Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

CHADEMA YAMVAMIA "ANNA KILANGO" HUKO SAME MKOANI KILIMANJARO, ANGALIA KILICHOTOKEA


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Jimbo la Same mkoani Kilimanjaro, kimewataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua Naghenjwa Kaboyoka, ili awaletee maendeleo ikiwamo kuboresha huduma za afya na miundombinu ya barabara.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo juzi, Katibu wa chama hicho mkoani Kilimanjaro, Basil Lema, alisema kuwa wananchi wa jimbo hilo wanapaswa kumchagua mtu atakayewaletea maendeleo na ambaye ni muibuaji wa miradi na muendelezaji badala ya kuchagua mtu asiyekuwa na shukrani kwao.
 
Alifafanua kuwa kwa kipindi kirefu, Kaboyoka amekuwa akiwasaidia akina mama kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwamo sekta ya afya pamoja na kutoa tope lililopo katika ziwa kilomeni ambalo ni tegemeo kubwa kwa wananchi wa jimbo hilo.
 
Akihutubia wakazi wa kata ya Miamba, mgombea ubunge huyo aliwataka wananchi hao kumchagua ili awaletee maendeleo huku akieleza vipaumbele vyake kuwa ni pamoja na elimu, afya na uchumi.
 
 
 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top