Ule mtanange uliokuwa unasubiriwa kwa hamu baina ya wapinzania wa jadi wa ligi kuu ya Uingereza, vilabu vya Manchester United dhidi ya Liverpool umepigwa usiku huu.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Old Trafford umemalizika kwa Mashetani wekundu kuendeleza ubabe dhidi ya Liverpool kwa mara ya tatu mfululizo.
Daley Blind alianza kuifungia United goli la kwanza muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza, kabla ya Ander Herrera kufunga la pili kupitia mkwaju wa penati.
Christian Benteke aliifungia Liverpool goli la kufutia machozi kwa mtindo wa ‘tik tak’ mwishoni mwa kipindi cha pili kabla ya mshambuliaji mpya wa Man United – Anthony Martial kufunga goli la 3 kwa United.
Baada ya mchezo wa mchana kati ya Chelsea vs Everton, Barclays Premier League imeendelea kutimua vumbi kwenye viwanja tofauti nchini Uingereza.
Arsenal wakiwa nyumbani waliikaribisha timu ngumu ya Stoke City- mechi ambayo imemalizika kwa vijana wa Arsene Wenger kupata ushindi wa 2-0.
Magoli ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott na Oliver Giroud.


Post a Comment