Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KOCHA WA TOTTENHAM AMTIMUA ADEBAYOR NA KUKATAA ASICHEZEE TENA SPURS

Emmanuel-AdebayorKocha wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino amethibitisha kuwa mshambuliaji raia wa Togo Emmanuel Adebayor hatacheichezea tena klabu hiyo ingawa bado ataendelea kupokea mshahara wake wa pauni laki moja kwa juma kadiri ya mkataba wake.
Adebayor mwenye miaka 31 amebakiza msimu mmoja katika mkataba wake ataendelea kupokea mshahara wake huo lakini hayupo katika mipango ya mwalimu Mauricio Pochettino.
Hali hiyo imekuja mara baada ya Adebayor kukataa siku za mwisho za usajili kuhamia klabu ya West Ham kwa ada ya pauni 5m huku akiwa hayupo katika mipango ya kocha.
Pochettino amesema; “kila kitu kipo wazi, tushafanya mazungumzo nae na sina haja ya kuyarudia tena. Hayupo katika mipango yangu na yeye analijua hilo”.
Pochettino pia alimshangaa Adebayor baada ya mshambuliaji huyo kukataa kujiunga na timu ya taifa lake alipoitwa wiki iliyopita katika kalenda ya FIFA.
Kocha huyo anasema kilichopo sasa ni kuangalia uwezekano wa kuweka sawa ilimradi pande zote mbili zinufaike. Anasema wanapishana katika korido lakini hilo halina tatizo kwa maana Adebayor anajua kila kitu.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top