Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

KILOSA TENA: Kaya zaidi ya 1,500 hazina pa kuishi Baada ya Nyumba Zao Kujaa Maji na zingine Kusombwa na mafuriko.

Kaya 1,500 katika kata ya Magomeni wilayani Kilosa hazina makazi baada ya nyumba zao zaidi ya 250 kubomoka na nyingine 500 kujaa maji baada ya mvua iliyo nyesha usiku kwa saa nne kusababisha mafuriko makubwa katika kata hiyo ambapo wananchi wamelazimika kujihifadhi chini ya miti na majengo ya shule jirani.
Wakizungumza kwa masikitika wananchi hao wametupia lawama serikali kuahidi kujenga matuta ya mto Mkondoa ambayo yatazuia maji pande mbili badala yake wamejenga tuta moja ambalo ndilo linalo sababisha mafuriko kuingia katika kata ya Magomeni ambapo wameiomba serikali kuwasaidia kwani makazi, nguo pamoja na vyakula kwakuwa vyote vimebebwa na maji.
 
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Morogoro Devota Minja amefika katika eneo hilo na kukuta wananchi wakiwemo watoto wadogo wakiwa hawana pakwenda ambapo amewataka wale wote waliobaki kwenye nyumba zao watoke wakati serikali ikiangalia jinsi ya kuwasaidia wananchi hao huku diwani wa kata ya Magomeni Abdallah Uweli akisema wananchi hao wanahitaji msaada wa haraka kwakuwa hasara waliyoipata ni kubwa.
 

ITV

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top