Gabriel Ng’osha na Mtandao
Funga kazi! ‘Dege’ kubwa la kijeshi la B-52 Stratofortress la Marekani lililotua nchini Kenya kwa ajili ya ulinzi wa Rais Barack Obama limetumika kulisambaratisha kundi haramu la kigaidi la Al-Shabaab lenye maskani yake nchini Somalia, Ijumaa Wikienda lina data.
Dege hilo la kivita liliwasili nchini Kenya hivi karibuni kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa kutosha kwa Rais Obama aliyefanya ziara nchini humo wikiendi iliyopita kabla ya kuelekea nchini Ethiopia.
Kwa mujibu wa habari za kiitelejensia kutoka Jeshi la Kenya, mbali na ndege hiyo, Jeshi la Marekani liliegesha manoari ya kivita inayoitwa Abraham Lincolin (jina la rais wa 16 wa Marekani) kwenye Pwani ya Mombasa katika Bahari ya Hindi kwa ajili ya ulinzi kwa nchi hiyo na Ukanda wa Afrika Mashariki.
Ilielezwa kwamba, ndege hiyo iliegeshwa kwenye eneo maalum la nchi kavu huko Lamu, Mombasa ikiwa na silaha nzito zilizotumika kuwapiga A-Shabaab.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la The British Broadcasting Corporation (BBC), hivi karibuni Jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi mfululizo kutokea Pwani ya Mombasa na kufanikiwa kuwasambaratisha Al-Shabaab waliodhaniwa wangeweza kuharibu usalama katika ziara hiyo ya Obama aliyetua usiku wa Ijumaa iliyopita.
Uchambuzi wa ndege hiyo unaeleza kuwa, ina uwezo wa kutoa huduma ya kuzalisha umeme hata kama shirika la umeme la nchi husika litakata au kutatokea dharura.
Ilidadavuliwa kwamba, ina uwezo wa kukata umeme moja kwa moja bila kusubiri kukimbilia kwenye mitambo yake huku ikipaa gizani bila kuwasha taa.
Pia data zinaonesha kuwa Ndege ya B-52 ambayo imetua Afrika kwa mara ya kwanza ina injini nane tofauti ya zilizozoeleka kuwa na injini mbili.
Ilielezwa kwamba, ina uwezo wa kurusha mabomu kama mvua ikiwa angani kwa kwenda mbele na chini huku baadhi ya makombora yakiwa na uwezo wa kugeuza ardhi ya chini kuja juu na ya juu kwenda chini.
Inakadiriwa zaidi ya wanajeshi 800 wa Kimarekani, 2,000 wa Kenya waliohusika kulitawanya kundi hilo hatari ambapo hadi sasa jamaa hao hawafahamiki walipo huku uwezekanao wa kuendelea kuwepo ukiwa ni mdogo kutokana na kipigo walichokipata.
Ziara ya Rais Obama ilitumia siku tatu kwa nchi hizo mbili huku akitumia saa 8 nchini Kenya ambako alihudhuria Kongamano la Ubunifu wa Kibiashara Ulimwenguni la 2015 lililokuwa likifanyika jijini Nairobi lililohusisha wajasiriamali kuzungumzia suala la kupambana na ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu. Kuwajua vizuri Al-Shabaab ni nani na kazi wanazofanya, usikose kusoma Gazeti la Risasi Jumamosi wiki hii.


Post a Comment