Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

CT-Scan ya Udom yapelekwa Muhimbili


Dodoma. Serikali imesema mashine ya CT-Scan iliyopelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ilichukuliwa kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangalla wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia aliyetaka kujua kuhusu mashine hiyo kuchukuliwa Dodoma wakati Serikali inasema ilinunuliwa.
“Kwanza naitaka Serikali ieleze ukweli, ni kwa nini wanasema kuwa walinunua mashine ya CT-Scan wakati ilichukua mashine hiyo Hospitali ya Ben Mkapa ya Udom na je mnataka wananchi wa mkoa huu wafe?” alihoji Nkamia.
Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kununua mashine mpya ya CT-Scan kwa ajili ya MHN.
Naibu waziri alisema Serikali ilipeleka mashine hiyo MNH ambayo inatumia teknolojia ya kisasa yenye X- ray tube 2 na uwezo wa kupiga picha ya 128 slice x 2 ili kusaidia kutoa huduma kwa wananchi.
“Faida ya mashine hii ni pamoja na kuhudumia mgonjwa kwa haraka na kutoa nafasi kwa mgonjwa mwingine, hali ambayo inatoa nafasi kwa wagonjwa wengi kupata kipimo hicho katika siku moja,”alisema Dk Kigwangalla.
Alisema mashine hiyo ina uwezo wa kuchunguza magonjwa yanayohusu moyo, mishipa ya damu, mishipa ya fahamu na ubongo.
Naibu waziri alisema ununuzi na usimikaji wa mashine hiyo, umesababisha Muhimbili kuwa na mashine mbili za CT-scan, hivyo Serikali haitegemei kama huduma zitasimama.
Kuhusu kuirudisha mashine hiyo Udom, alisema wanafanya mpango wa kununua nyingine na kuifunga.
Alisema waliichukua mashine hiyo na kuipeleka MNH kwa sababu jengo lililokuwa ifungwe bado halijakamilika.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top