Muziki wa Tanzania unazidi kufanya vizuri kwenye nchi za Kiafrika mtu wangu. TumeonaVanessa Mdee na Diamond Platnumz wakiiwakilisha Tanzania vizuri kwenye chati mbali mbali za redioni na Tv Africa, wakachaguliwa kwenye Tuzo za MTV MAMA Awards 2015ambazo Diamond Platnumz alirudi na ushindi wa Tuzo moja ya Best Live Act.
Good news kwako mtu wangu, wasanii wa Tanzania wanazidi kuonekana kwenye countdown za shows mbalimbali mmoja wao akiwa Superstaa wa Bongo Fleva Ommy Dimpoz.
Wiki hii Ommy Dimpoz ameshika namba moja kwenye countdown ya Soundcity Top Ten East na wimbo wa Wanjera hii ni good news kwa Watanzania kwa msanii mwengine waBongo Fleva kuonekana kwenye nafasi ya namba moja.


Post a Comment