Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

JE KULINGANA NAHALI HALISI HII KATIKA MASHULE YETU TUNAWEZA KUTOA MAPROFESA???

Serikali imeombwa tena kuingilia kati suala la wanafunzi zaidi ya 800 kati ya 2600 wa shule mbili za msingi za Muheza na Masuguru zilizopo makao makuu ya wilaya ya Muheza kulazimika kukaa chini kwenye majanvi kutokana na kukabiliwa na uhaba wa madawati na vyoo hatua ambayo imesababisha baadhi yao kwenda kujisaidia vichakani na kuhatarisha afya zao.
Wakizungumza na ITV wilayani Muheza,walimu wakuu wa shule hizo Benard Luhanda mwalimu mkuu shule ya msingi Muheza na Hosea Mwansasu mwalimu mkuu shule ya msingi Masuguru wamesema jumla ya wanafunzi wote wapo 2600 lakini matundu ya vyoo ni 12 huku baadhi yao wakiwemo wa darasa la awali la sita na saba wanakaa chini katika majanvi na hivyo kusababisha kushindwa kusoma kwa ufanisi wanapokuwa darasani. 
 
Mkuu wa wilaya ya Muheza Esterina Kilasi akielezea mkakati huo amesema Serikali ipo katika mkakati wa kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi hata mmoja anakaa chini.
 
Kufuatia changamoto hiyo Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini imesaidia kupunguza changmoto hizo kwa kutoa msaada wa madawati 50 ili kuwapunguzia adha wanafunzi ya kukaa chini wakati wanapojisomea darasani.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top