Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI YA HIVI PUNDE:..AJALI MBAYA YAUA WATU WAWILI NA KUJERUHI 15 HUKO LUSHOTO

Watu wawili wamefariki dunia na wengine 15  kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Longoi Kata ya Mtae wilayani Lushoto jana majira ya saa 11.00 jioni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji alisema leo kuwa ajali hiyo imelihusisha gari la Kampuni ya Shambalai ambalo lilikuwa likifanya safari zake kutoka Dar es salaam kuelekea Mtae ambapo lilipinduka na  kuingia kwenye korongo.

Kamanda Mwombeji amesema abiria waliofariki katika ajali hiyo miili yaoimeshatambulliwa ambapo mmoja ni mkazi wa Mtae na mwingine ni mkazi wa Vuli.

Aidha Kamanda Mwombeji alieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika ila ubovu wa barabara pia unaweza kuwa umechangia kwa ajali hiyo.

Majeruhi wa ajali hiyo akiwemo dereva wa basi hilo, Sadiki Ayoub mkazi wa Mlalo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa matibabu zaidi na hadi leo hali zao zinaendelea vizuri huku wengine wakipewa ruhusa.


Ingawa dereva wa basi hilo amejeruhiwa katika ajali hiyo lakini yupo chini ya uangalizi wa jeshi la polisi kwa ajili ya kuhojiwa zaidi kutokana na tukio hilo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top