Baada ya kufanya vurugu kwa muda kwenye ofisi hizo za wilaya za chama cha mapinduzi mjini sumbawanga,ndipo katibu wa CCM wa wilaya ya Sumbawanga mjini Bw.Gabriel Kiula alipojitokeza na kutangaza matokeo hayo, ambapo amesema aliyeongoza ni mbunge anayemaliza muhula wake mheshimiwa aeshi hilal kwa kupata zaidi ya kura 13,500, na kuwabwaga wagombea wenziwe kumi waliojitokeza mwaka huu.
Kufuatia matangazo hayo baadhi ya vijana wakaibuka na kutaka jina la kiongozi wao huyo lirudishwe bila ya kukatwa, kwa vile ameshinda kwa kishindo, na kutishia kujiondoa kwenye chama, huku mheshimiwa aeshi hilal akiwaomba vijana hao wawe na moyo wa subira na uvumilivu, na kuwashukuru kwa kuonyesha imani kwake.


Post a Comment