Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho leo majira ya saa 5 asubuhi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandsihi wa Lipumba amesema ametafakari sana katika kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho lakini dhamira yake inamsuta.
Amesema kuwa mwaka 2014 hakutaka kugombea nafasi hiyo kutokana na mchakato wa katiba mpya akaamua kugombea kwa lengo ya kuwapa watanzania katiba itakayoindoa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lipumba amesema katika mchakato wa bunge maalumu wakaunda umoja wa katiba wenye lengo wa kusimamia katiba iliyopendekezwa lakini sasa waliopitisha ndio wanataka kuisimamia katiba hiyo ambayo haingii akili.
Amesema alikuwa akishiriki vikao vya UKAWA lakini Aprili 1 mwaka huu alisema atangatuka katika nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Wanannchi (CUF).
Amesema amepita katika misukosuko mingi katika kukijenga chama hadi kufikia leo kabambikiziwa kesi ya kufanya maandamano bila kibali.
Lipumba amesema kazi yake atakuwa mwanachama wa kawaid, kufanya utafiti wa maendeleo endelevu pmoja na kufanya ushauri wa masuala mbalimbali katika chama hicho.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza ngumza na waandishi wa habari kuhusiana na kung'atua rasmi umwenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wakawaida wa chama hicho ikiwa atakuwa mwanachama halali kwani kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020 hayo ameyasema katika ukumbi wa mikutano wa Peacock hoteli jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Iblahimu Lipumba akitanga kujihuzuru wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Rasmu ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akikusanya makabrasha yake mara baada ya kumaliza mkutano wa kujivua uanachama wa chama cha CUF taifa katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


Post a Comment