Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

UKAWA WAJA JUU KWA KAULI ZA RAY (VINCENT KIGOSI) NA HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MSANII HUYO

Vincent Kigosi ‘Ray’ 
Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameendelea kushusha maneno kwa chama kinachounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) baada ya kufunguka hadharani kuwa hawakuwa na sera ambazo zingemfanya aendelee kubaki.

Staa huyo ambaye kwa sasa amerudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kurudi kwake CCM hakumaanishi kama amehongwa kama watu wanavyoendelea kusambaza habari hizo bali amekwenda kutokana na kuvutiwa na sera.

“Naomba nieleweke kuwa dhamira yangu ya kubaki Ukawa ndiyo ilikuwa ikinisuta. Nikiwa kama mmoja wa wasanii, nimevutiwa na sera za CCM hasa kwa upande wa wasanii ambapo Mgombea Urais, Magufuli (John Pombe) alisema moja ya sera zao ni kujali maslahi kwa wasanii na kuwafungulia mfuko maalum utakaowashughulikia,” alisema Ray.

1 comments:

Sera za Lowassa ni za danganya toto.

Anasema ataanzisha viwanda vya serikali. Anaebisha atizame Ufaransa.

Reli zote serikali, mandege ni yote serikali na nyumba zote ni za serikali.

Hivi Lowassa ameona wapi duniani reli isiyo ya serikali?

Mashirika ya ndege makubwa ni kawaida kuwa chini ya serikali.

Nyumba za serikali zimeuzwa sana Ufaransa mwaka 2012. Serikali ikajichukulia mapato.
Je ufaransa kuna viwanda vya serikali?

Lowassa anataka kuondoa umasiki kwa kufungua benki ya waendesha bodaboda. Really?
Ni wapi kwingine duniani kuna benki ya hivyo.

Nilitegemea apige marufuku bodaboda kwa jinsi zinavyouwa watu na kuwapa vilema. Yeye ndio anaona achukue kura hapo kwenye suala la bodaboda. Na apande bodaboda Ubungo - Posta wiki mbili tuone uzalendo wake.

Reply

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top