
Mchakato wa kura za maoni ukiwa unapamba moto kwa wagombea wa nafasi za ubunge ndani ya CCM, tuhuma za rushwa nazo zimejitokeza kwa vigogo ndani ya chama hicho.
Wakati huohuo habari kutoka Same zinaripoti Mbunge wa CCM Same Mashariki Anna Kilango inadaiwa alikamatwa na polisi jana usiku majira ya saa 5 usiku katika eneo la Dimbwi kijijini cha Bagamoyo, kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa wapiga kura. Mtoa taarifa wetu alisema kuwa Anna alikuwa anashikiliwa katika kituo cha polisi cha Gonja.
Vile vile mpambe wa Anna aliyejulikana kwa jina moja la Nuru juzi alimvamia dereva wa mgombea mmoja na kumpiga kwa kumtuhumu kuwa na bahasha za kuwagawia wapigakura, Nuru nae alikamatwa na kuwekwa ndani hata hivyo yuko nje kwa dhamana.



Post a Comment