Ikicheza mechi yake ya pili ya ligi Simba SC imeifunga Mgambo JKT ya Tanga kwa magoli 2 – 0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Goli la kwanza la Simba lilipatikana kwenye dakika ya 27 kipindi cha kwanza ambapo lilifungwa na mchezaji wa kimataifa Justice Majbvi, katika kipindi cha pili dakika ya 73 ya mchezo Simba ilipata goli la pili kupitia mshambuliaji wake wa kimataifa Hamis Kizza na hivyo kufanya matokeo mpaka mpira unakwisha kuwa Simba 2 – 0 Mgambo.
Akizungumza na Simbasports.co.tz baada ya mechi nahodha msaidizi wa kikosi cha Simba Hassan Isihaka ambaye alikuwa nahodha wa mechi hiyo baada ya nahodha wa timu ya Simba Musa Hassan Mgosi kutoka na kumpisha Ibrahimu Ajibu alisema “tunafurahi sana kupata ushindi wetu wa pili kwenye uwanja wa Mkwakwani ugenini, huu ni mwanzo mzuri na tunategemea timu yetu itafnaya vizuri kwenye mechi nyingine zinazofuata kwenye msimu huu mpya wa ligi kuu ya Vodacom.
Simba leo iliwakilishwa na
- Peter Manyika
2. Mohamed Hussen
3. Hassan Kessy
4. Murushid Juuko
5. Hassan Isihaka
6. Justice Majabvi
7. Awadh Juma
8. Said Hamisi Ndemla / Pape Ndaw
9. Mussa Hassan Mgosi / Ibrahim Ajibu
10.Mwinyi Kazimoto / Hamis Kizza
11.Peter Mwalyanzi


Post a Comment