Diwani wa kata ya Mtambani wilayani Kibaha mkoani Pwani, Godfrey Mwafulilwa(CCM) ameitaka Halmashauri ya wilaya hiyo kuondoa changamoto zinazokwamisha maendeleo kwa kutenga maeneo ya biashara na kusimamia miundombinu ya mashamba. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).
Kata hiyo iliyopo katika mji mdogo wa Mlandizi ni moja ya kata zilizopo ndani ya kata 14 za Jimbo la Kibaha vijijini, kata 14, zikiwemo Magindu, Kwala, Ruvu Station, Kikongo, Mlandizi, Mtambani, Janga, Mtongani, Kilangalanga, Kawawa, Dutumi, Soga.
Akizungumza na Mwanahalisi Online kuhusu changamoto za maendeleo katika kata yake, diwani huyo amesema kuwa vikwazo vinavyokumba kata hiyo ni miongoni mwa mifano tosha ya marekebisho ya miundondombinu yanayopaswa kufanyika katika jimbo la Kibaha vijijini.
Mwafulilwa amesema kuwa “hizo ni baadhi ya sababu zinazopelekea mji huo kukwama kimaendeleo ambazo ni vyema kushughulikiwa mapema kwasababu ndio misingi muhimu katika upatikanaji wa maisha bora ya jimbo pamoja na kata zake.” alisema
Alibainisha kuwa wafanyabishara wengi wanakwamishwa pia na kodi za majengo ya fremu za maduka kwa kuwa Mamlaka ya Mapato (TRA) wameweka kiasi kikubwa cha fedha kwa wananchi kulipia hivyo kushindwa kulipa na kufunga biashara zao.
Aliongeza kuwa “Katika suala la ulipaji wa kodi, wafanyabiashara wanaotumia fremu wanakimbia kulipa kodi kutokana na kuongezeka kwa bei ya kodi hiyo jambo linalopelekea halmashauri kukosa kiasi kikubwa cha mapato hivyo ni vyema kupunguzziwa kodi kwa wafanyabiashara hao”
Mwafulilwa aliweka bayana kuwa watu wengi ukwepa kodi kutokana na TRA kuongeza kodi za fremu na kama TRA wakipunguza kiasi cha kodi ndivyo idadi ya walipa kodi taongezeka.
Aidha kuhusu Kilimo Mwafulilwa ameiambia MwanaHALISI Online kuwa mashamba yaliyoko Ruvu kwa Dosa, pembeni kidogo mwa mji wa mlandizi. hayawanufaishi wakazi wa Mlandizi kutokana na utokuwepo kwa miundombinu salama ya kilimo inayopelekea kupoteza nguvu na hatimae kukata tamaa ya kulima.
Amesema kuwa wakulima waishio maeneo ya karibu na mashamba hayo wanalima kwa kumtegemea mungu yaani “hawana uhakika wa kufaidi matunda ya kilimo chao” kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu ya na uhakika ya kuzuia maji hasa wakati wa mvua.
Mwafulilwa amesema kuwa “Ni vyema viongozi tutambue kuwa wakulima na wanyabiashara ndio nguzo kubwa katika maendeleo ya nchi yetu hivyo tunapaswa kushughulikia hili katika uongozi wa huu wa awamu ya tano ikiwa ni moja ya mabadiliko.”
Post a Comment