Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Wasaliti waanza kuondolewa UVCCM

 Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema hauko tayari kusubiri kutumbuliwa majipu na Rais John Magufuli atakapokabidhiwa uenyekiti wa CCM hivyo wameanza wenyewe kujirekebisha kwa kuwaondoa wasaliti.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Hamasa, Sera na Mawasiliano wa umoja huo, Egla Mamoto, alisema msimamo wa umoja huo ni kuzisafisha njia zake kabla Rais Magufuli hajakabidhiwa uenyekiti wa CCM.
 
Mamoto alisema ndani ya umoja huo kuna wanachama waliokisaliti chama wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.
 
Katibu wa Hamasa, Sera na Mawasiliano, Mamoto alisema UVCCM itajisafisa ili kurudisha uadilifu ndani ya chama wakati wakijipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020.
 
Alisema lengo ni kuhakikisha wanawaondoa wasaliti ambao hawakitakii mema chama hicho katika uchaguzi ujao. 
 
Mamoto alimuahidi Rais Magufuli kuwa umoja huo utamsaidia kufichua wabadhirifu katika nyanja mbalimbali ikiwamo ndani ya UVCCM.
 
CHANZO: NIPASHE

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top