Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

MPYA ...CLUB YA YANGA IMESHUSHA VIFAA VIPYA KUTOKA AL -KHARTOUM

Wilbert Molandi na Hans Mloli
YANGA imeondolewa katika michuano ya Kombe la Kagame ambayo kesho itapigwa mechi ya fainali, kocha wa timu hiyo Hans van Der Pluijm ameona tatizo lipo kwa kiungo mkabaji na tayari amemtaja kiungo wa Al Khartoum ya Sudan, Anthony Akumu kuwa lazima amsajili.
Kocha huyo, hivi karibuni alitoa mapendekezo ya kumsajili kiungo mmoja mkabaji mwenye uwezo mkubwa kwenye kikosi chake kinachojiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Jina la Akumu limekuja baada ya harakati za kumnasa kiungo wa APR, Yanick Mukunzi kuonekana kuwa ngumu huku yule ya Gor Mahia, Khalid Aucho, mazungumzo yakiendelea.
Akizungumza na Championi Jumamosi,
Pluijm alisema ni ngumu kutamka moja kwa moja kama atamsajili kiungo huyo, lakini amemtaja Mkenya huyo kuwa ni kati ya wachezaji wanaostahili kuichezea Yanga.
Pluijm alisema kiungo huyo ana uwezo wa kupiga pasi fupi na ndefu, pia ni makini kwenye ukabaji, nafasi hiyo ya kiungo namba sita huchezwa na Mbuyu Twite na Salum Telela ambao bila shaka itabidi wasogee mbele au watafutiwe nafasi nyingine.
Aliongeza kuwa, kiungo mwingine mkabaji ambaye alimuona na kuridhishwa na kiwango chake ni Aucho pekee, japokuwa Championi Jumamosi linafahamu viongozi pia wanamnyemelea Mukunzi wa APR.
“Kwenye kikosi changu anahitajika kiungo mkabaji pekee mwenye uwezo mkubwa wa kukaba wakati huohuo akipiga pasi fupi na ndefu,” alisema Pluijm ambaye sasa ana kiungo mkabaji Said Makapu pekee ambaye ni majeruhi wa mgongo na hakucheza Kombe la Kagame.
“Kama viungo wachezeshaji na washambuliaji ninao Niyonzima (Haruna), Kaseke (Deus), Msuva (Simon), Mwashiuya Geofrey) na Telela hao wanatosha,” alisema Pluijm, raia wa Uholanzi.
“Hivyo hapa nimepanga kumuongeza mmoja kati ya Akumu au Aucho au wote kwa pamoja itategemea na mazingira,” alisema Pluijm.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top