Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

MTANZANIA ALIYEWAHI KUIFUNGA BRAZIL AFUNGUKA KUHUSU NDONDO CUP

Jabir Aziz, kiungo wa Mwadui FC ya Shinyanga
Jabir Aziz, kiungo wa Mwadui FC ya Shinyanga
Mchezaji pekee wa Tanzania aliyewahi kufunga goli dhidi ya mabingwa wa kihistoria wa kombe la dunia, timu ya Brazil amefunguka mengi juu ya michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup iliyohitimishwa jana ambapo timu ya Faru Jeuri iliibuka bingwa wa michuano hiyo kwa kuifunga timu ya Kauzu FC kwa mikwaju ya penati na kutwaa ubingwa huo.
Jabir Aziz Stima, kiungo wa Mwadui FC ya Shinyanga alifanya mazungumzo mafupi na mtandao huu wakati michuano ya Ndondo Cup inaendelea na kusema mambo mengi juu ya michuano hiyo ambayo yeye amesema anaiheshimu sana kwani ndiko alikotokea na kufahamika kwenye ramani ya soka la Tanzania.
“Michuano hii inadharauliwa sana watu wasiojua soka, mchezaji wa ligi kuu akija kucheza huku anaonekana wa ajabu sana kwamba hajithamini au anajishushia hadhi yake kumbe ni tofauti na wanavyofikiria wao”.
“Mimi nimecheza sana Ndondo na huku ndko mimi nilipotoka hadi watu wanakuja kunijua baadae. Wakati nacheza Ndondo nilikuwa nacheza kwenye timu ya Friends Rangers pamoja na Sure Boy na wachezaji wengine kibao wenye majina makubwa leo hii lakini watu hawajui hilo”.
“Kwahiyo mtu anapoamua kuja kucheza Ndondo ni sawa na kurejea nyumbani na kuja kuwasapoti watu wake wa kitambo ambao walicheza pamoja. Huku sisi ni nyumbani na kamwe hatuwezi kupakana kwasababu ndipo tulipotokea, hivyo watu wakituona huku wasitushangae ni kawaida”.
“Halafu wakati mwingine ligi inapokuwa kwenye mapumziko kila mtu anakuwa kwake kwahiyo sisi huwa tunarudi huku mchangani kufanya mazoezi na jamaa zetu hawa ambao wako chini huku”.
Katika hatua nyingine, mkali huyo wa zamani wa Azam FC amesema michuano hiyo kwasasa imepanda hadhi kwani watu wametambua umuhimu wake na kuanza kuidhamini huku akiamini kuwa, baadae michuano hiyo itakuwa mikubwa zaidi ya ilivyo sasa huku akiifananisha na ile ya FA.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top