Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI YA HIVI PUNDE: MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR (ZEC) "JECHA SALIM JECHA ATANGAZA RASMI TAREHE YA KURUDIA UCHAGUZI ZANZIBAR

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi visiwani humo baada ya matokeo ya uchaguzi uliopita kufutwa.
Uchaguzi huo sasa utafanyika Jumapili tarehe 20 Machi.
Tangazo hilo limefanywa na mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha.
Bw Jecha amesema tarehe hiyo iliamuliwa na tume baada ya mkutano hapo jana.
"Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni," amesema Bw Jecha.
"Wagombea wote walioteuliwa hapo awali wataendelea kuwa wagombea katika uchaguzi huu."
Chama cha Wananchi (CUF) kimekuwa kikipinga kurudiwa kwa uchaguzi. Chama hicho mapema mwezi huu kilionya kwamba hatua hiyo inaweza kusababisha vurugu.
Viongozi wa chama hicho walisusia maadhimisho ya Siku ya Mapinduzi wiki iliyopita.
Chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa tayari kimewashauri wanachama wake visiwani wajiandae kwa marudio ya uchaguzi, tangazo lililoshutumiwa vikali na viongozi wa CUF.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top