Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KILIO...MKUU WA WILAYA HUKO ZANZIBAR AMEFARIKI DUNIA NA KUZIKWA JANA

Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Nd. Jabu Khamis Mbwana aliyefariki Dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mfupi amezikwa Kijiji kwao Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Marehemu Jabu Khamis Mbwana alikuwa akisumbuliwa na homa kwa takriban wiki moja iliyopita.



Umati Mkubwa wa Wananchi, waumini wa Dini ya Kiislamu, Viongozi wa Kiserikali pamoja na Vyama vya Siasa wakijumuika pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi walihudhuria mazishi ya
Kiongozi huyo aliyekuwa na Fani ya Tasnia ya Habari.



Marehemu Jabu Khamis Mbwana alizaliwa mwaka 1958 na kupata elimu ya msingi katika skuli ya Kiuyu Mbuyuni na baadaye elimu ya Sekondari katika Skuli ya Fidel Castrol Chake chake Pemba.



Alijiunga na mafunzo ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Habari Tanzania           { TSJ } na kupata Stashahada ya fani hiyo mwaka 1984 ambapo aliajiriwa kazi ya Afisa wa Habari Wilaya ya Micheweni.



Marehemu Jabu KhaMIS Mbwana Aliamua kuingia katika ulingo wa Siasa na kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Vipindi viwili kuanzia kwamba 1985 hadi mwaka 1995.



Utumishi wake makini uliozingatia maadili na nidhamu kwa Jamii ulimuwezesha kuteuliwa kuwa Afisa Tawala wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba mwaka 1996.



Mwaka 2006 Marehemu Jabu Khamis Mbwana aliteuliwa na Rais wa Zanzibar kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chake chake, Wilaya ya Mkoani na hadi kufariki kwake alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni.



Nd. Jabu alikuwa Mfanyakazi hodari, shupavu, aliyejiamini katika utumishi wake na mwenye mashirikiano na watendaji wenzake wa Serikali na alimthamini kila mtu katika Uongozi wake.



Akiwasilisha salamu za Rais wa Zanzibar  kwenye maziko hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba  Dr. Ali Mohammed Shein amepokea kwa mshituko taarifa ya Kifo cha Msaidizi wake
katika Wilaya ya Micheweni Nd. Jabu Khamis Mbwana.



Alisema kifo hicho hakikuacha pengo wala msiba kwa familia pekee bali kwa Taifa zima jamii ikikumbuka ushupavu wa ndugu Jabu wakati wa uhai wake katika kusimamia haki na uadilifu.



Balozi Seif aliyepokea simu kutoka kwa Rais wa Zanzibar muda huo wa mazishi aliitaka familia ya marehemu pamoja na marafiki kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi kifupi cha msiba.au kukinga jambo hilo. Na hivyo ndivyo wajibu huo ulivyomkuta Ndugu Jabu Khamis Mbwana.


Mauti yanakata starehe ya Dunia, hayana kinga  na kamwe hayazoeleki jambo linaloiwajibikia kila nafsi kujiandaa na haki hiyo.



Marehemu Jabu Khamis Mbwana  ameacha familia ya vizuka Watatu na watoto 17. Mwenyezi Muungu ampe safari njema Marehemu  Jabu. Amin.

  WAUMINI mbali mbali wa Dini ya Kiislamu wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, wakimswalia Marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, swala iliyofanyika huko kijijini kwao Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni Ksiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)

 WANANCHI mbali mbali Kisiwani Pemba wakiwa wameubeba mwili wa Marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, kuupeleka kwenye makaazi yake ya Mwisho huko kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)
 MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akishuhudia mazishi ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Kisiwani Pemba, Mhe:Jabu Khamis Mbwana marehemu alifariki dunia jana na kuzikwa huko kijijini kwao Kiuyu Mbuyuni Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)
 MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akitia mchanga kwenye kaburi la Marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, aliyefariki duania jana na kuzikwa kijijini kwao Kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)
 MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akiitikia dua mara baada ya kumalizika kwa mazishi ya Marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, aliyefariki dunia jana na kuzikwa kijijini kwao Kiuyu Mbuyuni Kisiwani Pemba.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)
MAKAMO wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akikabidhi ubani kwa mmoja wa vizuka wa marehemu Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mhe:Jabu Khamis Mbwana, aliyefariki dunia na kuzikwa kijijini kwao kiuyu Mbuyuni Kisiwani Pemba. .(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top