Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

DONALD TRUMP ATAKA UCHAGUZI WA KUTEUWA MGOMBEA URAIS LOWA URUDIWE

Aliyekuwa miongoni mwa wanaowania nafasi ya
Iowa. Aliyekuwa miongoni mwa wanaowania nafasi ya kuteuliwa kugombea urais nchini Marekani Donald Trump amesema uchaguzi wa mchujo wa kuteua atakayewania urais kupitia Chama cha Republican katika Jimbo la Iowa urudiwe.
Trump alisema aliyetangazwa kuibuka mshindi Ted Cruz alitumia udanganyifu.
Alisema wakati wa kikao cha Iowa, maofisa wa kampeni wa Cruz waliwaambia wapigakura kwamba mgombea mwingine Ben Carson alikuwa amejitoa kwenye kinyang’anyiro hicho, jambo ambalo halikuwa kweli.
Maofisa wa kampeni wa Cruz walimuomba radhi Carson, wakisema lilikuwa kosa.
Trump alishika nafasi ya pili katika mchujo huo wa kwanza kufanyika nchini humo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Mchujo utakaofuata utafanyika New Hampshire wiki ijayo.
“Ted Cruz hakushinda Iowa, aliiba ndiyo sababu alipata kura nyingi kuliko ilivyotarajiwa. Ni vibaya!” alisema Trump. Awali, alikuwa ameandika kwenye Twitter kwamba Cruz alishinda mchujo wa Iowa kwa njia haramu, lakini baadaye akafuta ujumbe huo.
Matamshi ya Trump ni kinyume na hotuba yake ya kukubali kushindwa ambayo aliitoa Jumatatu usiku baada ya matokeo kujulikana, jambo ambalo lilishangaza wengi.
Awali, wakiwa kwenye mdahalo Trump alimshambulia Cruz akisema, hafai kuwa Rais wa Marekani.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top