Dr. Juma Mwaka (kushoto) akimkabidhi kombe la Ndondo Cup nahodha wa Faru Jeuri Selemani Bujji baada ya timu yake kutwaa ubingwa wa michuano hiyo
Baada ya michuano ya Sports Xtra kufikia tamati siku ya Jumapili ambapo bingwa mpya wa michuano hiyo ni Faru Jeuri kutoka mitaa ya Vingunguti walioifunga timu ya Kauzu FC ya Temeke kwenye mchezo wa fainali iliyopigwa kwenye dimba la Bandari.
Mbali na zawadi kwa timu zilizofanya vizuri kwenye michuano hiyo kwa kushika nafasi tatu za juu, pia kulikuwa na zawadi kwa wachezaji pamoja waamuzi waliofanya vizuri kwenye michuano hiyo. Zawadi hizo ni kwa mchezaji bora, mfungaji bora pamoja na mwamuzi bora huku kukiwa na zawadi kwa kikundi bora cha ushangiliaji ambapo kila mshindi anajichukulia shilingi laki tano (500,000).
Mchezaji bora wa Ndondo Cup
Zawadi hii imechukuliwa na Idd Mwalala kutoka Makumba FC baada ya kamati ya mashindano kujiridhisha na kiwango kilichooneshwa na mchezaji huyo kwenye michezo yote aliyoichezea timu yake.
Mfungaji bora wa mashindano ya Ndondo Cup
Baada ya awali kutangazwa Ally Kalulu wa Kauzu FC na Idd Mwalala wa Makumba FC kufungana kwa kufunga mabao manne kila mmoja, kamati ya mashindano imepitia ripoti za mechi za timu zote na kujiridhisha kuwa, Idd Mbaga wa Keko Furniture ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi akiwa amefunga magoli matano (5) hivyo kuibuka mfungaji bora.
Mwamuzi bora wa mashindo
Zawadi ya mwamuzi bora imekwenda kwa Jackson Mshirombo baada ya kamati ya mashindano kurihishwa na kiwango kilichooneshwa na mwamuzi huyo kwenye michezo yote alizochezesha kwenye michuano ya Ndondo Cup 2015.
Kikundi bora cha ushangiliaji
Kikundi cha ushangiliaji cha timu ya Kauzu FC chini ya uongozi wa Chief ‘Ostadh’ ambaye alikuwa mbele kwa kuishangilia timu yake tangu kuanza kwa michuano hiyo hadi siku ya fainali ya Ndondo Cup.
Zawadi kwa timu zilizofanya vizuri kwenye mashindano hayo
Bingwa wa Ndondo Cup 2015
Timu ya Faru Jeuri ndio imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ndondo Cup 2015 na kupata zawadi za medali, kombe na fedha taslimu shilingi milioni tano (5,000,000).
Mshindi wa pili
Kauzu FC imemaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye michuano ya Ndondo Cup mwaka huu na kufanikiwa kupata medali na fedha taslimu shilingi milioni tatu (3,000,000).
Mshindi wa tatu
Nafasi hii imechukuliwa na Makumba FC ambao wamejinyakulia shilindi milioni mbili (2,000,000).
Utaratibu wa kukabidhi zawadi zao unaandaliwa na katika siku za usoni wataitwa wahusika wote ili kukabidhiwa zawadi zao za fedha taslimu.


Post a Comment