusha mashabiki wao.
Mgosi aliliambia Championi Jumamosi kuwa, kwa kambi mbili walizopiga Lushoto, Tanga na Zanzibar hivi karibuni kikosi chao kimebadilika na sasa kina uwezo wa kuitetemesha timu yoyote.
Mgosi alisema atahakikisha anashirikiana vizuri na wenzake ili Simba ishinde kufuta dhana ya kufanya vibaya katika mechi za timu hiyo katika Simba Day.
“Binafsi naona maandalizi yameenda vizuri kuanzia katika kambi ya Lushoto na hata Zanzibar kwa sababu tumecheza mechi za kirafiki za kutosha, naamini kuwa zimetujenga vya kutosha,” alisema Mgosi.
“Nawaomba mashabiki waje kwa wingi kuiangalia timu yao maana tunafahamu kuwa ni kipindi kirefu hawajaiona na haitakuwa vizuri tukipoteza mbele yao, hivyo tutapambana ili tushinde.”

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top