Zikiwa zimebaki wiki takribani wiki 5 kabla ya dirisha la usajili barani ulaya halijafungwa, kocha wa Manchester United – Louis van Gaal amesema kwamba klabu yake ipo sokoni kutafuta mshambuliaji wa kumsajili kabla muda wa usajili haujaisha – huku akisisitiza mchezaji anayemtaka bado hajaandikwa na vyombo vya habari.
Van Gaal pia amethibitisha kwamba golikipa David de Gea ataukosa mchezo wa pili wa majaribio wa United huko Marekani kutokana na majeruhi yanayomsumbua.


Post a Comment