Wagombea hao; Juma Killimbah, David Jairo na Amon Gyunda walisema mjini hapa jana kuwa, baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, wanamfanyia kampeni za wazi Nchemba, ili apitishwe kuwa mgombea ubunge kwa jimbo hilo.
Nchemba ni Naibu Waziri wa Fedha, aliyekuwa miongoni mwa wana CCM 38, walioingia katika kinyang'anyiro cha kuomba chama hicho kiwachague kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi wa Oktoba.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Killimbah alisema, wamekubaliana kuchukua hatua hiyo endapo mchezo unaofanywa 'kumbeba' Nchemba utaendelea na kuathiri demokrasia ya kugombea na kuchaguliwa kwa kura halali.
Alisema kuwa, Msimamizi wa Uchaguzi katika kura hizo za maoni katika jimbo hilo, Mathias Shidagisha na Msaidizi wake, Mwita Rahael walikuwa miongoni mwa wanaombeba Waziri huyo.
Pia, alisema kuwa, mgombea mwenzao huyo amekuwa akivunja kwa makusudi kanuni na taratibu za mchakato wa kura za maoni, bila kuchukuliwa hatua yoyote.
Miongoni mwa mambo yanayo lalamikiwa ni pamoja na msimamizi huyo kutumia gari la Nchemba kumsambazia mabango yake kwenda katika kata mbalimbali.
Jambo lingine ni kitendo cha Msimamizi huyo kupita kwa makatibu kuwataka wahakikishe Nchemba anashinda.



Post a Comment