Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

BREAKING NEWS: MASIKINI MH LEMA NDIO BASI TENA YAMKUTA MAZITO MAHAKANI NI VILIO NA HUZUNI KUBWA SASA..


Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, Jaji Salma Maghimbi alimwamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kumfikisha Lema mahakamani hapo ndani ya nusu saa, baada ya kukaa mahabusu ya polisi kwa muda mrefu, kinyume cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
Wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, walilia kwa majonzi baada ya Lema kuamriwa na Hakimu Mkazi Desderi Kamugisha kwenda mahabusu ya Gereza Kuu la Kisongo lililoko mkoani hapa, baada ya kuwekewa na pingamizi la dhamana.
Wakati mbunge huyo akiondoshwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi, Lema aliinua juu Biblia huku akionekana kujiamini na ndipo wafuasi wa Chadema walipiga mayowe na kuangua vilio kwa ajili yake.
Awali, Lema ambaye alikamatwa usiku mjini Dodoma wiki iliyopita, alikokuwa akihudhuria vikao vya Bunge kabla ya kusafirishwa mpaka Arusha, alikuwa amesomewa mashtaka katika kesi mbili zilizofunguliwa dhidi yake, zote za tuhuma za kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais.
Alidaiwa kusema: "Nchi hii haitatawalika na itaingia kwenye machafuko iwapo Rais hatafuata katiba na sheria."
Lema aliamriwa kwenda mahabusu mpaka keshokutwa, kesi itakapotajwa tena na kutolewa uamuzi mdogo iwapo apatiwe dhamana au la.
Hatua hiyo ilitokana na mabishano ya kisheria kuhusiana na dhamana, baada ya mawakili wa serikali wakiongozwa na Maternus Marandu na Paulo Kadushi kupinga Mbunge huyo kuachiwa kwa dhamana.
Upande huo wa Jamhuri ulidai iwapo Lema atapewa dhamana, ataenda kuendelea kufanya mikutano ya hadhara ya uchochezi.
Aidha, Jamhuri ilitaka Lema anyimwe dhamana kwa sababu uchunguzi unaonyesha alipewa dhamana katika kesi zingine za uchochezi zinazomkabili mahakamani hapo na kwenda kurudia makosa yanayofanana kila mara.
Jopo la mawakili wanne wanaomtetea mtunga sheria huyo la John Mallya, Sheck Mfinanga, Ahmed Hamis na Charles Adiel, lilisema mshtakiwa ana haki ya kupata dhamani ukizingatia kesi inayomkabili bado uchunguzi wake haujakamilika.
Aidha, mawakili hao walisema Lema ana haki ya kupewa dhamana kulingana na sheria na katiba na kwa kuwa mtuhumiwa ni Mbunge, hivyo mahakama ina wajibu wa kumpatia dhamana ili kuendelea na majukumu ya wananachi waliomchagua.
MBUNGE WA TATU
Ndani ya mwaka huu, Lema anakuwa Mbunge wa tatu wa Chadema kukamatwa na polisi na kusafirishwa kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kujibu tuhuma mbalimbali.
Machi, mwaka huu, Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, alikamatwa na polisi jijini Mwanza kwa tuhuma za kukaidi wito wa kuhojiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na alilazwa rumande na siku iliyofuatwa alisafirishwa kwa ndege mpaka Dar es Salaam.
Pia Agosti, mwaka huu, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alikamwata mkoani Singida muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na kusafirishwa usiku huo mpaka Dodoma.
Alilazwa rumande mkoani humo na kesho yake alifikishwa Dar es Salaam kuhojiwa kwa tuhuma za kutoa kauli za uchochezi

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top