Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KILIO KIKUBWA!!!! ..JAMES MBATIA ATIMULIWA NA WANACHAMA WAMKATAA, HILI HAPA TUKIO ZIMA




WAGOMBEA udiwani kupitia CHADEMA, Jimbo la Vunjo, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, wamesema hawapo tayari kumuunga mkono mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, anayewakilisha UKAWA, Bw. James Mbatia.

Walidai Bw. Mbatia amekiuka makubaliano ya umoja huo, hivyo watampigia kampeni mgombea urais wa UKAWA, Edward Lowassa lakini si mbunge wao ambaye amekuwa akiwapiga vita wagombea udiwani kwa tiketi ya CHADEMA.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, walisema Bw. Mbatia amekiuka makubaliano na kusimamisha wagombea udiwani katika kata 16 za jimbo hilo jambo linalowanyima fursa wagombea udiwani kutoka chama   chao.

Akizungumzia msimamo huo, Fredy Shayo 'kisauti', anayegombea udiwani kupitia CHADEMA, Kata ya Mamba Kusini, alidai UKAWA katika jimbo hilo upande wa udiwani hawajaridhiana jambo ambalo ni hatari kubwa kwa umoja huo.

"Tulikaa vikao na kamati ya utendaji NCCR-Mageuzi zaidi ya mara saba ili kutafuta maridhiano ya kuzigawa hizi kata lakini wenzetu hawataki, nasi hatuwezi kuziacha kata zote kwa NCCR-Mageuzi kwa sababu tuna vigezo, msimamo wetu ni kusonga mbele," alisema.

Mgombea mwingine Beatrice Mtuy, (Kata ya Marangu Magharibi), alidai Bw. Mbatia alianza kuwabagua tangu alipozindua kampeni zake Septemba 5, mwaka huu.

Katibu Mwenezi wa CHADEMA jimboni humo, Charles Kawiche, alisema ni vyema Bw. Mbatia akaondoa mkanganyiko uliopo kwani hauleti picha nzuri katika umoja huo hasa jimboni humo.

Katibu wa chama hicho mkoani humo, Basil Lema, alisema chama hakiungi mkono wagombea udiwani kumsusa Bw. Mbatia ambaye ndiye mgombea ubunge na hawaungi mkono wagombea udiwani kubaguliwa.

Gazeti hili lilimtafuta Bw. Mbatia ili aweze kuzungumzia msimamo wa wagombea udiwani wa CHADEMA lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top