RAIS John Magufuli amekutana na Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki na kuzungumza masuala mbalimbali kuhusu Umoja wa Afrika (AU) Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Pamoja na kuzungumzia masuala yahusuyo umoja huo, Mbeki alimpongeza Dk. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbeki pia alipongeza Rais Magufuli kwa juhudi kubwa alizozifanya katika uongozi wa nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja madarakani.
Kwa upande wake Rais Magufuli alimshukuru Mbeki kwa kumtembelea na kufanya naye mazungumzo na pia akampongeza kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Usomi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wiki iliyopita


Post a Comment