Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

MAUZAUZA MAZITO YAMKUMBA MGOMBEA UBUNGE CCM JIMBO LA PERAMIHO AANGUKA ABEBWA NA MACHELA KWENDA MUHIMBILI

MGOMBEA Ubunge kupitia CCM wa Jimbo la Peramiho Razalo Bunungu ameanguka ghafla chooni nyumbani kwake  eneo la seedfarm manispaa ya songea wakati alipokuwa ameenda kujisaidia.
 
Habari zilizopatikana mjini songea ambazo zimedhibitishwa na mke wake Judith Mlelwa zimesema kuwa tukio hilo lilitokea  juzi majira ya saa 5 asubuhi nyumbani kwake na kwamba kwa sasa hivi hali yake mbaya na imealazimika kumkimbiza hospitali ya rufaa ya muhimbili kwa matibabu.
 
Mlelwa alisema kuwa aliamka akiwa salama na baada ya kupata kifungua kinywa alikwenda kwenye ofisi za CCM wilaya ya songea kuangalia ratiba ya kampeni ya uchaguzi ndani ya chama ambayo inatarajiwa kuanza jana asubuhi katika kata ya Maposeni peramiho.
 
Alisema kuwa baada ya kutokea tukio hilo aliwasiliana na ndugu zake wa karibu na kuwajulisha tukio hilo na baadaye waliwasiliana na katibu wa ccm wa wilaya songea ambaye walimjulisha kuwa Bunungu hali yake ni mbaya baada ya kuanguka chooni.
 
Kwa upande wake katibu wa CCM wa wilaya hiyo Rajabu Uhonde alisema kuwa Ofisi yake imepokea taarifa ya tukio hilo na kwamba kwa sasa hivi wanasubiri utaratibu namna ya kwenda kumuona licha ya kuwa wameambiwa kuwa alikuwa anafanyiwa mpango wa kusafirishwa kwenda muhimbili.
 
Uhonde alifafanua zaidi kuwa katika jimbo la peramiho makada watatu akiwemo aliyekuwa waziri wa wizara ya sera na uratibu Bungeni Jenista Mhagama walichukua Fomu kwa ajili ya kugombea ubunge kwenye jimbo hilo lakini mmoja kati ya hao fomu yake ilikatwa kwa kuwa haikusainiwa na mgombea.
 
Aliwataja waliochukua fomu kwenye jimbo hilo kuwa ni Jenista Mhagama, Razalo Bunungu ambaye ni mtumishi wa Tanroads Tanga na mfanyakazi wa Bank ya NMB tawi la Tunduru Cremence Makabuli Mwinuka  ambaye fomu yake ilitupiliwa mbali kwa kosa la fomu yake ya kuomba kugombea ubunge kusainiwa na Mtu mwingine.
 
Hata hivyo Uhonde alisema kuwa licha ya kuwa mgombea Bunungu anaumwa ratiba ya kampeni inabaki kama ilivyopangwa na ilitarajiwa kuanza  jana asubuhi katika kata ya Maposeni peramiho. Na Gideon Mwakanosya- jamvilahabari.com

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top