Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Breaking News: KILIO KIKUBWA TAJIRI MKUBWA TZ DEWJI APATA PIGO ZITO MAGARI YAKE YACHOMWA MOTO


WATANZANIA nane madereva wa malori kutoka Kampuni ya Simba Logistics inayomilikiwa na mfanyabiashara Azim Dewji, wamekaa kwenye mikono ya majeshi ya waasi kwa saa 48 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Hiyo ni baada ya kutekwa juzi na kutarajiwa kuachiwa leo mchana baada ya juhudi za serikali na wasafirishaji.
Madereva hao ni kati ya 12 waliotekwa juzi asubuhi ambao wanne kati yao ni Raia wa Kenya, na walikuwa wamepeleka simenti kwenye mgodi wa Namoya uliopo nchini Kongo.
Rais wa Chama cha Wamiliki wa Malori (Tatoa), Angelina Ngalula aliliambia gazeti hili jana kwamba, baada ya kuwateka, waasi hao walitaka kila dereva alipiwe dola za Marekani 4,000 (Sh. milioni 8.7) kufikia jana saa 10 jioni vinginevyo wangewaua.
Jana jioni, Dewji aliliambia gazeti hili kwamba walifanya mawasiliano na waasi hao na kwamba madereva wote sasa wataachiwa leo asubuhi.
Alisema kwa mujibu wa makubaliano, madereva hao watakabidhiwa kwa kampuni ambayo Simba Logistics inafanya nayo biashara kwa upande wa Kongo.
Alisema malori yake yaliyochomwa yalikuwa yamebeba sementi na tathmini ya awali waliyoifanya amebaini kupata hasara ya Sh. bilioni 1.6.
MAJIVU
"Manne kati ya malori yangu yamebaki majivu tu. Na mengine manne yameungua nusu lakini yameharibika vibaya. Taarifa tulizozipata kutoka Kongo ni kwamba malori manne yaliyoungua nusu yamepelekwa kituo cha polisi Namoya,” Dewji alisema.
Rais wa Tatoa, Ngalula, aliliambia gazeti hili kwamba madereva hao walitekwa wakati wakirudi nchini baada ya kufikisha mizigo kwenye mgodi wa Namoya.
Aliwataja madereva waliotekwa kuwa ni Hamdan Harafi, Athuman Fadhili, Juma Zaulaya, Adam James, Issa Iddi Omary, Bakari Shomari, Hussein Mohamed Mwamu na Mbwana Twaha.
Alisema jumla ya madereva wote waliokuwa wametekwa ni 12, wakiwamo raia hao wa Kenya.
Alisema baada ya kutekwa na kupelekwa kwenye kambi ya waasi hao msituni, madereva wawili walitoroka mikononi mwa watekaji na kukimbia kisha kupiga simu Simba Logistics.
Alisema kwa sasa madereva waliotoroka wapo kweye mgodi ambako walipeleka mizigo kabla ya kutekwa.
Alisema baada ya kuyateka magari hao, waasi hao walichoma moto malori sita, manne kutoka Tanzania na mawili ya Kenya.
Ngalula alisema licha ya madereva hao kutekwa juzi asubuhi, taarifa zilifika Tanzania jioni ya siku hiyo kutoka kwa madereva wawili waliotekwa na kutoroka.
Awali Ngalula alisema Tatoa ilikutana ili kujadili namna ya kuzipata fedha hizo na kuzilipa kwa waasi kwa kuwa kikubwa zaidi ni kuokoa uhai wa madereva hao. Kauli ya Dewji ina maana pande hizo mbili zilimalizana.
“Kutoa hizo fedha inaweza isiwe tatizo lakini je zitafikishwa kwa hao waliowateka kweli, maana kilichopo sasa ni mawasiliano tu ya simu kutoka Congo," alisema Ngalula.
"Inawezekana fedha zikatolewa ili kuwagomboa baada ya siku kadhaa wakatekwa wengine (pia),” alisema Ngalula ambaye wakati huo alikuwa akisubiri ushauri kutoka serikali na ubalozi wa DRC nchini.
Ngalula alisema jana Tatoa na Dewji walifanya kikao na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kujadili suala hilo.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top