Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

HABARI YA HIVI PUNDE:..KIGOGO HUYU MKUBWA SERIKALINI ATIMULIWA KAZINI LEO NA AMEAMBIWA ASIRUDI TENA>>>>SOMA HABARI KAMILI

Waziri wa maliasili na utalii Prof Jumanne Maghembe amemsimisha kazi mkurugenzi wa mipango na matumizi ya rasilimali wa wakala wa misitu nchini Bwana Mohamed Kilongo kutokana na kushindwa kuwasimamia maafisa maduhuri ambao wameshindwa kukusanya na kuwasilisha maduhuri ya serikali.
Akimsimamisha kazi mbele ya mkutano na wafanyakazi wa wizara hiyo, waziri Prof Maghembe amechukua hatua hiyo kutokana na uzembe katika usimamizi wa rasilimali za wakala huo, ambapo amemwagiza mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali-CAG- kupitia upya vitabu vyote vya mapato ya wakala huo wa misitu nchni baada ya kubaini kuwepo kwa maafisa maduhuli hawajawasilisha fedha za serikali kwa zaidi ya miaka kumi na mbili.
 

Katika hatua nyingine Prof Maghembe amewataka maafisa wa wakala wa misitu waliopanga ofisni nje ya jengo la wakala wa misitu kurudi haraka katika jengo la mpingo zilizo ofisi za wizara ya maliasili ya utalii ndani ya siku saba kaunzia januari tano ikiwa na pamoja kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa kuipa hasara serikali.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top