Jana usiku hatimaye mashabiki wa Chelsea wamepata tena smile baada ya muda kidogo kupitia mambo ambayo ni magumu kwao kama mashabiki wa club hiyo.
Baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv, Chelsea watakua kwenye maandalizi ya mechi ngumu kwenye EPL dhidi ya Arsenal. Kwenye mechi hiyo ni kwamba wachezaji Willian na Pedro hawatacheza kutokana na sababu tofauti.
Kwenye taarifa iliyotolewa na Chelsea inasema kwamba “Jose Mourihno ataanza kufikiria kuhusu mechi ya Arsenal kuanzia leo, lakini amesema kwamba Willian na Pedro hawatakuwepo kwenye kikosi”
Siku ni jumamosi kila kitu mambo hadharani nani mbabe kati ya hawa wawili. Endelea kunifuatilia utajua kila kitu kuhusu hii mechi.


Post a Comment