Loading...
http://go.ad2up.com/afu.php?id=778977

Jukwaa la Wahariri lalaani kupigwa mwandishi



Mwinyi Kazimoto
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) lalaani kupigwa na kuumizwa kwa mwandishi wa Mwananchi, Mwanaiba Richard.
Katika Tamko lao walilolitoa leo, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Theophil Makunga amesema mwandishi huyo alipigwa na mchezaji wa Klabu ya Simba Mwinyi Kazimoto wakati akitimiza majukumu yake Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga Jumatano wiki hii.
Makunga amesema Kazimoto alimshambulia mwandishi huyo kwa ngumi na mateke huku akimtuhumu kwamba aliwahi kumwandika vibaya gazetini. Alisema tukio hilo ambalo siyo la kiuanamichezo lilitokea mbele ya viongozi wa Simba na wachezaji wengine.
“TEF inalaani kitendo cha Kazimoto kumshambulia mwandishi wa habari akiwa kazini kwa kuwa kitendo hicho ni mwendelezo wa ukiukaji wa haki za mwandishi kufanya kazi zake kwa uhuru bila kutishwa, kubughudhiwa au kupigwa. Kumpiga mwandishi wa habari ni kitendo cha kijinai, pia kinajenga hofu kwa waandishi ili wasifanye kazi yao kwa uhuru,” alisema Makunga.
Kutokana na kitendo hicho, Jukwaa hilo la Wahariri limeutaka uongozi wa Simba na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya Kazimoto ili kuepusha kuibua mgogoro kati ya wanahabari kwa upande mmoja na klabu yake pamoja na TFF kwa upande mwingine.
Aidha, Makunga amewataka wanamichezo na wananchi kwa ujumla kuchukua hatua za kisheria au kulalamika kwa chombo cha habari husika au kulalamika kwenye Baraza la Habari Tanzania (MCT) kama hawatendewi haki.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright JAMIIYETU | Designed By BAKI NASI
Back To Top