Aliyekuwa Mbunge wa Kasulu Mjini(2010-2015) kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Moses Machali ambaye alihamia ACT- Wazalendo, ameamua kujiunga na CCM.
Machali ameamua kufanya hivyo baada ya kueleza kuwa CCM ya Rais John Magufuli siyo ile ya 2015 na kurudi nyuma kidogo.
“Tuachane na siasa nyepesi za kutaka kuona kwamba mazuri ni yale yanayofanywa na wapinzani huku mambo hayohayo yakifanywa na CCM yaonekane hayafai na kutajwa kuwa ni ya hovyo. CCM ya JPM siyo ile ya 2015 kurudi nyuma kidogo. Hii ni tofauti na ninaiunga mkono.”
Machali ambaye aligombea Kasulu Mjini kwa tiketi ya ACT na kushindwa katika uchaguzi mkuu uliopita amesema kelele wanazopiga baadhi ya watu kwamba maisha yamekuwa magumu kwa sababu ya Magufuli ni propaganda tu kwa sababu hakuna uhusiano wa maisha magumu na suala la kudhibiti wapiga dili wa fedha na mali za umma.


Post a Comment