Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote yaani Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 1 Julai 2015.
Kwa Mwezi Agosti 2015, bei za rejareja kwa Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kama ifuatavyo: TZS 18/lita sawa na asilimia 0.86 na TZS 29/Lita sawa na asilimia1.47 sawia, na kwa mafuta ya Petroli bei imeongezaka kwa TZS 92 /lita sawa na asilimia 4.19.
Vilevile kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla kwa mafuta ya Dizeli na Mafuta ya Taa nazo zimepungua kama ifuatavyo: TZS 17.50/lita sawa na asilimia 0.90 na TZS 29.27/lita sawa na asilimia 1.55 sawia na kwa mafuta ya Petroli bei imeongezeka kwa TZS 92.07/lita sawa na asilimia 4.40. Mabadiliko haya yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia.


Post a Comment